TAKUKURU yavuta mafaili ya vigogo wengine tena

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
  • Ni wale wote waliotajwa na Taasisi ya Makosa Makubwa ya Ufisadi ya Uingereza (SFO)
  • Serikali iliingia hasara ya Tshs Billioni 13
  • Kwenye ripoti wamo Mustapha Mkulo, Marehemu William Mgimwa, Godfrey Mgimwa ambaye ni mbunge wa Kalenga,
  • Wengine ni msaidizi wa ofisa mwandamizi (Msajili wa Hazina), Kamishna Msaidizi na mshauri wa sera wa Wizara, mwenyekiti wa ufundi wa Kamati ya Madeni ya Serikali (TDMC)
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inawachunguza watu wote waliohusika na utakatishaji fedha wakati Serikali ilipokopa Dola 550 milioni za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh1.1 trilioni) kutoka benki ya Standard ya Uingereza.

Tayari watu watatu wameshafikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa makosa manane likiwemo la kutakatisha fedha.

Msemaji wa Takukuru, Tunu Mleli aliliambia gazeti hili jana kwamba kila mtu aliyetajwa katika sakata hilo kama ilivyoripotiwa na Taasisi ya Makosa Makubwa ya Ufisadi ya Uingereza (SFO), anachunguzwa ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo, lakini hakutaja majina yao.

“Hatuwezi kumtaja ni nani kwa sababu suala hilo lipo kwenye uchunguzi na sheria inatukataza kutaja watu walioko chini ya uchunguzi, lakini tunafuatilia,” alisema Tunu alipoulizwa kuhusu habari kwamba wameanza kuwafuatilia maofisa kadhaa waliohusika katika kashfa hiyo iliyoisababisha hasara ya Sh13 bilioni kwa Serikali.

Ripoti ya SFO inawataja maofisa watano katika sakata hilo, akiwamo Waziri wa Fedha wa Serikali ya Awamu ya Nne.
Ripoti ya SFO inawatuhumu maofisa hao kushiriki katika majadiliano yaliyosababisha vitendo vinavyotiliwa shaka.


Ripoti hiyo inaeleza kuwa waziri aliyeshiriki kwenye mazungumzo hayo ni yule aliye aliyeondolewa wakati wa kipindi cha pili cha Serikali ya Awamu ya Nne, na mwingine aliyefariki dunia Januari 2014, ingawa haiwataji kwa majina.

Waziri wa Fedha aliyefukuzwa kazi Mei 2012 alikuwa Mustafa Mkulo, ambaye ripoti inaonyesha alikuwapo wakati mpango wa kuomba mkopo huo ukianza kabla ya kufifia wakati alipoondolewa. Wakati ulipofufuliwa na kufanyiwa marekebisho yaliyoingiza kampuni ya Egma, Mkulo hakuwapo.

Aliyerithi nafasi hiyo na baadaye akafariki wakati akitibiwa nchini Afrika Kusini Januari 2014 ni Dk William Mgimwa.

Wakati ilipowasilisha barua ya pendekezo la mkataba wa mkopo huo wizarani, Februari 2012, wizara ilikuwa chini ya Waziri Mkulo na mazungumzo ni kama yalififia kwa muda kabla hayajaanza upya Septemba chini ya Dk Mgimwa.

Juhudi za kumpata Mkulo kuzungumzia suala hilo, hazikufanikiwa.

Ripoti ya SFO inawataja wengine waliokuwamo kwenye timu ya Serikali ya majadiliano kuwa ni ofisa mwandamizi wa Hazina ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Madeni ya Serikali (NDMC), msaidizi wa ofisa mwandamizi (Msajili wa Hazina), Kamishna Msaidizi na mshauri wa sera wa Wizara, na mwenyekiti wa ufundi wa Kamati ya Madeni ya Serikali (TDMC).

Ripoti inaeleza kuwa hao ndio walikuwa wanakutana na timu ya maofisa wanne kutoka benki ya Stanbic. Kiongozi wa timu ya Stanbic (T) ni aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa Stanbic, Bashir Awale ambaye alifukuzwa kazi Agosti 19, 2013.

Mfanyakazi Z ametajwa kuwa ni mhitimu wa chuo kikuu aliyekuwa kwenye mafunzo ya kazi na ni mtoto wa Waziri wa Fedha. Dk Mgimwa ni Waziri wa Fedha aliyefariki na ana mtoto anayeitwa Godfrey ambaye ni mbunge wa Kalenga.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mgimwa alikiri kuwa amewahi kufanya kazi Stanbic, lakini hajui chochote kuhusu mchakato huo.

“Nimesikia habari hizo, lakini sifahamu lolote. Kuwa mtumishi wa Stanbic wakati tukio hilo linatokea haimaanishi kuwa watumishi wote walihusika. Nadhani ni uhusiano uliopo kati yangu na waziri ndio unafanya nihusishwe,” alisema Mgimwa.

“Ni vile tu hatupo naye hivyo hakuna wa kuelezea zaidi. Kwa kuwa mzee amefariki naona inatafutwa namna ya kutengeneza uhusiano uliokuwepo kati ya taasisi zilizohusika.”

