Takukuru watawachunguza mawaziri watuhumiwa! Walikuwa wapi hadi mambo yanafika hapa?

Tanzania nchi ya usanii na kudanganyana. Nani angeamini kuwa TAKUKURU ingekuja na kamba kuwa itawachunguza mawaziri watuhumiwa wa ripoti ya CAG.

Hivi Takukuru walikuwa wapi wakati wote huu au wanatafuta kuwatoa chochote kitu? Je Takukuru licha ya kupaswa kuvunjwa ina udhu wa kumchunguza mtu tena kigogo wa CCM na serikali? Nani anamdanganya nani?

Vyombo vya habari vilimnukuu mkurugenzi wa Takukuru Edward Hosea akisema, "Sheria inatutaka tufanye uchunguzi wa tuhuma zozote na katika hili, CAG alitakiwa atupe taarifa. Lakini sisi baada ya kusikia bungeni tulimwandikia barua (CAG) kumwomba atupatie ripoti ya mambo yanayotuhusu tuanze kuyashughulikia haraka

Aliyeanzisha hii taasisi (TAKUKURU) hakufikiri vizuri. Wafanyakazi na watumishi wanaoteuliwa ni zao serikali hivyo Serikali kuanzisha taasisi ya kukamata watumishi wezi na wapokea rushwa ni ushahidi kwamba Serikali inaajili na kuteua watumishi wezi na wapokea rushwa. Je kwa kuwa imebainika kimazingira kuwa jamaa (TAKUKURU) nao wanachukua kitu kidogo serikali itataka iunde taasisi nyingine ya kuwamonitor TAKUKURU?
 
Tanzania nayo! Huyu mbabaishaji anayeitwa Dr. Hosea sijui imemuokotea wapi. Si mpinga rushwa...ni mfadhili wa wala rushwa. Hakustahili kabisa kuiongoza PCCB
Italeta maana kama atamchunguza CAG, maana taarifa zote zimefanyiwa uchunguzi wa kitaalam na CAG
 
Wacheni TAKUKURU wafanye kazi yao. Na wao hawapo juu ya sheria kila mtu ni presumed innocent until proven guilty. Hawana uwezo wa kuhukumu wao ni kuchunguza na kama wakiona kuna case wanashitaki kwa vyombo husika.
 
TAKUKURU wenyewe choka mbaya hawana lolote kwani hata posho za kuendeshea ofisi hawana posho zenyewe za wafanyakazi hawazipati kwa wakati ubaguzi umewajaa kiasi cha kubaguana katika kazi za uchunguzi kama hizo ,fuatilia utakuta watoto ama ndugu wa vigogo ndio walio katika timu za uchunguzi huo,fikiria hata wanasheria wao hawajapata pesa za suti za mahakamani je hizo kesi zitaendeshwa wakiwa uchi?uozo mtupu kudumaza taaluma za watumishi wake u na kukuza majungu,ovyooooooooooooooooooooooooooooooooooo!
 
Ukweli ni kwamba hata TAKUKURU nao wachunguzwe matumizi yao ya pesa za bajeti wanazopewa kwani kuna ufisadi wa kutosha mfano vigogo kusoma kozi mbalimbali kwa kujilipia pesa za ofisi,safari zisizo za msingi ndani na nje ya nchi,tenda nyingi za vifaa vya ofisi visivyo na ubora,uhamisho wa watumishi usio na tija etc,kwa kweli hata wafanyakazi hawana uuwiano wa kimaendeleo na maisha yao ni duni je kutakuwa na ufanisi wa kazi hapo?
 
CAg wachunguze TAKUKURU kwanza ndipo na wao wakiwa safi ktk matumizi yao ndipo na wao wakawachunguze hao mafisadi <ok!OSEAH WE HAVE TYRED OF UUUUUUUUUUUUUUUUUUU>
 
Nimesoma comments humu na nimegundua ni kwa kiasi gani watanzania wengi hawajui kupambanua mambo badala yake wanaushabiki ambao hautasidia kitu. Pia wanauelewa mdogo sana wa mambo. Karibu comments zote zilizoandikwa ni za kufikirika na hazina ukweli. Watu hawafahamu muundo na majukumu ya TAKUKURU, hawajui mfumo na utendaji wa Taasisi hii na hawafahamu muundo na utendaji wa taasisi nyingine zinazofanya kazi na TAKUKURU kama mahakama, CAG, DPP, IKULU, na ndio maana wanatoa maelezo yasiyoshikika. Ni vema tujifunze zaidi elimu ya uraia ili tuelewe kiini cha tatizo la kimuundo ili tutoe hoja za msingi na zitakazojenga kuliko za kuwapaka watu matope. Kuna mchakato wa katiba mpya sasa jamani....Tubadilike na teknolojia itusaidie badala ya kuitumia vibaya. Tchao
 
Takukuru nadhani ni joka la kibisa!! halina maana kabsaa

Asee takukuru tunaweza kuwalaumu sana, sawa pia tunavyozilaumu taasisi nyingine kama tume ya maadili, haki za binadamu, polisi, mahakama, nk lakini tatizo kubwa siyo hizi taasisi bali ni mfumo uliopo. Mfumo wa wakuu wa hizi taasisi za umma kuteuliwa na rais kunazinyima uhuru wa kutenda haki hasa pale inapokuwa serikali inabanwa.

Mteule wa rais lazima atafuata maagizo kutoka kwa aliyemteua tu hakuna jingine, ni wachache sana wanaweza kuwa na msimamo hata kupingana na maagizo batili ya waliowateua na hapa ndo unasikia mtu kajiuzulu nafasi yake.

Lakini kwa tamaduni zetu na njaa tunayokuwa nayo, mtu yupo tayari kufuata maagizo kutoka juu hata kama ni kunyume kabisa na ustaarabu na haki za watu wengine. Kwa hiyo mfumo huu ubadilike kwanza na katiba mpya ilenge maeneo kama haya.

Viongozi/Watendaji wa taasisi muhimu kama hizi na nyingine wawe wanaomba na kuajiriwa kwa kushindanishwa, ila kuzipa uhuru kamili wa kutenda haki.
 
Tanzania nchi ya usanii na kudanganyana. Nani angeamini kuwa TAKUKURU ingekuja na kamba kuwa itawachunguza mawaziri watuhumiwa wa ripoti ya CAG.

Hivi Takukuru walikuwa wapi wakati wote huu au wanatafuta kuwatoa chochote kitu? Je Takukuru licha ya kupaswa kuvunjwa ina udhu wa kumchunguza mtu tena kigogo wa CCM na serikali? Nani anamdanganya nani?

Vyombo vya habari vilimnukuu mkurugenzi wa Takukuru Edward Hosea akisema, “Sheria inatutaka tufanye uchunguzi wa tuhuma zozote na katika hili, CAG alitakiwa atupe taarifa. Lakini sisi baada ya kusikia bungeni tulimwandikia barua (CAG) kumwomba atupatie ripoti ya mambo yanayotuhusu tuanze kuyashughulikia haraka

Here we go. Inaonekana kuwa vyombo vya Serikali havina coordination. Hongera JK kwa kujenga mazingira
 
Back
Top Bottom