Takukuru washindwa kuwachunguza mafisadi sasa wawageukia maaskofu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takukuru washindwa kuwachunguza mafisadi sasa wawageukia maaskofu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by 2015ready, May 1, 2011.

 1. 2015ready

  2015ready JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Subject: Re: TAKUKURU WASHINDWA KUWACHUNGUZA MAFISADI SASA WAWAGEUKIA MAASKOFU?

  Habari za uhakika ni kuwa baada ya kuona maaskofu wengi wakipiga vita dhidi ya ufisadi, mipango imeandaliwa kuanza kuwachunguza maaskofu na makanisa yao pamoja na kubaini mali zao na jinsi walivyozipata. Katika jitihada zao chafu za kuwanyamazisha, taasisi ya kuzuia rushwa sasa imeanza mikakati hiyo michafu kwa kumhoji Askofu mmoja wa jijini Mwanza ambaye kwa takriban masaa manne alijikuta akihojiwa na maafisa hao katika jengo moja kubwa ambalo hapo nyuma lilikuwa likitumiwa na TRA. Mahojiano hayo yalifanyika siku ya alhamisi tarehe 21, 2011 kabla ijumaa kuu majira ya saa tatu asubuhi hadi alasiri.

  Katika mahojiano hayo, nyepesi nyepesi tulizozipata zinasema kuwa pamoja na mambo mengine walitaka kujua mali za askofu huyo, na jinsi alivyozipata mali hizo. Kwa jinsi askofu huyo alivyo mwadilifu alitoa ushirikiano kwa yote waliyoyahitaji.

  Inasemekana kuwa zoezi hilo si rasmi ila kuna agenda za kumdhoofisha askofu huyo katika mikakati yake ya kuielimisha jamii juu ya mambo mbali mbali yahusuyo imani ya dini, maadili mema, utaifa na maendeleo katika jamii.

  Katika kipindi cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka jana, askofu huyo alifanya mkutano mkubwa sana wa kuiombea nchi uliohusisha makanisa yote ya jiji la Mwanza......
  Inasemekana kuwa mafundisho yake kwenye moja ya radio za hapa Mwanza, yamegusa maslahi ya baadhi ya viongozi wa kidini na kiserikali na hivyo mikakati ya kumnyamazisha na hata kufunga kituo cha radio imeandaliwa......

  Hii inaonekana kuwa ni mikakati ya kimakusudi inayolenga kuwanyamazisha viongozi wa kidini katika suala zima la kuielimisha jamii katika nyanja mbali mbali...

  Pia tumesikia kuwa askofu huyo kwa sasa amesafiri nje ya nchi kwa mambo ya utume na ya kuwa TAKUKURU wamekuwa wakimtafuta awapatie namba za akaunti za benki za familia yake, pamoja na nakala ya cheti cha kuandikishwa kwa kanisa analoliongoza na mambo mengine.

  Tunahoji, Je, TAKUKURU ni chombo sahihi cha kuchunguza taasisi za kidini,? Kama ni sehemu ya kazi yao, mbona hatuoni wala kusikia jitihada hizo hizo zilizotumika kwa askofu huyu zikitumika kuwahoji mafisadi ambao majina yao yamekuwa yakitajwa kila kukicha? Kwa hilo tunapata picha kuwa TAKUKURU inatumia fedha za walipa kodi vibaya kwa kushughukia mambo yasiyo na tija kwa Taifa, wakati yale yenye tija yakiachwa.

  Namba za simu za afisa ambaye amelivalia njuga jambo hili ni 0755 846 306 anayejulikana kwa jina la Bukuku.

  Tunafanya jitihada za kumpata askofu huyo (_______) na mara tukimpata tutawarushia taarifa zaidi.
  HABARI HII SIYO YA KUIDHARAU NI KISA CHA KWELI KIMETOKEA MWANZA.
  Wana JF - Naomba tulijadili hili suala maana linahusiana kabisa na siasa za chama cha magamba - ccm.
   
 2. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  hahahahah
  dahhhh kushinda TZ ngumu sana
  Je wameanza kuchunguza ya Ridhiwani au ndo yameisha?? (wameyachimbia)
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,609
  Trophy Points: 280
  Mhhhh! Huu ni ushahidi mwingine wa wazi kwamba Mafisadi wameshika hatamu! Yaani hata wamefikia kuwatisha maaskofu wanaokemea ufisadi! wakati mafisadi chungu nzima ndani ya Chama na Serikali wanaendelea kupeta tu!
   
 4. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  dawa ya hawa vibaraka wa kikwete ni kuwanyima ushilikiano na kuwatenga katika jamii,
  na mtu ukipata nyeti zao ni kuzitupa hewani, mbona kikwete kaboma kutaja mali zake hakuna anayemgusa
  na majina ya wauza unga kayakalia ikulu hanakuna anayemuuliza
   
 5. 2015ready

  2015ready JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Inabidi sasa tutumie nguvu za maombi ili kuwang'oa mafisadi wote.
  Kikwete, tunakupa siku sitini (60) ili uwashughulikie mafisadi wote na siku saba (7) uwazuie hao vibaraka wako wa "TAKUKURU" kuwasumbua watumishi wa Mungu.
  Taarifa kwa wana maombi wote nchini Tanzania, hii ni vita dhidi ya wachungaji na watumishi wa Bwana. Wao wanatuombea siku toze, sasa ni zamu yetu kuwaombea wao.
  Acts 4:18-20 (New King James Version)

  18 So they called them and commanded them not to speak at all nor teach in the name of Jesus. 19 But Peter and John answered and said to them, "Whether it is right in the sight of God to listen to you more than to God, you judge. 20 For we cannot but speak the things which we have seen and heard."


