TAKUKURU yabaini rushwa ya ngono kutawala katika upangaji wa vituo vya kazi vya walimu

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imebaini kughubikwa na vitendo vya rushwa ya ngono katika upangaji wa vituo vya kazi kwa waajiriwa wa idara ya elimu.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Sosthness Kibwengo akitoa taarifa kuhusu utendaji wa taasisi hiyo, amesema TAKUKURU imefanya uchambuzi katika mifumo sita ikiwemo mfumo wa elimu na kubaini uwepo wa mianya ya rushwa katika sekta hiyo.

“Tumebaini kuwa maeneo hatarishi ya uwepo wa rushwa ya ngono ni katika upangaji wa vituo vya kazi kwa asilimia 72,” amesema Kibwengo.

Aidha ameeleza kuwa eneo lingine hatarishi kwa uwepo wa rushwa ya ngono ni eneo la uhamisho wa walimu ndani ya halmashauri hiyo ambayo ni kwa asilimia 63.

Hata hivyo ameongeza kuwa taasisi hiyo imefuatilia utekelezaji wa miradi 41 ikiwemo sekta ya ujenzi, afya, maji na elimu yenye thamani ya shilingi bilioni 11.2 na kubaini miradi 10 ina upungufu ikiwemo vifaa viinavyotumika kutokidhi ubora.

Chanzo: Swahili Times
 
Hizo mambo mbona zipo toka kitambo sana miaka ya 1985 huko

Mtoto mzuri alipokuwa akiripoti katika halmashauri fulani wale wakubwa wanampanga hapo hapo mjini ili waendelee kumtumia, ila uzuri wa zamani hao jamaa walikuwa wanaoa kabisa. Kule vijijini ulikuwa huwezi kuona mwalimu mzuri wa kike tena mweupe kwa enzi hzo.
 
TAKUKURU ndio wanaongoza kwa kuchukua RUSHWA.

Muhimu mtoaji Rushwa huwa anaaamua Ni Nani hampendi, anataka kumkomesha Nani na Nani anataka Rushwa nafuu.
 
Hizo mambo mbona zipo toka kitambo sana miaka ya 1985 huko

Mtoto mzuri alipokuwa akiripoti katika halmashauri fulani wale wakubwa wanampanga hapo hapo mjini ili waendelee kumtumia,ila uzuri wa zamani hao jamaa walikuwa wanaoa kabisa,kule vijijini ulikuwa huwezi kuona mwalimu mzuri wa kike tena mweupe kwa enzi hzo
Brainwashed, kwani akiwa mweupe ndio anakuwa mzuri? Sema usingeona mwalimu wa kike mzuri, lakini ujue uzuri Ni mental constructed variable. Kizuri kwako sio kwa mwenzio
 
Brainwashed, kwani akiwa mweupe ndio anakuwa mzuri? Sema usingeona mwalimu wa kike mzuri, lakini ujue uzuri Ni mental constructed variable. Kizuri kwako sio kwa mwenzio
Hata ukichukulia miaka ya zamani wasichana weupe waliolewa kwa mali nyingi sana

Unazani walioleta carolight ni wajinga

Pole kwa kuzaliwa familia ya watu weusi,wanawake weusi mna bahati ya kupendwa na wazungu ila nao kuwapata sio raisi

Hata rais wako magufuri kila kukicha alikuwa akiwasifia wanawake weupe
 
Hata hivyo ameongeza kuwa taasisi hiyo imefuatilia utekelezaji wa miradi 41 ikiwemo sekta ya ujenzi, afya, maji na elimu yenye thamani ya shilingi bilioni 11.2 na kubaini miradi 10 ina upungufu ikiwemo vifaa viinavyotumika kutokidhi ubora.
 
Uwepo utaratibu wa kuwepo kisanduku ambacho zitawekwa vikaratasi vya vituo! kisha wahusika wanafoleni na kuingiza mkono kwenye kisanduku na kuchukua karatasi moja ya kituo atakachoenda!
 
Kwa hii nchi ilipofika, inabidi kila mzazi mwenye mtoto wa kike ajitahidi juu ya uwezo wake kumjengea uwezo wa kimawazo na kifedha pia ili kumuepusha na hizi changamoto zilizopo hasahasa kwenye vitu kama rushwa ya ngono.
 
Hata ukichukulia miaka ya zamani wasichana weupe waliolewa kwa mali nyingi sana

Unazani walioleta carolight ni wajinga

Pole kwa kuzaliwa familia ya watu weusi,wanawake weusi mna bahati ya kupendwa na wazungu ila nao kuwapata sio raisi

Hata rais wako magufuri kila kukicha alikuwa akiwasifia wanawake weupe
Una ulimbukeni mwingi saana,kwahiyo kwako weupe ni uzuri
 
Hizo mambo mbona zipo toka kitambo sana miaka ya 1985 huko

Mtoto mzuri alipokuwa akiripoti katika halmashauri fulani wale wakubwa wanampanga hapo hapo mjini ili waendelee kumtumia,ila uzuri wa zamani hao jamaa walikuwa wanaoa kabisa,kule vijijini ulikuwa huwezi kuona mwalimu mzuri wa kike tena mweupe kwa enzi hzo
khaaaaah
 
Back
Top Bottom