TAKUKURU wana mpango gani na Tanzania yetu?

bojuka

Senior Member
Sep 9, 2010
128
1
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa chenge hausiki na kashfa ya ununuzi wa radar. Kwanini wanataka kutuona kuwa watanzania ni wavivu wa kufikiri , kama waliouza wamesema kuwa chenge alihusika takukuru wanakataa kwa maslahi ya nani?

Au walipewa mgao ?
Au wanampigia ndogo ndogo za uspika ili waendelee kuinyonya tanzania?
Au ndio sera za ccm?
 
Hivi hamjui kuwa hata huyo bosi wa TAKUKURU alipigiwa debe na EL ili ateuliwe kwenye huo wadhifa? Huu ni mtandao wa kimafia. Chenge na RA na wengineo wana mtandao ambao wanafikiri wanaweza kufanya wanachokitaka kwa pesa waliyoivuna kwa walalahoi
 
we subiri utaona tu! Mh Chenge nadhani ndiye anayeandaliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri la Tanzania. unapoona mambo ya kusafishana yanakuja kwa kipindi hiki ujue tayari!!! Usiulize kisu kwenye bucha
 
ni muda muafaka kujua kuwa PCCB siyo ya kupambana na ufisadi bali chombo cha CCM na mafisadi kujilinda. Watanzania mlipigwa changa la macho mkidhani kuwa PCCB ni chombo chenu. Wanaokimiliki chombo hiki hawazidi kumi.
1. Kikwete
2. Rostam
3.Chenge
4. Lowasa
5. Jitu
6. Manji
7.
8.
9.
10.
 
Mh. REMA,
Mbunge wa Arusha mjini, TAKUKURU wamejidhihirisha ukibaraka wao kwa CCM baada ya kuwakamata wana ccm pala kwa ngulelo na kuwaachia eti wanafanya kampeni ya nyumba kwa nyumba.Usikuu saa 2.30. Wana Arusha wakaandamana kupinga udhalimu wa TAKUKURU. Sasa umepewa rungu fanya kazi mjengoni. TAKUKURU hawawezi kura kodi zetu kwa kulinda maovu kinyume na majukumu yao.
 
Back
Top Bottom