TAKUKURU Waita watu kwa usaili wa ana kwa ana

mkongwensibi

Senior Member
Feb 1, 2022
133
215
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) anapenda kuutangazia umma kwamba usaili wa ana kwa ana (Oral Interview) kwa walioomba nafasi za kazi TAKUKURU utafanyika Jijini Dodoma kuanzia tarehe 1 Machi, 2022.

Mambo Muhimu ya Kuzingatia
1. Tarehe ya usaili ni kuanzia tarehe 1 Machi, 2022;
2. Usaili utakuwa unaanza saa 2:00 asubuhi kila siku;
3. Kila mtu aliyeitwa kwenye usaili anatakiwa kufika kwenye usaili kwa siku na muda aliopangiwa akiwa na nyaraka zifuatazo:-
3.1 Nakala halisi za vyeti vya masomo (Taaluma na kozi​
mbalimbali)​
3.2 Picha tatu β€œPassport Size”​
3.3 Nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa​
3.4 Anwani, namba ya simu na picha za wadhamini wawili​
4. Kuwasilisha nyaraka za kugushi ni kosa la jinai
5. Kila mtu atakayefika kwenye usaili huu anapaswa kujigharamia
6. Kila mtu aliyeitwa kwenye usaili huu anapaswa kuhakikisha anachukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 muda wote anaposafiri na anapokuwa kwenye chumba cha usaili;
7. Majina ya watu wote walioitwa kwenye usaili pamoja na eneo la kufanyia usaili yanapatikana kwenye wavuti ya TAKUKURU www.pccb.go.tz;
 

Attachments

  • TANGAZO LA USAILI - ORAL.pdf
    80.9 KB · Views: 95
  • AJIRA 2022 - WACHUNGUZI WASAIDIZI.pdf
    648.6 KB · Views: 97
  • AJIRA 2022 - MAAFISA UCHUNGUZI.pdf
    543.1 KB · Views: 97
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€kwahyo miezi miwili na bado majina yametoka mawili mawiliπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€Tz nchi yangu.
 
Tusubiri second selection tutatoboa tu πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜†πŸ˜†ndugu zangu pisisibi mtuonee huruma ata km mna ndugu zenu Yan ndo mtuchinje kibabe namna hiyo kwa PDF ya mchongo namna hiyo!?

Sasa namba tuliandika ili mjue tunajua kuandika namba au!?aaah pisisibi mmetuangusha watt wa wakulima tuliopewa nauli na wazee wetu kwa kujibana Sana wakiamini ktk sis kuwa mambo yatakuwa vzr....ila mbarikiwe Sana.Dunia haina haki.

Tuendeleee kupambana bila kuchoka,tumebeba matumaini makubwa ya familia zetu tukikata tamaa tutawaumiza wengi.
 
Tusubiri second selection tutatoboa tu πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜†πŸ˜†ndugu zangu pisisibi mtuonee huruma ata km mna ndugu zenu Yan ndo mtuchinje kibabe namna hiyo kwa PDF ya mchongo namna hiyo!..
Mkuu una maneno mengi sana, sidhani kama ungepata nafasi ya oral ungerudi kuja kutuongelea sisi watoto wa wakulima wenzio.

Alafu comments zako nyingi unajaza hizo 'image', zina faida gani kwenye kuwasilisha ujumbe wako?

Jifunze kukubali matokeo.
 
Mkuu una maneno mengi sana, sidhani kama ungepata nafasi ya oral ungerudi kuja kutuongelea sisi watoto wa wakulima wenzio.

Alafu comments zako nyingi unajaza hizo 'image', zina faida gani kwenye kuwasilisha ujumbe wako?

Jifunze kukubali matokeo.
Image zipi mkuu!?Amna Kaka sio kwamba sijakubali ila ni vile tu,haki inavyopindishwa,ndo maana naongea ila matokeo nimeyakubali...kwasababu ndo ishakuwa hivyo.
 
Back
Top Bottom