Takukuru watawachunguza mawaziri watuhumiwa! Walikuwa wapi hadi mambo yanafika hapa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takukuru watawachunguza mawaziri watuhumiwa! Walikuwa wapi hadi mambo yanafika hapa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpayukaji, May 1, 2012.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tanzania nchi ya usanii na kudanganyana. Nani angeamini kuwa TAKUKURU ingekuja na kamba kuwa itawachunguza mawaziri watuhumiwa wa ripoti ya CAG.

  Hivi Takukuru walikuwa wapi wakati wote huu au wanatafuta kuwatoa chochote kitu? Je Takukuru licha ya kupaswa kuvunjwa ina udhu wa kumchunguza mtu tena kigogo wa CCM na serikali? Nani anamdanganya nani?

  Vyombo vya habari vilimnukuu mkurugenzi wa Takukuru Edward Hosea akisema, "Sheria inatutaka tufanye uchunguzi wa tuhuma zozote na katika hili, CAG alitakiwa atupe taarifa. Lakini sisi baada ya kusikia bungeni tulimwandikia barua (CAG) kumwomba atupatie ripoti ya mambo yanayotuhusu tuanze kuyashughulikia haraka
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hakuna ubaya wa Maige na Ngeleja kumiliki mijengo ya malaki ya dola bana....hata kama maelezo yao hayaeleweki.
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Takukuru nadhani ni joka la kibisa!! halina maana kabsaa
   
 4. M

  Mngendalyasota Senior Member

  #4
  May 1, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TAKUKURU ivunjwe kwani wanakula hela ya walalahoi pasipo kufanya kazi.Kwa mfano nimeona vijana wadogo kabisa walioajiriwa miaka ya karibuni tu PCCB Mbinga-Songea wameshanunua magari ya kutembelea, hii inaonesha kwamba wanapeana tu mahela mengi bila kutekeleza wajibu wa kukamata wahalifu wanaotafuna nchi yetu.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,665
  Likes Received: 82,490
  Trophy Points: 280
  ....Taasisi nzima ni ya kufungwa tu haina maana yoyote. Wanapewa bajeti kubwa sana ya kupambana na ufisadi/rushwa lakini hadi hii leo hakuna hata moja walilolifanya zaidi ya usanii tu na huku ufisadi na rushwa vikiendelea kushamiri nchini kwa kasi ya kutisha.
   
 6. M

  Mngendalyasota Senior Member

  #6
  May 1, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  PCCB wameshindwa kukamata mkurugenzi wa Njombe Town council kutokana na ujenzi wa daraja chini ya viwango hata baada ya Mwamri kukataa kukabidhiwa lile daraja. Kibaya zaidi ni ndani ya jimbo la biroboto ambaye tangu uhuru wilaya yake ya Njombe haina barabara ya rami hata moja.
   
 7. p

  politiki JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Takukuru hii ambayo kamati ya Bunge ya kuichunguza Richmond ilipendekeza mkurugenzi na wenzake watimuliwe kazi kwa kushindwa kuona rushwa iliyokuwa wazi ??
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  binafsi sina imani na TAKUKURU so vyovyote watakavyofanya ndio hao hao...TAKUKURU wanateuliwa na serikali ambayo iko chini ya chama tawala CCM hakuna kitu hapo:A S-fire1:
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]
  [/FONT]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 30 April 2012 20:35[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]


  [​IMG]
  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah
  Boniface Meena
  SAKATA la ufisadi ulioanikwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), limeingia sura mpya baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuanza kuwachunguza watendaji wote waliohusika, wakiwamo mawaziri.

  Hatua hiyo ya Takukuru imekuja wakati tayari Kamati Kuu (CC) ya CCM imebariki uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kulisuka upya Baraza la Mawaziri kama hatua mojawapo katika kutekeleza maazimio ya Bunge kutaka mawaziri wanane na watendaji waliotajwa katika ripoti ya CAG wawajibishwe.

  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alisema jana kuwa pamoja na hatua ya Rais ya kufanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri, taasisi hiyo imeanza uchunguzi wake dhidi ya wahusika.

  Dk Hoseah alisema ofisi yake imeshaanza kushughulikia tuhuma zote za rushwa zilizotolewa na CAG na baadaye kupigiwa kelele na wabunge ili watakaobainika wafikishwe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

  “Sheria inatutaka tufanye uchunguzi wa tuhuma zozote na katika hili, CAG alitakiwa atupe taarifa. Lakini sisi baada ya kusikia bungeni tulimwandikia barua (CAG) kumwomba atupatie ripoti ya mambo yanayotuhusu tuanze kuyashughulikia haraka,” alisema Dk Hoseah.

  Hata hivyo, Dk Hoseah alisema asingeweza kuwataja watu wanaowachunguza kwa majina, kwa kuwa sheria (Kifungu cha 37 cha Sheria ya Takukuru ya mwaka 2007, kinazuia kuzungumzia mchakato wa uchunguzi).

  Lakini, mawaziri waliotajwa katika ripoti hiyo ya CAG na hivyo kushinikizwa kujiuzulu ni William Ngeleja wa Nishati na Madini na Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu.

  Wengine ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), George Mkuchika; Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami.

  “Siwezi kusema tunamchunguza nani kwani sheria hairuhusu ila elewa tu kwamba tuko serious (makini) na tunafanyia kazi tuhuma zote na wote tutahakikisha tunawafikia,” alisema Dk Hoseah.

  CAG akiri

  Kwa upande wake CAG, Ludovick Utouh alikiri kuwasiliana na Takukuru kuhusu kuwachunguza wote waliotajwa katika ripoti yake.

  “Kimsingi ofisi yangu inafanya kazi kwa karibu na Takukuru na barua waliyotuandikia tunaendelea kuifanyia kazi. Sheria inatueleza kwamba katika ukaguzi wetu, tunapokutana na suala lolote la rushwa tuliwasilishe Takukuru na tumekuwa tukifanya hivyo,” alisema Utouh.

  Awali, wakati sakata hilo likiwa bungeni, kuliibuka malumbano ya hapa na pale miongoni mwa mawaziri na wasaidizi wao huku watendaji hao wa wizara, wakitupiana mpira kuhusu kashfa mbalimbali zinazoelekezwa kwenye ofisi zao.

  Kashfa za mawaziri
  Waziri Nundu na Naibu wake, Athuman Mfutakamba kwa upande mmoja na Waziri Chami na Naibu wake, Lazaro Nyalandu walianza kutupiana mpira huku kila mmoja akijisafisha kiaina.

  Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu katika utetezi wake alisema Naibu wake huyo amekuwa akishinikiza Kampuni ya China Communication Construction Company (CCCC), ipewe kazi ya kujenga gati namba 13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam kwa kuwa ilimgharamia safari kadhaa kwenda nje.

  Waziri Nundu pia alishangazwa na shinikizo la Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu chini ya Mwenyekiti wake, Peter Serukamba kuingia na kushinikiza CCCC ipewe kazi hiyo huku akihoji kuna nini?

  Hata hivyo, Mfutakamba alipoulizwa kuhusu safari zake hizo za nje kugharamiwa na CCCC na baadaye kuandika ripoti akishinikiza ipewe kazi ya kujenga gati hizo, alikiri kusafirishwa na kampuni hiyo, lakini akasema alifuata taratibu zote za kiserikali.

  Nyalandu kwa upande wake, alionekana kutua mzigo wa kashfa ulioigubika wizara hiyo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege kudaiwa kuiingizia Serikali hasara ya karibu Sh30 milioni kwa ukaguzi hewa wa magari nje ya nchi akisema alimshauri Waziri wake, Dk Chami kumsimamisha kazi mkurugenzi huyo mapema.

  Lakini Dk Chami alisema hadi Bunge linamalizika mjini Dodoma, alikuwa hajaiona ripoti ya Kamati ndogo ya Bunge iliyomchunguza Ekelege ambayo alisema ingemsaidia kupata tuhuma zinazomkabili mkurugenzi huyo ili kuchukua hatua.

  Mkulo ambaye alikuwa waziri wa kwanza kutakiwa ajiuzulu, anatuhumiwa kuvunja Bodi ya Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC) ili kuficha tuhuma zake ikiwemo uuzaji wa kiwanja Na.10 kwa Kampuni ya Mohamed Enterprises (MeTL).

  Mkuchika alitakiwa aachie ngazi baada ya ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) kubaini mtandao mkubwa wa wezi wa mali za umma. Ripoti hiyo ilibainisha kuwa kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2010, Sh583.2 milioni zililipwa kama mishahara hewa, kiasi ambacho kingetosha kujenga madarasa 194.