SFO inasema katika ripoti yake kwamba ofisa wa benki ya Standard aliyeshiriki ni Florian Von Hartig (FVH) ambaye alikuwa akiiwakilisha katika soko la mitaji jijini London. Ofisa huyo alikuja nchini na Septemba 20 alipokuwa anaondoka kurudi Uingereza alifahamishwa juu ya ongezeko la asilimia moja ya ada na mshirika wa ndani, yaani Stanbic.

Katika kesi iliyofunguliwa wiki iliyopita, washtakiwa wote watatu walisomewa mashtaka manne likiwamo la utakatishaji wa fedha kiasi cha Dola 6 milioni za Kimarekani 6, lakini Sinare aliyekuwa mrembo wa Tanzania mwaka 1996, anakabiliwa na mashtaka mengine mawili ya kughushi na mawili mengine ya kuwasilisha nyaraka za uongo wakati Serikali ya Tanzania ilipokopa fedha kutoka benki ya Standard ya Uingereza kati ya mwaka 2012 na 2015.

Mbali na shtaka la kutakatisha fedha, mashtaka mengine waliyosomewa ni kula njama ili kutenda kosa la kujipatia pesa, linalowakabili washtakiwa wote; mashtaka matatu ya kughushi huku moja likiwakibili wote, na mawili yanamkabili Sinare peke yake.

Mashtaka mengine ni mawili ya kuwasilisha nyaraka za uongo yanayomkabili Sinare peke yake, na shtaka la kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu linalowakabili washtakiwa wote.

Washtakiwa hao watatu wamo katika ripoti ya SFO yenye kurasa 55 ambayo ni matokeo ya uchunguzi wa ndani uliofanywa na mwanasheria wa benki ya Standard ya Uingereza, Jones Day. Baada ya Day kukamilisha uchunguzi aliwasilisha SFO ushahidi wote wa kimaandishi, baruapepe, simu na mazungumzo mengine aliyokusanya ya wote waliohusika na ukiukwaji wa taratibu za kibenki.

SFO iliitumia ripoti hiyo katika shauri la kuangalia namna ukiukwaji wa taratibu za kibenki katika mkopo wa Dola 550 milioni kutoka benki ya Standard ulivyosababisha Sh13 bilioni kuingizwa katika kampuni ya Egma inayodaiwa kuwa ilikuwa wakala.

Shauri hilo liliisha kwa Standard kukubali kuilipa Tanzania fidia chini ya makubaliano maalum ya DPA katika mahakama ya Southwark Crown. Chini ya mpango huo wa DPA, taasisi hiyo ya kifedha imepata unafuu wa adhabu, jambo ambalo pia linalalamikiwa na wapambanaji dhidi ya ufisadi nchini Uingereza.


Chanzo: Mwananchi
 
Bado sipati picha na haya maigizo yanayofanyika hapa Tanzania.

Tuliambiwa kuwa ITAUNDWA MAHAKAMA MAALUMU KWAAJILI YA MAFISADI MA MAJIZI.

SASA MBONA WANAPELEKWA KISUTU AU NDIO HII IMEBADILISHWA JINA?????

ISIJE KUWA NI CHANGA LA MACHO KESI ZINACUKUA MUDA MREFU NA MWISHO WA SIKU; ZINAPOTEA KIMYAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Bado sipati picha na haya maigizo yanayofanyika hapa Tanzania.

Tuliambiwa kuwa ITAUNDWA MAHAKAMA MAALUMU KWAAJILI YA MAFISADI MA MAJIZI.

SASA MBONA WANAPELEKWA KISUTU AU NDIO HII IMEBADILISHWA JINA?????

ISIJE KUWA NI CHANGA LA MACHO KESI ZINACUKUA MUDA MREFU NA MWISHO WA SIKU; ZINAPOTEA KIMYAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!
Aliseye kwambia mchakato wa kuunda mahakaman ni swala la wiki mbili ni nani au hukumsikia rais kuwa zoezi lipo kwenye mchakato bado,wewe vipi?
 
SFO wametaja majina bila kuficha hapa Takukuru wanasema sheria zinawabana zipi izo tena...
 
ESCROW ndiyo tunataka wahusika wapelekwe mahakamani. Kesi yake na ushaidi ulishakamilika.. tukidhibiti wakubwa wadogo hawatathubutu kuiba
 
Nasubiri ya Chenge, au nguvu za GAMBOSHI zinasaia kwenye hili?! cc: mshana Jr.
 
Bado sipati picha na haya maigizo yanayofanyika hapa Tanzania.

Tuliambiwa kuwa ITAUNDWA MAHAKAMA MAALUMU KWAAJILI YA MAFISADI MA MAJIZI.

SASA MBONA WANAPELEKWA KISUTU AU NDIO HII IMEBADILISHWA JINA?????

ISIJE KUWA NI CHANGA LA MACHO KESI ZINACUKUA MUDA MREFU NA MWISHO WA SIKU; ZINAPOTEA KIMYAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!

Mkuu wewe endelea kukosa tu hiyo ni haki yako kidemokrasia, Ila wenye macho tunaona hatua zinavyochukuliwa Kwa mstakabali wa nchi yetu sote.
 
Back
Top Bottom