Uchaguzi 2020 TAKUKURU yaingilia kati rushwa za baiskeli na pikipiki anazogawa Hamis Kigwangalla Nzega Vijijini

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
48,772
102,128
TAKUKURU wilayani Nzega wamezuia zoezi la ugawaji wa pikipiki na baiskeli lililokuwa likiendelea kwenye chuo cha Uuguzi, Kitongo Nzega.

Kwenye zoezi hilo, Katibu wa Mbunge wa Nzega vijijini Furaha Bazirio anahojiwa kwa tuhuma hizo za kutoa Rushwa ya pikipiki na baiskeli na kundi la wajumbe 43 toka kata ya Wela waliokuwa wamekusanyika kwenye eneo hilo wametakiwa kuondoka bila kuchukuwa zawadi.

Pia soma> Waziri Kigwangalla amwaga baiskeli Nzega

Kigwa.JPG
 
Nje ya mada..

Huyu jamaa mtozi naonaga tangazo la kipindi chake nikiwa nashangaa dira ya BBC.. ah nilivyoona mikogo yake tu na kipindi chake nikawazia atakuwa mtu wa namna gani... And now look! Here we are!
 
Pole sana jana Simba kwa kubanwa mbavu na Ruvu. Hata CHADEMA unayoshabikia Oktoba mwendo ni huo
 
Mtajuana wenyewe, pambaneni huko wee sisi tunawasubiri Mamati Kuu Dodoma...tutabaki na tunaowahitaji....wahamiaji hata mmoja hakatwi hata kama ana kura 2 jimboni...hutaki hama chama mapemaa.
 
Kigwangalla ananikumbusha mwaka 2010 alipopitishwa na chama chake cha CCM kugombea ubunge kwenye hilo Jimbo la Nzega huku akiwa ameshika nafasi ya 3! nyuma ya Husein Bashe (Msomali) na Mbunge aliyekuwa akitetea kiti chake (Lucas Seleli)
Seleli walimfanyia fitna sema tu jamaa ana utu sana, akakubali yeishe...

Ndani ya CCM yakikufika huna pa kwenda ndugu, unabakia na mkeo mnalia kwa kupokezana!!
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom