TAKUKURU yazindua Huduma mpya ya 'LONGA NASI'

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
160524102535_corruption_tanzania_longa_nasi_640x360_bbc.jpg


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania imezindua huduma mpya katika juhudi za kuimarisha vita dhidi ya rushwa nchini humo.

Kupitia huduma hiyo iliyopewa jina Longa Nasi, wananchi wataweza kutoa taarifa kuhusu visa vya ulaji rushwa kupitia simu za mkononi.

Anayetoa taarifa anaweza kuwapasha maafisa kwa kupiga simu au kwa kutuma ujumbe mfupi kwa nambari maalum.

Huduma hiyo inatumika katika mitandao yote ya simu bila malipo.

Rais wa Tanzania John Magufuli aliahidi kukabiliana vikali na ulaji rushwa wakati wa kampeni na amekuwa akiwafuta kazi baadhi ya maafisa wakuu serikalini kwa tuhuma za kuhusika au kutozuia ufisadi.

Desemba mwaka jana, alitengua uteuzi wa mkuu wa Takururu Dkt Edward Hoseah kutokana na “kutoridhishwa na namna taasisi hiyo ilivyokua ikitekeleza wajibu wake katika kukabiliana na rushwa hususani kwenye upotevu wa mapato ya serikali katika bandari ya Dar es salaam.”

Dkt. Magufuli amesifiwa na baadhi ya mashirika na viongozi kutoka nje kwa juhudi zake kukabiliana na rushwa.

Majuzi, Dkt Magufuli alipohudhuria sherehe ya kuapidhwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, kiongozi huyo wa Uganda alisema hatua zake zimerahisisha shughuli mpakani .

"Napenda kasi yako ya uongozi, napenda jinsi unavyopambana na rushwa, kwa sababu rushwa ilikuwa inazaa matatizo mengine kama vile ucheleweshaji wa mizigo bandarini na vikwazo vya mpakani, hivyo nakupongeza sana kwa hilo,” alisema Bw Museveni.
 
Sasa kupitia Airtel,unaweza kutoa taarifa za Rushwa bure kwa kupiga 113 au *113# na zitapokelewa TAKUKURU.Ukiwa na swali au maoni tuma SMS bure kwenda 113
 
Mleta uzi kamilisha taarifa maelezo yako ni nusu malizia basi. Tuwekee hizo namba, au umesikia watu wakiongea na wewe ukakurupuka
 
Usalama wa mtoa taarifa unakuwaje? Maana ukituma message si inaonesha nani katuma. Best way ni kutengeneza njia ya kukusanya taarifa anonymous yaani bila taarifa za nani katuma.

I can even help them if they want
 
Makamu wa Rais azindua mtandao wa kufichua wala rushwa kupitia mtandao wa Simu kwenda PCCB maarufu kwa jina la "longa nasi"
Source ITV Habari.

Tuanze na Lugumi.
Tuje Escrow
Tufuatie Meli Chakavu
Then Nyumba za umma
EPA
Rada
Richmond Dowans
Sukari

Ongezeni wadau.....
 
Hizo naona ni sarakasi na kutaka kuwakwepa wanaofilisi nchi kwa rushwa kubwa. Hivi unaweza kweli tumia "Longa Nasi" kwa issue ya Escrow au Lugumi au Richmond au rushwa kwenye kamati za Bunge? Manesi, madactari, polisi na watumishi wa kawaida ndio walengwa wakubwa.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Hizo naona ni sarakasi na kutaka kuwakwepa wanaofilisi nchi kwa rushwa kubwa. Hivi unaweza kweli tumia "Longa Nasi" kwa issue ya Escrow au Lugumi au Richmond au rushwa kwenye kamati za Bunge? Manesi, madactari, polisi na watumishi wa kawaida ndio walengwa wakubwa.
PCCB haijafanya lolote kwenye Lugumi, Escrow, Meli Chakavu, Nyumba za Umma, na leo inakuja na Mitandao ya Simu. Huku ni kujipendekeza.
 
Katika mtandao yote inayotoa huduma hiyo ya kufichua wala rushwa sijaisikia Vodacom ikitajwa na valentine mlowola, MAMVII aligoma nini??? Au sikio linapancha halikuskia vizuri
 
Katika mtandao yote inayotoa huduma hiyo ya kufichua wala rushwa sijaisikia Vodacom ikitajwa na valentine mlowola, MAMVII aligoma nini??? Au sikio linapancha halikuskia vizuri
Lugumi
Lugumi
Lugumi
Lugumi
Lugumi
Lugumi
Lugumi
 
Mtoa mada we ni kichwa kwelikweli ! Hivi pale Ilboru ulikua bweni gani ? Mawenzi , kibo , oldonyo .
 
Makamu wa Rais azindua mtandao wa kufichua wala rushwa kupitia mtandao wa Simu kwenda PCCB maarufu kwa jina la "longa nasi"
Source ITV Habari.

Tuanze na Lugumi.
Tuje Escrow
Tufuatie Meli Chakavu
Then Nyumba za umma
EPA
Rada
Richmond Dowans
Sukari

Ongezeni wadau.....
Udalali wa vyama vya siasa
 
Back
Top Bottom