Takukuru wana ubavu kuingilia rushwa katika Uchaguzi Mkuu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takukuru wana ubavu kuingilia rushwa katika Uchaguzi Mkuu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Aug 17, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Wadau, mara kadha nimekuwa najiuliza hili swali: Baada ya kuona Takukuru ikiingilia rushwa katika mchakato wa kura za maoni za ugombea wa CCM, na ‘kufanikiwa’ kuwanasa watoa rushwa kadha makada wa CCM na wengine hata kupelekwa mahakamani.

  Jee Takukuru wanaweza kufanya hivyo hivyo tena dhidi ya rushwa ambayo ni hakika itatembea wakati wa uchaguzi mkuu October 31? Wana ubavu kuwakamata wagombea wa CCM watakaokuwa wanagawa rushwa kwa wapiga kura na kuwapeleka mahakamani na hivyo kuwaharabia ushindi jimboni na mwishowe jimbo kuchuliwa na upinzani? Takukuru wanaweza kweli kuifanya kazi hii? Kazi ambayo inaweza kuwapunguzia CCM ushindi wao “wa kishindo?”

  Au hizi harakati zao za hivi karibuni ni danganya toto tu?
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Jibu ni wazi kabisa -- Takukuru haiwezi kuchunguza kwa makini rushwa zitakazotolewa na wagombea wa CCM wakati wa uchaguzi mkuu. Ikifanya hivyo itakiumiza chama tawala - CCM. Inaweza kujifanya ti kufanya hivyo bila ya kuwa na dhamira ya matokeo hasi. Lakini Taasisi hiyo inaweza kuwabana wagombea wa upinzani ingawa inavyoeleweka wengi wao watakuwa hawana hata hela ya kampeni ya halali, achilia mbali hela ya kuhonga wapiga kura.
   
Loading...