Takukuru yazidi kuitikisa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takukuru yazidi kuitikisa CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Jul 24, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Mbunge Limbu akamatwa, ahojiwa
  Diwani kortini, vigogo UVCCM matatani
  Nape alalamika kuhujumiwa Ubungo  [​IMG]
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Mnauye, akilalamika jukwaani baada ya msimamizi wa mkutano wa wagombea ubunge kupitia chama hicho Kata ya Manzese jijini Dar es Salaam, kumzuia kujibu swali aliloulizwa na mwanachama wa CCM.  Mchakato wa kampeni za kura za maoni ndani ya chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kuteua wagombea ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu, umeendelea kutawaliwa na matukio mengi, yakiwemo kuhojiwa mbunge kwa tuhuma za kutoa rushwa na wabunge wanaomaliza muda wao kubanwa kwa maswali na wapigakura.
  Mbunge ahojiwa na Takukuru
  Mbunge wa Magu, Dk. Festus Limbu, ambaye ni miongoni mwa wanaoomba uteuzi wa CCM kugombea katika jimbo hilo, alijikuta katika wakati mgumu baada kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma za kumpa mmoja wa wapiga kura Sh. 5,000 walipokutana njiani wakati wakitoka kwenye mchakato wa kura za maoni.
  Habari zimeeleza zinadai kuwa baada ya wagombea wenzake kuona akitoa fedha hizo, walimkamata Dk. Limbu pamoja na mpokeaji na kisha kupiga simu katika ofisi za Takukuru.
  Habari zinadai kuwa maofisa wa Takukuru walipofika katika eneo la tukio na wagombea wote akiwemo Dk. Limbu walikubali kutoa ushirikano na kwenda kwenye ofisi za taasisi hiyo kwa ajili ya mahojiano yaliyoanza saa mbili hadi saa tano usiku na baada ya mahojiano hayo, wote waliachiwa.
  Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Christopher Mariba, alithibitisha kuhojiwa kwa wagombea wote nane wa jimbo hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi na wagombea wenyewe na kwamba uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
  Alipoulizwa na Nipashe jana jioni kuhusiana na tuhuma hizo, Limbu alidai hakutoa fedha bali ilivumishwa ili kumchafulia jina lake.
  Hata hivyo, alithibitisha msafara wao kuhojiwa na Takukuru na kufafanua kuwa wakiwa wamesimama kuchimba dawa, wananchi walipita na kuomba fedha na mmoja wao alisogea kwenye gari lake na alipotoka alikimbizwa na baada ya kupekuliwa, alikutwa na kadi mbili za vyama tofauti.

  Makada watatu wahojiwa Lindi
  Viongozi watatu wa CCM Wilaya ya Lindi Mjini, jana walishikiliwa kwa muda na Takukuru kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.
  Habari za uhakika kutoka kwa baadhi ya wanachama ambao wanapenda haki na kuthibitishwa na Naibu Kamanda wa Takukuru mkoani hapa, Charles Myava, ambaye hata hivyo, alikataa kufafanua, zinaeleza kuwa viongozi hao walikamatwa kwenye nyumba ya wageni iitwayo Machenza mjini Lindi.
  Viongozi hao (majina tunayo) walikamatwa majira ya saa 1:00 na 2:00 usiku.
  Baadhi ya mashuhuda wameliambia gazeti hili kwamba viongozi hao walifika katika nyumba hiyo wakiwa na baadhi ya wanachama kwa lengo la kupanga mikakati ya kumuwezesha
  “Kwa kweli bado haijaweza kufahamika mara moja, walikuwa wapewe kiasi gani cha fedha, lakini baadhi ya wanachama walipogundua hali hiyo waliitonya Takukuru ambao walifika na kuwakuta,” alisema mmoja wa mashuhuda hao.
  Naibu Kamanda wa Takukuru mkoani Lindi, Myova, alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alithibitisha kuwakamata viongozi hao na kueleza kuwa taarifa kamili atazitoa leo.
  “Ni kweli viongozi hao tumewakuta wakiwa katika nyumba hiyo, lakini tunachowaomba tukutane kesho (leo) tutawapeni taarifa kamili,” Myava.
  Katibu wa CCM mkoani Lindi, Albert Mgumba, hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa maelezo kuwa bado hajapata taarifa rasmi zaidi ya kusikia mitaani.
  “Hii taarifa ninaisikia kijuu juu tu, lakini kiofisi bado sijapewa rasmi, ninawaomba nipeni muda wakati naendelea kulifanyia kazi,” Mgumba.

  Diwani kizimbani Kigoma
  Takukuru Mkoa wa Kigoma, imemfikisha aliyekuwa Diwani wa Kata ya Muzye, Onesmo Hosen Kilatobetisye, kujibu mashtaka ya kutoa rushwa kwa wanachama wa CCM ili wamchague kwenye kura za maoni.
  Kamanda wake, Emmanuel Kiyabo, alisema mtuhumiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kasulu juzi na kusomewa mashtaka ya kutoa Sh. 20,000 kuwashawishi wanachama wamchague.
  Kiyambo,alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa wakati alitoa kiasi hicho kwa wanachama hao wa vikundi vya ngoma ya mshikamano na migongwa ambao ni vya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT).
  Alisema katika mkutano huo aliwapa kiasi hicho cha fedha kama kishawishi ili waweze kumpigia kura za maoni, jambo ambalo kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ni kosa la jinai .
  Hata hivyo, alisema mtuhumiwa huyo alikana shtaka hilo na kuachiwa kwa dhamana hadi Agosti 19, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

  Nape Nnauye alalamika
  Mgombea wa ubunge katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam, Nape Nnauye, amecharuka na kudai kuwa anahujumiwa na vigogo wa CCM ambao hawataki apate nafasi hiyo.
  Kadhalika, Nnauye amesema hana imani na kamati nzima inayosimamia mikutano ya kampeni ya wagombea hao kwa madi kuwa wanatumika kumhujumu asipate fursa ya kuchaguliwe kuwa mgombea wa jimbo hilo CCM.
  Madai hayo yalitolewa jana jijini Dar es Salaam katika tawi la CCM la Kilimani, Manzese baada ya kuulizwa swali na mmoja wa wanachama wa chama hicho kwamba amesikia mgombea huyo ni [FONT=ArialMT, sans-serif]mkorofi na anatumika kukigawa chama hicho na kumtaka ampe majibu.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, mwenyekiti wa kamati hiyo inayosimamia mikutano ya wagombea hao jimbo la Ubungo, Thadeus Kiwenge, alikataa Nape asijibu swali aliloulizwa, hatua ambayo ilizua mzozo baada yeye mwenyewe kutaka atoe ufafanuzi ili wananchama waelewe ukweli.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Baada ya mwenyekiti kushikilia msimamo wake wa kukutaa Nape asijibu swali hilo, alishikwa na hasira na baada ya kushukua jukwaani aliingia kwenye gari lake na kuondoka eneo la mkutano huku akiwaacha wagombea wenzake wakiwa wamekaa kwenye basi wanalolitumia ambalo wameandaliwa na CCM.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Hizi ni hujuma ambazo zilishafanywa na vigogo waliokuwa akipita kwenye matawi na kueneza uvumi kwamba mimi ni mkorofi na nimekigawa chama hivyo haya maswali ni ya kutengenezwa na hawa wazee ndiyo wanaotumika baada ya kuona nimewabana,” alisema. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza na waandishi wa habari akiwa nje ya eneo la mkutano, alisema swali hilo alianza kuulizwa siku ya kwanza walipoanza mikutano hiyo.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Tangu jana niliulizwa swali hilo, lakini ninachoona hapa maswali haya ni ya kutengenezwa na wapinzani wangu na hasa hawa wazee ndiyo wanaonihofia,” alisema.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Keenja amponza Ng’umbi[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha, mmoja wa mwanachama wa CCM, alimuulizwa mgombea mwingine, Hawa Ng'humbi, kwamba mwaka 2005 alikuwa Meneja wa Kampeni wa Mbunge aliyemaliza muda wake, Charles Keenja, kwa nini hakuwahi kumwambia arudi angalau siku moja kuwaona wanananchi waliomchagua.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Wewe Mheshimiwa mgombea umesema ulikuwa meneja kampeni wa Keenja, ina maana huko ulikokuwa ukipita hukuwahi kumuona Keenja ili umwambie wananchi wananchi waliomchagua wana matatizo ili arudi kutuona je kama tukikuchagua huwezi kuwa kama yeye?” alihoji.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika hali ya kushangaza, mwenyekiti wa mkutano huo alimtaka Ng'humbi ajibu madai hayo wakati Nape alikataliwa kujibu swali aliloulizwa.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Ajinadi kwa samaki wa Magufuli[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika jimbo la Kinondoni, mmoja wa wagombea aliwaacha hoi wanachama baada ya kuwaambia wampe kura kwa kuwa yeye ndiye alifanikisha kukamatwa wavuvi wa Samaki katika Bahari ya Hindi maarufu kama "Samaki wa Magufuli".[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Aliwaambia wanachama kuwa yeye aliwaona Maharamia akiwa ofisi kwake kupitia kompyuta hivyo ana uwezo mkubwa wa kuwasaidia wananchi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika Jimbo la Kigamboni, mgombea mmoja aliwataka wanaCCM kumchagua kwa kuwa anataka kuongeza kauli mbiu ya Rais Jakaya Kikwete kuwa Ari zaidi, Kasi zaidi, nguvu zaidi na Maarifa zaidi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mgombea huyo, Pheres Magesa aliwaambia wanaCCM hao kuwa kuongeza kwa kauli mbiu hiyo itampa nguvu ya kuleta maendeleo ndani ya jimbo hilo kwa haraka.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mwinchumu ajitetea[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa upande mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Msomi Mwinchumu, ilimbidi atatumia mbinu ya kukwepa kubanwa na wanachama hao baada ya kuwaomba wasimnyime kura kutokana na kutofika kwake kwenye matawi, ila waangali kazi alizozifanya wakati akiwa madarakani. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mbunge huyo ilimbidi kutoa kauli hiyo katika mkutano uliofanyika katika Tawi la CCM Kizinga, baada ya mwanachama mmoja kumuuliza swali kama atakuwa tayari kufika eneo hilo kwa kuwa toka awe madarakani hawajamuona kutembelea tawi hilo.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Ninakuja sana na kueleza kazi nilizozifanya, ingawa sikufika hapa mara nyingi nilikwenda ofisi za kata na wote mashahidi, ninawaomba mnyonge mnyongeni haki yake mpeni kutokana na maendeleo makubwa niliyoyafanya,” alisema.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Temeke mkutano chupuchupu[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa upande wa Jimbo la Temeke, mkutano nusura uvurugike baada ya mtu mmoja anayedaiwa hakuwa mjumbe halali wa mkutano huo kuingia na redio ya kurekodia pamoja na mabango ya mmoja wa wagombea hao.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hali hiyo iliibuka baada ya Mbunge wa jimbo hilo, Abbas Mtevu, kukatisha hutuba yake ya kijielezea na kumuomba mwenyekiti wa mkutano huo kumuondoa mtu ambaye hakuwa mjumbe ndani ya kikao.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, hali ya utulivu ilirudi kama kawaida baada ya mtu huyo kuondolewa na wagombea waliobaki waliendelea kujinadi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Burian ang’ara, Mrema azomewa[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mjini Arusha, Jeshi la Polisi lililazaimika kutumia nguvu ya ziada kumlinda Dk. Batilda Burian baada ya mamia ya watu waliofurika kwenye mkutano wa kura za maoni waliokuwa na jazba baada ya kunyimwa nafasi ya kumbeba. