TAKUKURU yampinga Askofu Mokiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAKUKURU yampinga Askofu Mokiwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jibaba Bonge, Oct 6, 2010.

 1. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Wednesday, 06 October 2010
  Na Leon Bahati

  TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imepinga kauli aliyotoa askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana, Valentino Mokiwa kwamba wananchi wakipewa fedha za rushwa na wagombea wapokee kwa kuwa si dhambi kula fedha za wajinga.

  Takukuru, ambayo inalalamikiwa kwa kutofanyia kazi taarifa za rushwa kwenye uchaguzi zinazotolewa na wananchi, imesema kwamba itamchukulia hatua kali mtu yeyote atakayetekeleza kauli hiyo ya Askofu Mokiwa kwa kuwa kupokea rushwa na kuvunja sheria.

  Akizindua mpango wa Bima ya Afya ya Imani kwa Watu Wenye Kipato cha Chini jijini Dar es Salaama juzi, Askofu Mokiwa aliwataka waumini wa kupokea na kula pesa zote zinazotolewa na wagombea wa nafasi mbalimbali katika kampeni zinazoendelea nchi nzima akisema "fedha za namna hiyo si dhambi, si haramu wala si rushwa".

  Lakini Askofu Mokiwa aliwaonya waumini kwamba fedha hizo zisiwafanye wawapigie kura wagombea wanaowapa fedha kwa kuwa wanaotoa rushwa hiyo ni "wajinga na kula fedha ya mjinga bila ya kumtekelezea azma yake si kosa".

  Kauli kama ya Askofu Mokiwa zimekuwa zikitolewa na hata wanasiasa ambao huwaeleza wananchi kuwa wapokee fedha zinazotolewa na wagombea, lakini waadhibu siku ya kupiga kura.

  Jana, ofisa uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani aliiambia Mwananchi kwamba sheria ya rushwa iko wazi na kwamba mtoaji na mpokeaji ni wahalifu.

  Kapwani alisema watakaofuata kauli zinazotolewa majukwaani wanaweza kujikuta matatani kwa sababu Takukuru ni chombo kilichoundwa kisheria na kinaongozwa kwa kanuni za sheria hiyo.

  "Sheria hii katika kifungu cha 15 inatamka wazi kuwa mtu yeyote anayetoa au kupokea hongo atakuwa ametenda kosa chini ya sheria hii," alisema.

  Kutokana na hali hiyo, Kapwani aliwataka wananchi wanapowaona wagombea au mtu yeyote anayetoa rushwa watoe taarifa Takukuru ili hatua zinazofaa zichukuliwe.

  SOURCE : MWANANCHI

  Hawa Takukuru ni wapuuzi sana. Wanapelekewa taarifa hawazifanyii kazi kwa sababu wahusika ni CCM. Mbaya zaidi wanawapigia simu kuwaambia waondoke haraka kwenye eneo la tukio kama alivyosema Lema pale Arusha. Sasa wanajifanya kumjia juu Askofu.

  Siku zao zinahesabika.
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hadi pale takukuru itakapofumuliwa na kuundwa upya ndipo itaheshimika na kuaminiwa na watanzania, vinginevyo kwa hali hii ya sasa chini ya uogozi wa Hoseah, takukuru haina uwezo kabisa wa kupambana na rushwa. Na kwa kuanzia ni lazima bw. Hoseah ang'oke kwanza takukuru ndipo mambo mengine yafuate.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,584
  Trophy Points: 280
  Hivi mpaka sasa Takukuru imemchukulia nani hatua kutokana na majigambo yao haya?
   
 4. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hakuna kwa sababu wanatuhumiwa kuhusika na rushwa ni wana ccm. Ukitaka kuona efficiency ya Takukuru waambie wagombea wa upinzani wajihusishe na rushwa.
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  TAKUKURU kushindwa kukamata watoa rushwa ni sawa na kuhamasisha rushwa. Askofu Mokiwa kawapa taarifa kuwa rushwa inatembea, sasa ninyi zifanyieni kazi badala ya kubwabwaja tu.
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kama kutoa na kupokea rushwa ni kosa takukuru walitakiwa kuanza kuifanyia kazi taarifa za Askofu badala ya kupiga kelele magazetini. Alichofanya askofu ni kuwashtua takukuru kuwa rushwa inatembea fanyeni kazi.

