Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,807
- 11,969
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Stenga
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inawashikilia wafanyakazi 30 wa Bohari ya Dawa (MSD) Mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za ubadhirifu wa dawa na vifaa tiba zenye thamani ya zaidi ya Sh. 254 milioni.
Mbali na wafanyakazi hao, pia kuna mtumishi mmoja wa Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Stenga akitoa taarifa ya kushikiliwa kwa watumishi hao leo Jumanne tarehe 23 Juni 2020 amesema, uchunguzi unaendelea na watakaobainika wafanyikishwa Mahakamani.
“Natoa wito kwa wafanyakazi wa umma kuridhika na vipato vyao,” amesema Stenga.