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wananchi hao waliokuwa wamegawanyika katika makundi mawili wakiwemo waliokuwa wanazomea wagombea walioshindwa kujieleza vizuri nawaliokuwa wanataka kuwapongeza wagombea wakiwemo waliojieleza vizuri, yalidhibitiwa na polisi waliokuwa wamesheheni silaha za aina mbalimbali ya kiwemo mabomu ya machozi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika purukushani hizo, watu watano walikamatwa na polisi, baada ya kutaka kuleta fujo. .Dalili za kuwepo kwa vurugu zilianza baada yaaliyekuwa mbunge wa Arusha, Felix Mrema, kuanza kujieleza na kuzomewa na baadhi ya wanachama waliokuwa wanaimba nyimbo za kejeli wakidai kuwa wamechoka na hawadanganyiki tena. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mrema aliyekuwa ameingia ukumbini akiwa amejifunga mgorori wa kimasai na kirungu mkononi pamoja na kujaribu kuelezea alichofanya kwa muda wa ubunge wake, hakusikilizwa badala yake ukumbi mzima ulizizima kwa kelele za kumzomea huku wajumbe wakianza kuondoka ukumbini wakiendelea kuimba nyimbo za kumkejeli Mrema .[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati Mrema anakutwa na hali hiyo, Dk.Batlida Buriani alikuwa akishangiliwa kwa nyimbo za Mama ..Mama…huku wajumbe wakitaka kumbeba jambo lililowafanya polisi kufanyakazi ya ziada ya kuwatawanya. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Profesa Sarungi apata wakati mgumu[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mbunge wa Rorya, Profesa Philemon Sarungi, na mgombea wa Tarime, Christopher Kangoye Masero, wameanza kampeni kwa kupata wakati mgumu kwa wanachama kutokana na kuulizwa maswali magumu. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Profesa Sarungi aliulizwa kuhusu umri wake mkubwa wakati Kangoye alihojiwa sababu za kugang’ania kugombea huku akishashindwa mara tatu na na kuwa katika wadhifa wa ukuu wa wilaya na kumtaka aachie wasomi wengine wasomi.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wagombea hao walikumbana na wakati mgumu juzi ambapo Kangoye na wenzake sita walipotembelea Kata za Manga, Komaswa na Nyandoto na kuulizwa maswali mengi.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa upande wa Rorya Profesa Sarungi anapata wakati mgumu kila kijiji ambapo makundi ya vijana yamekuwa yakijikusanya wanaposikia msafara wake ukipita na kumtaka aachie vijana.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, Sarungi anajibu kuwa wananchi wa Rorya wanaelewa maendeleo aliyoyaleta na kwamba wawakilishi wanapeleka hoja zao na kuzitetea bungeni bila kuangalia uzee.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Makatibu Mbeya wasimamishwa[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Makatibu kata wanne wa CCM Wilaya ya Mbeya mjini, wamesimamishwa kazi hadi uchaguzi mkuu utakapomalizika kwa madai kuwa wamekiuka kanuni na maadili ya chama kwa kugawa kadi bila kufuata taratibu na kutumia vibaya fedha za ruzuku za matawi.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, kusimamishwa kwa makatibu hao kumeelezwa kuwa ni kutokana na kumuunga mkono mmoja wa wanachama walioomba kuteuliwa kuwania ubunge Mbeya Mjini.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Makatibu waliosimamishwa ni Said Ilanga wa Kata ya Itende, Tamson Kisanga (Tembela), Zabibu Kimati (Ilemi) na Mwanjangu wa kata ya Mbalizi Road ambao walisimamishwa tangu Julai 16 mwaka huu kwa kuandikiwa barua zenye kumbu namba CCM/MBW/MK.34/3/33 iliyosainiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Bahati Makalanzi.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wakizungumza na Nipashe, walisema kusimamishwa kwao kuna walakini kwa sababu kamati za siasa za kata zao hazijawahi kukaa kujadili tuhuma dhidi yao badala yake suala hilo limechukuliwa maamuzi moja kwa moja ngazi ya wilaya, kitu ambacho ni kinyume na utaratibu wa chama.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Bahati Makalanzi alipoulizwa, alithibitisha kusimamishwa kwa makatibu hao, lakini akakataa kutoa ufafanuzi kwa maelezo kuwa hafanyi kazi na magazeti.