Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,499
- 9,279
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mara imekamata dawa za binadamu zenye thamani ya zaidi ya Sh155.1 milioni ambazo zimeisha muda wake zikiwa zinauzwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
Kamanda wa Takukuru wa mkoa huo, Alex Kuhanda alisema jana kuwa dawa hizo zilikamatwa katika vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali na binafsi kuanzia Oktoba mwaka jana.
Alisema baada ya kupata taarifa za uwepo wa dawa hizo, ofisi yake iliamua kufanya uchunguzi na kubaini dawa hizo mbali na kuwepo katika vituo hivyo vya kutolea huduma.
Kuhanda alisema dawa hizo ziliisha matumizi tangu Agosti mwaka jana.
“Kutokana na hali hiyo, madaktari wawili walikamatwa na hivi sasa wako nje kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea, uchunguzi ukikamilika hatua za kisheria zitachukuliwa,” alisema Kuhanda.
Pia, alisema uchunguzi wa awali umebaini dawa hizo zilisambazwa muda mchache kabla ya kuisha muda wake kwa maelekezo ya kugawiwa bure ingawa zilipofika katika vituo hivyo zilianza kuuzwa kwa watumiaji.
Alisema dawa walizokamata ni za ‘antibayotiki’ kama vile ‘Amoxyline, Ampisiline na Chlorofenical’ dawa ambazo kiuhalisia zina uhitaji mkubwa katika jamii.
Alisema endapo utaratibu ungefuatwa ni vigumu kwa dawa kiasi hicho kuisha muda wake wa matumizi kabla ya kufikia watumiaji.
“Dawa zote, ni zile zinazotumiwa sana, hivyo ni vigumu kwa dawa kiasi hiki kuisha muda wake kabla ya kumfikia mtumiaji, hivyo kwa haraka haraka unaweza kubaini hapa kuna hujuma ya makusudi ilifanyika; kwa hiyo tunachunguza ili tubaini nani alizuia hizi dawa kugawiwa kwa wahitaji zikiwa bado muda wake wa matumizi unaendelea,” alisema Kuhanda.
Katika hatua nyingine, Kuhanda alisema ofisi yake pia inafanya uchunguzi wa tuhuma za ufisadi wa zaidi ya Sh15 bilioni fedha zilizotolewa na Serikali kwa Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji ndani ya mkoa huo.
Alisema wamebaini fedha hizo zimetumika kinyume cha utaratibu kwa kuwa lengo la upatikanaji wa maji bado halijafanikiwa katika maeneo yaliyolengwa, lakini fedha zimetumika bila kufuata utaratibu na kuzingatia thamani ya fedha.