TAKUKURU yautupilia mbali ushahidi ulioletwa na Nassari na Lema wa madiwani kuhongwa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Takukuru yautupa ushahidi wa video wa wabunge wa Chadema, Joshua Nassari na Godbless Lema ukiwaonyesha madiwani wa chama hicho waliohamia CCM wakihongwa rushwa, kwa madai kuwa wabunge hao waliharibu uchunguzi baada ya kuingiza siasa katika jambo hilo.
===============

TAKUKURU imesema haiwezi kuendelea na uchunguzi wa madai ya rushwa yaliyoletwa na wabunge wa CHADEMA, Joshua Nassari na Godbless Lema kuwa madiwani waliohamia CCM walipewa rushwa

- Imeeleza wabunge hao waliingilia uchunguzi na kuuvuruga ila hawawezi kusema ni jambo gani walivuruga kwa sababu mambo mengine ni ya kiuchunguzi

TAKUKURU yautupilia mbali ushahidi wa video wa Mbunge wa CHADEMA, Joshua Nassari ukiwaonyesha Madiwani wa chama hicho waliohamia CCM wakishawishiwa kwa rushwa, yadai kuwa Mbunge huyo aliharibu uchunguzi baada ya kuingiza siasa katika jambo hilo.
 
0dbab534bea0f7a14d446c30e08dfc98.jpg
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imetupilia mbali ushahidi wa video wa Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari, ukiwaonyesha madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), waliohamia CCM wakishawishiwa kwa rushwa kwa madai kuwa Mbunge huyo aliharibu uchunguzi baada ya kuingiza siasa katika jambo hilo.

Chanzo: Mtanzania
 
Takukuru yautupa ushahidi wa video wa wabunge wa Chadema, Joshua Nassari na Godbless Lema ukiwaonyesha madiwani wa chama hicho waliohamia CCM wakihongwa rushwa, kwa madai kuwa wabunge hao waliharibu uchunguzi baada ya kuingiza siasa katika jambo hilo.
Niulize tu, kuna mtu alitegemea hatua zaidi ya hiyo? Mtuhumiwa kupandishwa cheo/madaraka takukuru wafanye nini zaidi ya hilo?
 
Kitengo cha uchwara pale Ikulu eti kimchunguze uchwara kutoa rushwa kwa Madiwani na Wabunge wa UKAWA!!!

Takukuru yautupa ushahidi wa video wa wabunge wa Chadema, Joshua Nassari na Godbless Lema ukiwaonyesha madiwani wa chama hicho waliohamia CCM wakihongwa rushwa, kwa madai kuwa wabunge hao waliharibu uchunguzi baada ya kuingiza siasa katika jambo hilo.
 
Wangefanya tofauti ingeshangaza sana!nilitegemea hivyo tangu mwanzo!kesi ya Nyani hakimu Ngedere unategemea nini?lakini yana mwisho ni suala la muda tu.
 
Back
Top Bottom