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Nusura mkutano uvunjike Arusha[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mkutano wa kwanza wa kampeni za kura za maoni katika Jimbo la Arusha umenusurika kuvunjika, baada ya baadhi ya wagombea kutaka kuwakatazawaandishi wa habari kufanya kazi yao, jambo lililozua tafrani kubwa kutoka kwa washiriki waliopinga vikali kitendo hicho.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kauli ya kufukuzwa kwa waandishi wa habari [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]ilitolewa na Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Arusha, Semmy Kiondo, kwa madai kuwa ni makubaliano ya wagombea wote wa ubunge na udiwani, jambo lililowafanya wananchi kumzomea na wengine[/FONT] [FONT=ArialMT, sans-serif]wakinyanyuka kutaka kususia mkutano huo.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, baada ya kiongozi huyo kupata pingamizi toka kwa wananchi[/FONT] [FONT=ArialMT, sans-serif]alibadilisha kauli yake na kuwaruhusu waandishi na mkutano ukaendelea.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mkutano huo pamoja na kuwa chini ya ulinzi mkali wa askari polisi wa vikosi mbalimbali, ulimalizika kwa amani na utulivu huku asilimia kubwa ya washiriki wakijihami dhidi ya maofisa wa Takukuru. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wanaotumia ukabila waonywa[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]CCM Wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara, kimetishia kuwafuta wagombea watatu wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Musoma Vijijini baada kutoa kauli za ukabila katika mikutano ya hadhara ya kampeni za kura za maoni za chama hicho.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katibu wake, Ferouz Bhano, alisema wagombea hao wanadaiwa kutoa kauli za ukabila katika mikutano ya kampeni katika matawi Buraga, Busekera Chitare, Chimati na Buganda katika kata ya Bukumi juzi siku ya kwanza ya uzinduzi wa kampeni hizo.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Nimewaita wote jana usiku(juzi)na kuwakemea na kuwapa onyo kali na wakiendelea nitawasimamisha ama kuwafuta kwani kutumia ukabila kuomba kura kwa wanachama ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni ya uongozi na maadili pia nchi haitafuti viongozi kwa misingi ya ukabila wala udini,”alisema Bhano.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mwingine ashindwa kupanda mlima[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mgombea ubunge kupitia CCM Jimbo la Makete, Amelek Ngajiro, alibebwa baada ya kushindwa kupanda mlima Kigulu kwenda kuomba kura kwa wanachama.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mgombea huyo alishindwa kupanda mlima huo mrefu na kulazimika kubebwa na katibu mwenezi wa Kata ya Kigulu.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wagombea watano waliorudisha fomu za kuwania ubunge katika jimbo hilo, walianza kampeni juzi katika Kata za Kigulu, Matamba na Itundu, ambapo wanatarajia kumaliza kampeni hizo katika kata 22 za jimbo hilo Julai 31, ambapo Agosti Mosi ndiyo itakayokuwa siku ya kupiga kura za maoni. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Imeandikwa na Thobias Mwanakatwe (Mbeya), Asraji Mvungi na John Ngunge (Arusha), Joctan Ngelly (Kigoma), Samson Chacha (Tarime), Renatus Masuguliko (Geita), Grace Chilongola (Mwanza), George Marato (Musoma), Said Hamdani (Lindi), George Marato (Musoma), Richard Makore na Moshi Lusonzo (Dar) na Beatrice Shayo (Makete).[/FONT]  CHANZO: NIPASHE

