TAKUKURU yaiomba Mahakama kwenda kumuhoji Mtuhumiwa gerezani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwenda gerezani kumuhoji mshtakiwa Alloyscious

Mandago katika kesi ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni mbili inayomkabili yeye na wenzake wanne.

Katika kesi hiyo, mshtakiwa Mandago anashtakiwa pamoja na mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali takriban Sh. Milioni saba kwa dakika, Mohamed Yusufali.

Wakili wa Serikali kutoka Takukuru Leonard Swai Maombi hayo amewasilisha maombi leo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Swai alidai, wapo hatua za mwisho za kukamilisha taarifa ili kuwasomea washtakiwa maelezo ya mashahidi(Commital). pia aliiomba mahakama kumuhoji mshtakiwa huyo akiwa gerezani.

Mahakama imeridhia mshtakiwa huyo kuhojiwa na kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 8, mwaka huu itakapikuja kwa ajili ya kutajwa. Mbali na Yusufali na Mandago washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni

Isaack Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif ambapo wanakabiliwa na mashtaka 39 likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni mbili.

Michuzi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom