TAKUKURU yaomba kumuhoji Mkurugenzi wa UDART

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,376
2,000
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumhoji Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART) Robert Kisena (46) na wenzake wawili.

Kisena ambaye hakufika Mahakamani kwa sababu anaumwa na wenzake watatu ambao ni Kulwa Kisena(33) na Charles Newe(47) wanakabiliwa na mashtaka 19 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kuusababishia Mradi wa UDART hasara ya zaidi ya Bilioni. 2.41.

Maombi hayo yaliwasilishwa Mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Simon alidai kuwa wanawaomba washtakiwa hao kwenda kuhojiwa kwa siku moja TAKUKURU kisha kurudishwa na kubainisha kuwa mshtakiwa wa kwanza Kisena ameshindwa kufika mahakamani hapo kwa sababu ni mgonjwa.

Hata hivyo mahakama hiyo imeridhia washtakiwa hao kuhojiwa na kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 11, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa hao na mwenzao mmoja ambaye ni raia wa China, Cheni Shi (32) walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 11, 2019 na kusomewa mashtaka 19 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kuusababisha mradi huo hasara ya zaidi ya Bilioni. 2.41.

Katika mashtaka hayo, lipo shtaka moja la kuongoza uhalifu, lingine moja la kujenga kituo cha mafuta bila kibali, la kuuza mafuta sehemu zisizoruhusiwa pamoja na shtaka la wizi wakiwa Wakurugenzi.

Pia wanakabiliwa na mashtaka manne ya utakatishaji fedha, ya kughushi manne, kutoa nyaraka za uongo manne, mashtaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na shtaka moja la kuisababishia mradi huo hasara.

Katika kosa la kuisababishia UDART hasara, linalowakabili washitakiwa wote inadaiwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 Washtakiwa hao kwa mamlaka waliyonayo waliisababishia UDART hasara ya Sh. Bilioni.2.41.

Pia inadaiwa mshtakiwa Robert Kisena na Shi, Mei 26, 2016 wakiwa katika Benki ya NMB tawi la Ilala kwa pamoja wakiwa Wakurugenzi wa Longway Engineering huku Kisena akiwa Mkurugenzi wa UDART walihamisha Sh. Milioni 603 kutoka akaunti ya benki ya UDART kwenda kwenye akaunti ya Longway ambapo ndani ya siku mbili walizitoa fedha hizo huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa la kughushi.

Katika kosa la kujipatia nyaraka kwa njia ya udanganyifu,inadaiwa mshtakiwa Robert Kisena na Shi, Mei 30, 2016 katika Benki ya NMB Ilala walijipatia nyaraka kwa njia ya udanganyifu kutoka katika benki hiyo ikiwa na jina la Fund Transfer Request Form ya Aprili 6, 2016 kwa lengo la kuonyesha kiasi cha Sh.Milioni 750 zimelipwa na Kampuni ya Longway kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa Kituo cha Mwendokasi Kimara, Kivukoni, Ubungo na Morocco huku wakijua kuwa siyo kweli.

Katika kosa jingine la utakatishaji fedha linalowakabili washitakiwa wote wanadaiwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa wakiwa na lengo hovu walibadilisha mafuta kuwa fedha ambayo ni Sh. Bilioni 1.21 huku wakijua mafuta hayo ni zao la kosa la wizi.

Robert Kisena na Kulwa Kisena wanadaiwa kati ya Januari 1, 2015 na Desemba 31, 2017 huko Katika maeneo ya Jangwani Ilala, wakiwa Wakurugenzi wa Kampuni ya Zenon Oil and Gas Ltd
walijenga kituo cha Mafuta bila ya kupata kibali kutoka EWURA.

Millard
 
msani

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
1,773
2,000
Hahahahaha tutaishi kama mashetani.
Uzuri hapa hakuna msafi, ngoja wamalizane wao kwa wao.
"Ukipiga mbwa subiri kauli ya mmiliki" Uswahilini kwetu unalogwa mchana kweupe.
 
kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
321
250

ahojiwe tu
 
MLUGURU

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
1,977
2,000
Nimekuwa interested na huyo Dogo Janja Kulwa kisena....at the very young age of 33 tayari kashaunganishwa katika deal za billions of money.

Ingekuwa sio workforce ya awamu hii angekuwa ni mmoja Wa Vijana wanaoleta heshima maeneo ya starehe hapa Mjini.

Kulwa kisema,Robert kisena kweli Maji hufata mkondo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom