TAKUKURU: Watu 8 wakiwamo Watumishi 7 wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kushitakiwa kwa makosa ya rushwa na Uhujumu Uchumi

Ma-tamthilia yanaendelea, huwa nasikitika sana nikikumbuka ishu ya yule askari aliyefukuzwa kazi baada ya video yake akipokea rushwa kutoka kwa dereva wa daladala kusambaa.

Nasikitika Kwasababu alitolewa kafara wakati kuna watu wanapiga mipunga mizito inayoadhiri karibia kila MTANZANIA.

Hivi wale waliopunguza gawio la SERIKALI kwenye madini wako wapi?...
Piga rushwa kubwa uwe salama.
 
naomba mwenye konection ya ajira/vibarua bandarini. nahtaji kufanya kaz huko
 
Batch no 2 hiyo ya kufungia mhula imeingia tumeanza na MSD,NEMC NA TPA, za watu binafsi zimeisha sasa
 
Ma-tamthilia yanaendelea, huwa nasikitika sana nikikumbuka ishu ya yule askari aliyefukuzwa kazi baada ya video yake akipokea rushwa kutoka kwa dereva wa daladala kusambaa.

Nasikitika Kwasababu alitolewa kafara wakati kuna watu wanapiga mipunga mizito inayoadhiri karibia kila MTANZANIA.

Hivi wale waliopunguza gawio la SERIKALI kwenye madini wako wapi?

Wale waliomsafirisha Twiga mpaka Uarabuni, je?

Lugumi naye alipotelea wapi?

Yule mkubwa na zile pesa za pembejeo?!

HUU MSUMENO WA TAKUKURU UKO UPANDE MMOJA TU?
Leo mko Kasi kwa CHADEMA wakati masoo kibao mmeyalia ganzi?

Elf 2 kwa nesi au daktari au askari anapoteza ajira na jela inamsubiri wakati kuna watu WALITIA SAINI MIKATABA MIBOVU YENYE HARUFU YA RUSHWA LEO BADO WAPO NA VYEO BUNGENI.

NB:
SITETEI KUPOKEA WALA KUTOA RUSHWA YA AINA WALA KIASI CHOCHOTE BALI HAYA NI MAWAZO YANGU YA RUSHWA INAVYOSHUGHULIKIWA HAPA KWETU TZ.
kwahio ilitaka huyu askari aachwe. mbona unashindwa ku reason. kutokamatwa kwa wengine hakumfanyi huyo asksri kuachwa
 
Hapo ndipo ma-jobless kama mimi hua tunafarijika kama vile tutafaidika na chochote kwenye inshu hio.
Mkuu bora tulime tupambane na tembo na mvua na jua..

Hata matuhuma haya siyo mazuri..

Everyday is Saturday....................... :cool:
 
JF siku hizi raha sana! Enzi zile hapa watu wangekuwa wanaweka vidokezo kuhusu "uhusika" wa watuhumiwa! Sasa hivi tunaponda tu, hii inaweza dalili ya kuwa tumegundua kuwa hela za mafisadi zilikuwa zinafanya maisha yetu kuwa "mepesi" nawaza tu wakuu!
Double standard mkuu
 
Back
Top Bottom