  Nawapongeza Takukuru wazidi kuendelea kuwafichuwa Mafisadi hongera Takukuru fanyeni kazi yenu.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hii katuni kiboko, aisee! Naona jamaa (Takukuru) anawaburuza jamaa bila kuwaangalia usoni. Hana utani.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,827
  Trophy Points: 280
  Miye bado siwaamini hawa TAKUKURU mpaka nione wanafanya kweli. Ndiyo hawa hawa walisema mkataba wa Richmond ulikuwa na kasoro ndogo ndogo tu za hapa na pale na si kingine zaidi. Ndiyo hawa hawa wameshindwa kupambana na mafisadi wa EPA, ununuzi wa RADA, na wizi wa Kiwira. Tusubiri labda watafanya kweli, lakini kwa sasa naona ni mazingaombwe tu ya kuelekea October 31, 2010.
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Bubu,
  Umesikia CUF wanawasifia? Kunani?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,827
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jasusi hawa CUF siwaamini kabisa inaelekea CCM imeshawaweka sawa. Si unamuona Mrema? badala ya kupigia debe chama chake sasa amekuwa mpiga debe maarufu wa CCM kuliko hata CCM wenyewe.

   
 7. M

  Mutu JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Bubu
  Ni tatizo la muundo wake ,may be watanzania tuanze kujifunza kujiuzuli tukishindikizwa kusema visivyo.
  Kwenye kesi kubwa kama richmond ,epa hawa Takukuru huambiwa ya kusema hilo ndili tatizo.
   
 8. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  I give them the benefit of the doubt kwenye huu uchaguzi. Kila kitu kina mwanzo na mwisho labda huu ndio mwanzo wao wa kuwa upande wetu(Wananchi) na mwisho wa kuwa upande wa mafisadi.
   
 9. K

  Kenge (Eng) JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2010
  Joined: Dec 7, 2006
  Messages: 502
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kwa taarifa sahihi TAKUKURU ni vipofu na wako pale kwa masilahi ya mtandao. wanachokifanya ni ku scandalize baadhi ya wagombea na kama mmemsikia MAKAMBA akisisitiza hawa CCM wanatafuta visingizio vya kuwatema wasiowataka. Mifano hipo.

  Mjini Bukoba nimepata habari toka mtu aliyekuwa ndani ya mpango mzima wa kum scandalize MAYOR wa Manispaa ya BUKOBA Mh. Ruangisa. Yeye na Mbuge Hamis Kagasheki, hawaivi na baada ya kusikia kuwa Mh. Mayor atakuwa na mkusanyiko wa kuvunja KAMATI ya mwanae aliyeoa ikaandaliwa kila aina ya uzalilishaji ambapo alikamatwa mbele ya vyombo vya habari na kutembezwa mitaani toka eneo lile hadi ofisi za TAKUKURU huku akiwa amekwidwa! Ni wakati gani TAKUKURU inaweza kuwa na taarifa na kuandaa akina Renatusi Mutabuzi (ITV) Star TV, radois, n.k kabla ya kukamata? Kwa nini wamtembeze badala ya kumweka kwenye gari. Na kwa nini wamtangaze kwenye vyombo vya habari na kutoa tukio hilo bila uchunguzi? Pale kwa kuwa ni THREAT wa Mh. Kagasheki hapo TAKUKURU imetumiwa! Binafsi hakuna cha TAKUKURU ila sasa ufisadi umekamata chombo hicho. Hapo ni mchakato wa CCM subiru hapo CCM itakapoingia ulingoni kwenye kampeni na upinzani, mtasikia jinsi wagombea wa UPINZANI watakavyokamatwa na hongo za kubambikiziwa. Ni mpinzani yupi anayo jeuri ya kuonga?
   
Loading...