TAKUKURU yawasaka wamiliki wa Kampuni ya MEIS Industries kwa tuhuma za kutoroka na mabilioni

Miiku

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
3,835
2,628
TAKUKURU inawatafuta wamiliki wa kampuni ya Meis Industry LTD inayodaiwa kutoroka na shilingi bilioni 46 walizokuwa wamekabidhiwa kwaajili ya kujenga kiwanda cha saruji mkoani Lindi.
FB_IMG_1560859027288.jpeg


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini Tanzania inawatafuta wamiliki wa Kampuni ya Meis Industriesltd inayodaiwa kutoroka na mkopo wa fedha kiasi cha Sh46 bilioni kwa ajili ya kujenga kiwanda cha saruji mkoa wa Lindi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Juni 18,2019 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema wamebaini kampuni ya Meis ilikabidhiwa fedha hizo kama mkopo mwaka 2011 kutokana na sehemu ya fedha za uwekezaji zilizotolewa na Serikali ya Libya kwa Serikali ya Tanzania.

"Mwaka 2009 Serikali zote mbili zilisaini mkataba wa nyongeza ambao uliitaja kampuni ya Meis kama kampuni itakayopewa kiasi cha dola 20,000,000 kwaajili ya uwekezaji wa ujenzi wa kiwanda cha saruji eneo la Machole Mkoani Lindi,” amesema Brigedia Mbungo.

Amewataja wahusika wa kampuni ya Meis ambao hawajapatikana na wanaendelea kutafutwa ni Islam Balhabou, Merey Awadh Saleh, Sabri Kuleib na Abdallah Bin Aliya.

Brigedia Mbungo amesema mwenye taarifa ya watuhumiwa hoa awasiliane na Takukuru ili kuweza kuwakamata na kuja kujibu tuhuma zinazowakabili.
 
wala "rushwa"wanawasaka wala "rushwa"wenzao hapo patamu!!
hawa TAKUKURU wajibu kwanza tuhuma dhidi yako zilizotolewa na Cyprian Musiba waache "utapeli" wao!
Wananchi tunasubiri Cyprian Musiba na gazeti lake wakijibiwa na hao majizi TAKUKURU kwa ufasaha na hoja kwa hoja.... haya mambo ya ubabaishaji yaliofanywa na huyo kaimu kamanda wa TAKUKURU ndio yametufikisha hapa tulipo!Watanzania tujifunze kuwajibika kama Mh. JPM sio lazima Rais awatumbue!
 
Ni kichekesho
Mnawapa watu pesa bila kujua office zipo wapi
Hawana mali zisizohamishika
Anzeni na Wizara husika watasema
Hii ndio ccm mbele kwa mbele
Wamewafanya wananchi mabwege
Jiwe umeisikia hii Mzee a kutumbua na kuteua hahahahhh interesting...
 
Tanzania tuna shida gani? Mbona tunajiabisha hivi kwa kuwa wezi. Kibaya wezi unaanzia juu kwa watu wa heshima mpaka kina siye
Kwani wamiliki wa hii kampuni ni wa Tz?....ila all in all pamoja na kumuweka mwanajeshi watu wanakula rushwa bila woga hii hatari sana aisee
 
Kwani wamiliki wa hii kampuni ni wa Tz?....ila all in all pamoja na kumuweka mwanajeshi watu wanakula rushwa bila woga hii hatari sana aisee
Hakuna wa kuaminika hii nchi yetu. Tunakula rushwa kupitiliza. Hizi story zinathibitisha kuna matatizo makubwa sana ya ethics
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom