Takwimu hazidanganyi; ukimpanga Diarra golini ujue tayari umeshafungwa goli 1

escrow one

JF-Expert Member
Nov 29, 2014
1,472
2,867
Kwa mujibu wa takwimu zinazotolewa na wachambuzi mbalimbali hapa nchini zinaonesha Mdaka Mishale huyu hajawahi kuonja utamu wa clean sheet tangu atue jangwani.

Ni sawa na kusema uwepo wa Diarra golini unafanya aliyebet OVER 0.5 kuweka dau la Milioni moja huku anachekelea.

Hivyo kwa haraka haraka ni kwamba kwenye ligi, Yanga tutafungwa magoli yasiyopungua 30 msimu ujao maana tutacheza mechi 30 za ligi.
 
Naona uwajui Dar Young Africans kweli na kuruhusu goal.

Clean Sheets Kwa Dar Young Africans Naziona Kama 20 Msimu Tunaoanza Kesho.
 
Unachozungumza inaweza kuwa ni sahihi lakini kwa wajuao mpira tumeona mpaka sasa amefsnya saves nyingi sana tena za one against one. Na magoli yametokana makosa ya mabeki wake wanaogezwa kama chapati
 
Unachozungumza inaweza kuwa ni sahihi lakini kwa wajuao mpira tumeona mpaka sasa amefsnya saves nyingi sana tena za one against one. Na magoli yametokana makosa ya mabeki wake wanaogezwa kama chapati
kama hali hii itaendelea tatizo linakuwa ili yanga tushinde au kudroo inabidi tuwe na uhakika wa kufunga angalau bao 2 kila mechi kuziba mapengo.
 
Diarra atawauwa watu mwaka huu. Maana ajaanza hata mechi moja ya Ligi lakini amekwisha anzishiwa Uzi kama 8 hivi humu ndani.
 
Huyu kipa ni Ovyo kweli, Metacha was a good goalkeeper, ila kiburi chake tu ndio tatizo. Huyu wa mishale hata simuelewi kabisa
 
Logic ya mleta mada iko hivi. Kama yanga atanarajiwa kumaliza ligi akiwa amefungwa magoli 30 basi ni sawa na kusema Yanga SC itamaliza chini ya nafasi 7 katika msimamo wa Ligi 2021/22.

Kwa Yanga SC hii ya Djuma, Makambo, feisal, Aucho, Mukoko, Diarra yaani imalize chini ya nafasi 7 ktk msimamo.
Capture.JPG

Hapo juu ni picha ikionyesha alama nyekundu ambazo ni nafasi za timu zilizo concede magoli kuanzia 30.

Asante Kwa Uchambuzi.
 
Huyu kipa ni Ovyo kweli, Metacha was a good goalkeeper, ila kiburi chake tu ndio tatizo. Huyu wa mishale hata simuelewi kabisa
Ina maana wewe ndio unajua kumchambua Diarra kuliko kocha wa timu ya Taifa ya Mali (ambayo ni timu bora ya taifa namba 9 africa).?
 
Asante kwa uchambuzi makini ila kipa ndo aachwe kufungwa kila mechi sasa, vinginevyo tutakuwa kama hizo timu.
 
asante kwa uchambuzi makini ila kipa ndo aachwe kufungwa kila mechi sasa, vinginevyo tutakuwa kama hizo timu.
Ubora wa Kipa sio idadi ya magoli aliyo fungwa.

Kuna aspects ambazo zinamfanya kipa kuendelea kuwa kipa bora hata kama anafungwa kia mechi. Leo hii ata Manuel Neuer akidakia Ndanda ni lazima afungwa kila mechi licha ya Ubora wake. Hii ni kutokana na ubora wa kipa unategemea factors tofauti tofauti.

Mfano wa factors zinazochangia Diarra kuwa goikipa bora ni kama zifuatazo:-
1. Uwezo wake wa ku-bypass hard pressing.
2. Kuharakisha transition ya mashabulizi kutoka defensive na kuwa offensive.
3. Ni mtulivu na mwenye uwezo wa ku-maintain umiliki wa mpira.
4. Proactiveness(Kutambua hatari na kuikabiri kwa haraka zaidi) yake ni ya hali ya juu kuliko kipa yeyote yule tanzania. kumbuka zile one-on-one.

Mfuatilie Diarra kwa jicho la kiufundi zaidi utagundua jambo.
 
Logic ya mleta mada iko hivi. Kama yanga atanarajiwa kumaliza ligi akiwa amefungwa magoli 30 basi ni sawa na kusema Yanga SC itamaliza chini ya nafasi 7 katika msimamo wa Ligi 2021/22.

Kwa Yanga SC hii ya Djuma, Makambo, feisal, Aucho, Mukoko, Diarra yaani imalize chini ya nafasi 7 ktk msimamo.
View attachment 1948575

Hapo juu ni picha ikionyesha alama nyekundu ambazo ni nafasi za timu zilizo concede magoli kuanzia 30.

Asante Kwa Uchambuzi.
app gani hii mkuu
 
Back
Top Bottom