Takukuru yaburuza kortini watumishi wanne Stamigold

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,862
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Kagera, imewafi kisha mahakamani watumishi wanne wa Kampuni ya Stamigold kwa mashitaka ya matumizi mabaya ya ofi si, kujihusisha na vitendo vya rushwa na kuisababishia ofi si hasara ya Sh bilioni 1.1 mwaka 2016/2017.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera, John Joseph alisema watumishi hao walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya Biharamulo na aliwataja kuwa ni Dennis Sebugwao aliyekuwa Meneja Mkuu wa mgodi katika kipindi cha 2016/2017.

Mwingine ni Bwire Eliaseph ambaye alikuwa Ofisa Manunuzi wa Mgodi kipindi hicho, Sadick Kasuhya aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Clara Mwaikambo ambaye alikuwa Mkuu wa Idara ya Fedha kipindi hicho cha mwaka 2016/2017.

Alisema kuwa katika kipindi cha Juni 30, 2016 hadi Desemba 31, 2017, kwa nyakati tofauti wakiwa watumishi wa kampuni, walitumia vibaya nafasi zao na kuingia makubaliano ya mkataba baina ya Stamigold na Kampuni ya Supercore wenye thamani ya Sh bilioni 4.6 badala ya Sh bilion 3.4, hivyo kusababisha Kampuni ya Supercore kujipatia manufaa ya Sh bilion 1.1 na kuisababishia serikali hasara.

Mkuu huyo wa Takukuru wa mkoa alisema mkataba huo, ulihusu kuchoronga miamba katika mgodi wa kuchimba madini wa Stamigold uliopo Biharamulo. Kesi hiyo itatajwa tena Februari 25 mwaka huu.
 
Back
Top Bottom