TAKUKURU yaanza kuichunguza CHADEMA kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,283
2,000
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imeanza kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, inazokikabili Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

“Kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo, kuna matumizi mabaya ya fedha za michango ya wanachama, ambayo kwa mujibu wa katiba yao wanadai imeanishwa wachangie.”

“Lakini, matumizi yake ndio wanatilia mashaka, kuna fedha nyingi zinatumika ndivyo sivyo, kwa mujibu wa makubaliano yao,” amesema Jenerali Mbungo.

“Kwa hiyo, tunachunguza matumizi yasiyo sahihi ya fedha zao, Takukuru inayomamlaka ya kuchunguza taasisi yoyote iwe ya umma, watu binafsi, chama, klabu, iwe chochote Takukuru wanaingia kufanya uchunguzi, ilimradi kuwe na ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha na rushwa,” amesema bosi huyo wa Takukuru.

Mbungo amewataja baadhi ya watakaohojiwa ni; Dk. Vincent Mashinji, aliyekuwa Katibu Mkuu Chadema, ambaye kwa sasa amehamia Chama cha Mapinduzi (CCM), John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki na Mambo ya Nje Chadema, pamoja na mhasibu mkuu wa chama hicho, Dk. Roderick Lutembeka.

Aidha, Jenerali Mbungo amesema wameshindwa kumhoji Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuhusu sakata hilo, kwa kuwa aliieleza TAKUKURU kwamba yuko nje ya jiji la Dar es Salaam.

Amesema, taasisi hiyo imeshaanza kukusanya nyaraka mbalimbali, zinazohusiana na tuhuma hizo.

“Tumeshapata nyaraka kutoka sehemu mbalimbali, wametupatia nyaraka, wamekuwa wanatoa ushirikiano katika hili,” amesema Mbungo.

Jumamosi ya tarehe 23 Mei 2020, Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, alikanusha tuhuma hizo, akisema kwamba, hakuna uthibitisho unaoonesha chama hicho kina matumizi mabaya ya fedha.

Kigaila alisema, fedha za michango ya wabunge na zinazotoka kwa wadau wengine wa Chadema, matumizi yake hupangwa na vikao vyake vya chama, wakati bajeti ya matumizi hayo ikipitishwa na baraza kuu, kisha taarifa zake hutolewa na kamati kuu ya chama hicho.

Kigaila alisema, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), hukagua taarifa za matumizi ya Chadema, na kwamba kwa mujibu wa ukaguzi huo, hakuna ushahidi kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.
 

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,524
2,000
Huyu mkuu wa takukuru pamoja na kuwa ametoka kwenye taasisi inayo heshimika kama JWTZ lakini amekubali kutumika kunyanyasa wananchi wasio na hatia kwa manufaa ya CCM.

Hii ndio hatari kubwa ya kutumia wanajeshi sehemu ambazo sio zao

Wakisha zoea kupindisha mambo ipo siku watapindisha sehemu siyo lwa manufaa yao wenyewe.

Wait and see.
 

Sumve 2015

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
3,645
2,000
Huyu mkuu wa takukuru pamoja na kuwa ametoka kwenye taasisi inayo heshimika kama JWTZ lakini amekubali kutumika kunyanyasa wananchi wasio na hatia kwa manufaa ya CCM.

Hii ndio hatari kubwa ya kutumia wanajeshi sehemu ambazo sio zao

Wakisha zoea kupindisha mambo ipo siku watapindisha sehemu siyo lwa manufaa yao wenyewe.

Wait and see.
Kwani si ni uchunguzi tu? kuna kitu hutaki tukijue baada ya kubainishwa na uchunguzi? kufanya kazi yao wanapopata malalamiko ni kutumika?
 

Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
4,757
2,000
Kwamba Mashinji huyu anayesusiwa salamu na akina Halima atahojiwa kuhusu chama cha akina Halima.

Kama hakuna upigaji ni vizuri au huo upigaji umhusu Mashinji pia tofauti na hapo hana sababu ya kutokuwachomea!
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,171
2,000
Huyu mkuu wa takukuru pamoja na kuwa ametoka kwenye taasisi inayo heshimika kama JWTZ lakini amekubali kutumika kunyanyasa wananchi wasio na hatia kwa manufaa ya CCM.

Hii ndio hatari kubwa ya kutumia wanajeshi sehemu ambazo sio zao

Wakisha zoea kupindisha mambo ipo siku watapindisha sehemu siyo lwa manufaa yao wenyewe.

Wait and see.
Tulia mkuu, kama hakuna ulaji na matumizi mabaya ya Fedha, si Itakuwa ni heshima Kwa Chadema na Mh M/kiti Sana?

Lakini pia umaarufu wa Chama si utapanda? Hofu ya nini mkuu

Tulia ukamliwe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom