Elections 2010 TAKUKURU yamtia nyavuni Felix Mrema - Arusha mjini

Mzee wa Usafi

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
644
292
Mambo ya CCM kutumia fedha kwa kujipatia uongozi yanaendelea kujidhihirisha. Kwa sasa PCCB ina mshikilia Mh.Mrema na mabalozi kadhaa kwa tuhuma za rushwa.....nitawaletea habari kamili baadaye kwani mpaka sasa bado wanahojiwa.
 
PCCB endeleeni :fish2: wote hadi waishe tunataka uchaguzi safi mwaka huu
 
nadhani kutakuwa na habari kamili muda mfupi ujao.....hapa kwetu arusha jana sombetini kulikuwa balaaa. Fedha nje nje....
 
CCM wote ni watoa na wapokea rushwa, hakuna chaguo la Mungu hata mmoja.

hakuna lolote hapa. Kinachofanyika ni kukamata watu wote ambao si wanamtandao ili wasirudi bungeni ngwe ijayo. Simpendi Mrema kama Mbunge maana hajafanya lolote Arusha, lakini Batilda anatoa rushwa nje nje wala hakamatwi. Na wala hutasikia Chenge, Karam,gi nk wamekamatwa. Watakamatwa akina Selelii, Sita, Mwakyembe nk ili tu wasipate haki tena. Hiyo ndiyo kazi ya TAKUKURU.... poleni Wa TZ.
 
Kweli kabisa. Nshaanza kuhisi kuwa takukuru wanafanya kaz nyingine zaidi ya kukamata rushwa,,,
 
hakuna lolote hapa. Kinachofanyika ni kukamata watu wote ambao si wanamtandao ili wasirudi bungeni ngwe ijayo. Simpendi Mrema kama Mbunge maana hajafanya lolote Arusha, lakini Batilda anatoa rushwa nje nje wala hakamatwi. Na wala hutasikia Chenge, Karam,gi nk wamekamatwa. Watakamatwa akina Selelii, Sita, Mwakyembe nk ili tu wasipate haki tena. Hiyo ndiyo kazi ya TAKUKURU.... poleni Wa TZ.
Ni hisia tu. TAKUKURU sio mtu mmoja, wapo wanaowajibika na pia wapo wazembe. Wale ambao wamewajibika ipasavyo tuwapongeze kwani wamefanya. Wazembe tuwasaidie wawajibike, au kusanyeni ushahidi na muuweke hapa ili tuwasaidie wakuu wao kuwawajibisha watendaji wao wazembe.
kama rushwa iliitwa takrima, si rahisi sana kusahau mazoea hayo ndo maana mpaka leo watu wanaendelea kusikiliza miziki ya zamani na kusema zilizpendwa ilhali bado wanazipenda
 
Takukuru watakamata wale wote waliokuwa wanamsakama bosi wao kwa kashfa ya rich-rich
 
atakamatwa hila hatafikishwa popote TAKA KURU Hamuna kitu wawapeleke mahakamani ndo tutaamini

King, si unajua mashtaka ni mchakato? Ni kweli ili tuamini, tuone hatua za juu zaidi zimefikiwa. Hili la kuhusisha vyombo vya habari ni kitanzi kwao, wakiwaachia tutapoteza imani iliyoanza kurudi. wana wajibu wa kuendelea na kurudisha na kulinda hadhi yao iliyopotea
 
wote wanatoa rushwa ila ni kweli waliokua wanajifanya wanamsakama ''kucheka'' watakiona, hawatapata kinga ya wengine kwa iyo wakati wanajifanya wanatoa tu wazee hawa!
 
hakuna lolote hapa. Kinachofanyika ni kukamata watu wote ambao si wanamtandao ili wasirudi bungeni ngwe ijayo. Simpendi Mrema kama Mbunge maana hajafanya lolote Arusha, lakini Batilda anatoa rushwa nje nje wala hakamatwi. Na wala hutasikia Chenge, Karam,gi nk wamekamatwa. Watakamatwa akina Selelii, Sita, Mwakyembe nk ili tu wasipate haki tena. Hiyo ndiyo kazi ya TAKUKURU.... poleni Wa TZ.

Hii kali kaka. umesomeka kupita maelezo, Nilikua najiuliza hawa Takukuru Huu muamko wameupata wapi?
 
Malaria sijui yuko wapi leo aje atoe mchango wake tuusikie kuhusu waccm wanavyokamatwa na takukuru
 
King, si unajua mashtaka ni mchakato? Ni kweli ili tuamini, tuone hatua za juu zaidi zimefikiwa. Hili la kuhusisha vyombo vya habari ni kitanzi kwao, wakiwaachia tutapoteza imani iliyoanza kurudi. wana wajibu wa kuendelea na kurudisha na kulinda hadhi yao iliyopotea

Mkuu Majala Hapa hukuna lolote kesi ngapi zimefikishwa na TAKA KURU wakiwa na ushahidi still WANASEMA UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA

HAPA HAKUNA KITU we subiri kipenga kikipulizwa hawa wote watakuwa kwenye kampaini kama kawa, we waache TAKA KURU waboreshe jengo lao kwa kuweka mahandsome na maduuu, sorry kama nimekwaza mtu

Kama CCM wako serious kwa nini anayekamatwa asiondolewe mara moja kwenye mchakato wa wagombea?
 
Chaguzi zote zilikuwa hivo hivo, hawa ni danganya toto. TAKUKURU nitaiamini kama watakuwa wame mhoji Rukuvi make ndiye alikuwa wa kwanza kugawa pikipiki, Rostam, Karamagi. May be hawa ni wana mtandao?
 
Back
Top Bottom