   
 6. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndiyo serikali ya kifisadi inavyo-operate. Wanaacha kupambana na mafisadi halisi badala yake wanawasumbua watumishi wa Mungu. TAKUKURU ianze na watumishi wa umma kwanza wanaoishi maisha ya peponi katikati ya maskini.
   
 7. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kha! Walah siamini kama inaweza kufikia hatua hii, Yani mafisadi lukuki kila kona wanajinehemesha jasho la walalahoi. Walah siamini kama mapadri wana anziwa na takukuru.
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kazi ipo kwa kweli khaaaa.sijawai kuona nchi inaingia kwenye mkanganyiko kama sasa...yaani TAKUKURU kuchungua maaskofu? basi kuna siku watataka CAG akamfanyie auditing babu kule Loliondo
   
 9. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tunasafari ndefu, lakini mkanganyiko huu ndo mwanzo wa mwisho wa serikali katili ya ccm. Sote watanzania tuendelee kupashana habari, kuungana na hatimaye tuikomboe nchi yetu kutoka kwa madharimu hawa. Tuhakikishe tunakuwa wamoja na kuunga mkono jitihada za yeyote anayenyanyaswa na serikali ya ccm kwa ajili ya jitihada zake za kuelimisha umma, awe mtumishi wa mungu au taasisi yeyote au mtu binafsi!! Tuwe tayari kuanguka naye pamoja. Mungu ibariki tanzania yetu...
   
 10. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,036
  Likes Received: 8,526
  Trophy Points: 280
  Nasikia pengo naye ni fisadi mkubwa naomba takukuru
  wamchunguze huyu mtu haraka sana
   
 11. katabu

  katabu JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wanajitafutia mabalaa hao!!. Nitatizo la vyombo vyetu vya dola kutokuwa huru. Mpaka mkubwa flani aseme, nd'o wanafanya vile walivyo agizwa. Hata kama maagizo mengine hayana kichwa wala miguu.
   
 12. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Inaonekana kawashika pabaya eti???na bado mwaka huu
   
 13. d

  dkn Senior Member

  #13
  May 1, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ufisadi uko kila mahali inabidi tukubali, lakini strategy ya serikali kuitumia Takukuru kunyamazisha mashirika ya kidini ni upumbavu wa hali ya juu na hii Takukuru inabidi iwe huru na ivunjwe mara moja. Fedha zinazofujwa serikalini kama mtoto wa JK kuwa bilionea na leo unamfuata Askofu au kiongozi yoyote wa kidini umefuja pesa....amezitoa serikalini? haya ni mashirika ya kidini kama ilivyo kwa OIC, sijui Rome wanatoa misaada mingi ya kijamii kwenye dini zao ziwafikie walengwa wote na inatokea mara nyingine pesa kuchakachuliwa na viongozi wa dini ila uhalali wa kuhoji ungeanzia na kwa wahisani si takukuru au takukuru ishirikishwe kwa kuombwa siyo kujitokeza na kuanza kushambulia viongozi wa kidini ambao wakuwa mstari wa mbele kupinga ufisadi sasa wanataka kuanzisha vita za kidini na serikali ambayo serikali ikicheza karata vibaya itakula kwao kwani viongozi wa kidini wana nguvu kubwa sana ya kuwashinikiza waaumini wao wapi pa kwenda.
   
 14. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #14
  May 1, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Be demonstrative,how far are you sure about his embezzlement.
   
 15. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,036
  Likes Received: 8,526
  Trophy Points: 280
  kanisa linaendeshwa kwa pesa za walipakodi rejea pesa serikali imetoa kwa kanisa majuzi bilioni 60.so takukuru wana haki kisheria kufuatilia kama hao maskofu wanatumia vibaya hela hiyo lazma wawajibike
   
 16. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hilo jengo la TRA ya zamani ndipo zilipo ofis za mwanasheria mkuu wa serikali mkoa wa mwanza,ni karibu na geti la kuingilia uwanja wa nyamagana
   
 17. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Ni udhalilishaji sana wa kanisa sijui kwa nini kanisa limekaa kimya!!!takukuru wache kutumiwa kisiasa kwanza Hosea anaetoa maamuzi hayo hatakiwa kuwepo pale acha avute vute muda maana naye tunamsubiria pale kisutu siku yake yaja soon ngoja jk atoke atatinga tu
   
 18. ADAM MILLINGA

  ADAM MILLINGA Senior Member

  #18
  May 1, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kabla ya kuropoka kaa na mkeo ushauriane nae hacha kuropoka tabia za madada
   
 19. ADAM MILLINGA

  ADAM MILLINGA Senior Member

  #19
  May 1, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KAMA WAMESHNDWA KAZ WASEME MAASKOF TUNAWAJUA NASIS NDO WATOA Sadaka hvyo TAKUKURU AIWAUSU WAKAMCHUNGUZE RIDHIWAN KAMA WAO VIDUME MSIUE DAGAA ANZA NA SANGARA MSIWAPE MBWA CHAKULA CHA WATOTO
   
 20. T

  Tyegelo Member

  #20
  May 1, 2011
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninaandika nikiwa sifungamani na upande wowote. TAKUKURU kama wamepokea taarifa kwamba mtumishi wa Bwana anamiliki kiasi cha mali ambacho hakilingani na vipato vyake vyote halali, ina jukumu,kisheria, kufanya upelelezi kwa lengo la kukusanya ushahidi (ikiwa ni pamoja na kumhoji mtuhumiwa) ili kuithibitisha au kutoithibitisha taarifa pokelewa. TAKUKURU kama wamezikalia taarifa za mafisadi kutenda vitendo vya ruswa ni kosa, lakini kosa hili haliwezi kuhalalisha kuwa taarifa ya mtumishi wa Bwana kujilimbikizia mali isifanyiwe upelelezi.
   
Loading...