  Ripoti ya CAG ilibaini kuwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa mwaka mmoja wa fedha linafanya ununuzi wenye thamani ya Sh300 bilioni hadi Sh600bilioni, hivyo kumtaka Waziri Ngeleja awajibike.

  Katika mwaka wa fedha 2009/2010, Tanesco ililitumia Sh1.8bilioni ukilinganisha na Sh65 milioni zilizokuwa zimepangwa katika bajeti ya ukarabati wa gati mojawapo katika Kituo cha Bwawa la Mtera na kuingia mikataba isiyo na tija kwa taifa.

  Waziri Maige anakabiliwa na tuhuma za kutengeneza mazingira ya rushwa katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji, ambao inadaiwa ulitawaliwa na dosari nyingi ikiwa ni pamoja na kutangaza majina ya waliopata vitalu bila kuonyesha maeneo waliyopewa.

  Pia, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili ilieleza kuwa kampuni 16 zilizopewa vitalu hivyo hazikuomba na kwamba vitalu hivyo vilikuwa vya daraja la kwanza na la pili.

  Mbali na tuhuma hizo, Maige pia anakabiliwa na kashfa ya kununua nyumba kwa Dola za Marekani 700,000 iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam, tuhuma ambazo alizipinga na kusema kuwa nyumba hiyo ameinunua kwa Dola 410,000, (wastani wa Sh600 milioni).

  Waziri Mponda ametakiwa kuwajika baada ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), ambako ukaguzi maalumu wa MSD uliofanyika kubaini kuwapo tofauti ya Sh658.9 milioni ikiwa ni pungufu ya kiasi ambacho kilipokewa na kuripotiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwenda MSD na ushahidi wa kupokewa haukutolewa.

  Pia kulikuwa na kiasi cha Sh100 milioni kilichopelekwa na MSD kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kikatumiwa na MSD bila kuwapo na mchanganuo wa matumizi.

  Ukaguzi maalumu ulibaini pia kuwapo kiasi cha Sh4.5 bilioni zilizotoka Hazina kwenda Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa vya hospitali, lakini ni kiasi cha Sh4.344 bilioni tu kilichopokewa na MSD ikiacha Sh196 milioni bila kuwepo na ushahidi wa kupokewa na MSD kutoka wizarani.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Itawapeleka Mahakamani na kuwashitaki?
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  another circus in the making.......... walikua wapi siku zote???

  kupoteza tu pesa ya taifa kwa maigizo...

  TAKOKURU INATAKIWA KUFUTA, WITH OR WITHOUT IT RUSHWA IMEONGEZEKA
   
 12. O-man

  O-man JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 318
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ni kweli maigizo. Mwisho wa siku wote wanapata clean bill of health! Why the funfare? Nachukia sana mtu kunifanya mimi ***** na mali zangu.
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  TAKUKURU haifai kabisa.

  Hapo wameshaona kuna mshiko.
   
 14. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  Ukitaka kujua takukuru inapambana nenda kwenya magesti. Vitanda vya misaipras wala ata avifai!
   
 15. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hii si ndio TAKOKURU iliyosema Richmond ilikuwa clean. It is useless.
   
 16. RUBERTS

  RUBERTS Senior Member

  #16
  May 1, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  TAKUKURU ni kijiwe cha kuhalalisha ufisadi. Walimshindwa Andrew Chenge licha ya vielelezo vya kumwaga, watamchunguza nani na kumshitaki nani kati ya hawa mawaziri? Pamoja na serikali ya Uingereza kurejesha chenji bado TAKUKURU hawajachukua hatua yoyote. Katika nchi hii naona Chenge yupo juu ya sheria. Wakae kimya huko, hawana wanaloliweza. Eti CAG awapelekee taarifa wakati taarifa ziko kila mahali kwenye ripoti yake. Wanataka wachunguze nini wakati hela zimeishaliwa na wao wako hapo? Hawa wanataka wakapozwe na wao. Tena inabidi wachunguzwe wao kwanza na hatimaye ivunjwe.
   
 17. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Takukuru hawana lolote,ninawadharau sana.
   
 18. Higash

  Higash JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  takukuru wenyewe wachunguzwe ni walarushwa wa kutupwa.
   
 19. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Takukuruuuu mnaamka saa hizi??kweli usingizi mtamu jamani!!!mnaonea watendaji wa vijiji na watendaji wilayani mafisadi papa yanaranda tu mijini ,kweli kazi ipo!!
   
 20. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanatafuta namna ya kuwasafisha.
   
Loading...