  Issue ya Arusha imewatia Doa kabisa mnapewa taarifa mnalala, mnapewa taarifa mnakoroma tu, watu wanaandamana mpaka ofisini kwenu badalaya kuwasikiliza mnaita polisi ili kuwafukuza watu wanaowasaidia.
   
 7. minda

  minda JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Wednesday, 06 October 2010
  Leon Bahati

  TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imepinga kauli aliyotoa askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana, Valentino Mokiwa kwamba wananchi wakipewa fedha za rushwa na wagombea wapokee kwa kuwa si dhambi kula fedha za wajinga.

  Takukuru, ambayo inalalamikiwa kwa kutofanyia kazi taarifa za rushwa kwenye uchaguzi zinazotolewa na wananchi, imesema kwamba itamchukulia hatua kali mtu yeyote atakayetekeleza kauli hiyo ya Askofu Mokiwa kwa kuwa kupokea rushwa na kuvunja sheria.

  Akizindua mpango wa Bima ya Afya ya Imani kwa Watu Wenye Kipato cha Chini jijini Dar es Salaama juzi, Askofu

  Mokiwa aliwataka waumini wa kupokea na kula pesa zote zinazotolewa na wagombea wa nafasi mbalimbali katika kampeni zinazoendelea nchi nzima akisema "fedha za namna hiyo si dhambi, si haramu wala si rushwa".

  Lakini Askofu Mokiwa aliwaonya waumini kwamba fedha hizo zisiwafanye wawapigie kura wagombea wanaowapa fedha kwa kuwa wanaotoa rushwa hiyo ni "wajinga na kula fedha ya mjinga bila ya kumtekelezea azma yake si kosa".

  Kauli kama ya Askofu Mokiwa zimekuwa zikitolewa na hata wanasiasa ambao huwaeleza wananchi kuwa wapokee fedha zinazotolewa na wagombea, lakini waadhibu siku ya kupiga kura.
  Jana, ofisa uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani aliiambia Mwananchi kwamba sheria ya rushwa iko wazi na kwamba mtoaji na mpokeaji ni wahalifu.

  Kapwani alisema watakaofuata kauli zinazotolewa majukwaani wanaweza kujikuta matatani kwa sababu Takukuru ni chombo kilichoundwa kisheria na kinaongozwa kwa kanuni za sheria hiyo.
  “Sheria hii katika kifungu cha 15 inatamka wazi kuwa mtu yeyote anayetoa au kupokea hongo atakuwa ametenda kosa chini ya sheria hii,” alisema.

  Kutokana na hali hiyo, Kapwani aliwataka wananchi wanapowaona wagombea au mtu yeyote anayetoa rushwa watoe taarifa Takukuru ili hatua zinazofaa zichukuliwe.

  Source: Mwananchi
   
 8. C

  Chokona Member

  #8
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi hawa wenzetu wana akili ama ndo hivyo!! naomba kuuliza hivi ukimuonga mke wa mtu shillingi millioni naye akaipokea na asikutimizie matakwa yako, akachukua ile hela akampelekea mumewe na kumweleza chanzo,wakachukua hiyo hela na kuiweka katika badgeti yao je huyu mwanamama anahesabiwa mzinifu?
  Rushwa : tunaichukia rushwa na kuikataa kwa maana rushwa ni adui wa haki, inanunua na kuharibu haki na utu wa mtu hivi ni mbaya, lakini kama mtu kanipa hela akitaka nimtekelezee matakwa yake nami nikaichukua ile hela lakini nisimtekelezee matakwa yake kwa maana kwamba haki ikaendelea kuwa pale pale sioni kama hiyo ni rushwa maana hiyo hela haikusababisha kuuza au kununua haki kwa maana ingine, hiyo hela siyo adui wa haki na kwa hivyo si rushwa, jamani hawa takukuru hawaoni mantiki ndogo kama hiyo!!!
  Kama wanataka kuwatetea mafisadi kama kawaida yaho waseme, anyway si shangai maana wao mpaka kesho hawakuona rushwa yoyote katika mkataba wa richmond, na nashauri kwa nia njema kabisa Dr. Slaa akiingia Ikulu cha kwanza ni kupeleka mswada Bungeni wa kuvunja takukuru na kuundwa kwa chombo kingine cha kupambana na rushwa sio hiki tulichonacho sasa.
   
Loading...