TAKUKURU wachunguze mkataba tata kati ya Mahindra Tech na TANESCO. Huenda kuna harufu kubwa ya ufisadi

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
2,480
2,000
Kwa taifa masikini kama Tanzania ambalo raia wake maskini wanakamuliwa kodi na tozo za kila aina kuingia mkataba wa bil 60+ ili kukodi software ya gharama ya bil 60+ ili hali wanafunzi hawana madarasa, maji ya uhakika, umeme na hata makazi mazuri ni kukosa busara.

Hivi kweli Tanesco wanahitaji software kama hii kwa wakati huu? Ok kama wanauhitaji ndio kusema hakuna watanzania waliosoma Computer science?

Je, ndio gharama kubwa namna hii.

Kukodi Software kama kwa gharama kubwa ni dalili kubwa kuwa kuna ufisadi mkubwa. Maana bil 60+ kwa taifa letu masikini ni pesa nyingi ambazo zingetumika.

Kuhusu mkataba, soma: TANESCO yaingia mkataba wa kukodi software kutoka India kwa USD 30M
 
CARDLESS

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
3,531
2,000
Wewe umejuaje kuwa mkataba ni wa KIPIGAJI? BASI UPEWE WEWE HIYO MIKATABA UISAINI KWA NIABA YA NCHI. Maana unataka kujionesha una akili kuliko watu wote, kuliko serikali, kuliko bunge na kila kilichomo.

Kwa ufupi wewe ni Matrako
 
Michael N

New Member
Nov 23, 2021
3
45
Kuna shida mahali otherwise wabongo wapewe hiyo kandarasi. Bilioni 69 ni nyingi sana, kwani hiyo software ndo itakuwa suluhu ya umeme kukatika kabisa?
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
10,111
2,000
Chief: haya mambo ya kitalaam kabla ya kuandika ni vyema kwanza ukafanya uchunguzi na kujiridhisha. Siwatetei wahusika lakini concern yangu ipo hapa, binafsi nafahamu zipo software duniani zinauzwa duniani kwa gharama kubwa kwa ajili ya kuendesha na kucontrol mifumo tofauti tofauti.

Tanesco kama shirika kubwa lenye mitambo miiingi inayohitaji maintenance na spareparts na controlling kwa ujumla ili iwe na ufanisi unahitaji mifumo ya kisasa uweze kufanya controlling ya mitambo na spareparts na watu wako ili upate performance nzuri. Hivi vitu vinahitaji utalaam wa hali ya juu na watalaam wabobezi sio blah blah.
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
10,111
2,000
Kuna shida mahali otherwise wabongo wapewe hiyo kandarasi. Bilioni 69 ni nyingi sana, kwani hiyo software ndo itakuwa suluhu ya umeme kukatika kabisa?

Unafahamu kama usimamizi butu wa mitambo unaweza kupelekea mitambo kuharibikaharibika? Unafahamu kushindwa kuwa na proper maintenance programs na spare parts invetory kunaweza kupelekea mitambo kusimama? Kuna vitu wabongo tuwe tunazama deep kidogo.
 
Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
2,480
2,000
Chief: haya mambo ya kitalaam kabla ya kuandika ni vyema kwanza ukafanya uchunguzi na kujiridhisha... siwatetei wahusika lakini concern yangu ipo hapa, binafsi nafahamu zipo software duniani zinauzwa duniani kwa gharama kubwa kwa ajili ya kuendesha na kucontrol mifumo tofauti tofauti......

Tanesco kama shirika kubwa lenye mitambo miiingi inayohitaji maintenance na spareparts na controlling kwa ujumla ili iwe na ufanisi... unahitaji mifumo ya kisasa uweze kufanya controlling ya mitambo na spareparts na watu wako ili upate performance nzuri...Hivi vitu vinahitaji utalaam wa hali ya juu na watalaam wabobezi sio blah blah..
Mkuu unafahamu maana ya software? Na unajua hii software waliokodi Tanesco ipo vipi?
 
mtolewa

JF-Expert Member
Jan 18, 2011
635
500
Tulikuwa tukiwaambia uhuru wa watu demokrasia ni Kila kitu mlikuwa mnatuona mazuzu na jiwe wenu aliyekuwa anawadanganya kuwa upinzani unachelewesha maendeleo. Kungemuwepo na uhuru na demokrasia mkataba huu hata Kama ungeisainiwa,ungevunjwa kwa nguvu ya umma hata kupitia maandamano tu. Tuwekeze katika mifumo siyo watu na matukio.
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
18,888
2,000
Ku divert maji kunawashinda halafu wanajifanya wanaenda na technology

Nchi maskini ni shida sana maana ni wachache wanapika data na kuiba
Na ukidhibiti sana unaenda na maji
 
mtumishiwaleo

JF-Expert Member
May 4, 2020
646
1,000
Huyu mama yupo pale kutuonesha jinsi ambavyo hii nchi bila mkono wa chuma haiendi. Kilichomcost mwenda zake ni kuwaacha mafisadi uraiani
Alijaribu kuwakamata mkaanza kusema anachuki na matajiri, maana kisa alisema anataka kuona waliokuwa wanyonyaji wa pesa za umma wakiishi kama Malaika nao waishi kama mashetani.Sasahivi Ndio mnaanza kuona umuhimi wa Magufuri
 
NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
978
1,000
Kwa taifa masikini kama Tanzania ambalo raia wake maskini wanakamuliwa kodi na tozo za kila aina kuingia mkataba wa bil 60+ ili kukodi software ya gharama ya bil 60+ ili hali wanafunzi hawana madarasa, maji ya uhakika, umeme na hata makazi mazuri ni kukosa busara.

Hivi kweli Tanesco wanahitaji software kama hii kwa wakati huu? Ok kama wanauhitaji ndio kusema hakuna watanzania waliosoma Computer science?

Je, ndio gharama kubwa namna hii.

Kukodi Software kama kwa gharama kubwa ni dalili kubwa kuwa kuna ufisadi mkubwa. Maana bil 60+ kwa taifa letu masikini ni pesa nyingi ambazo zingetumika.

Kuhusu mkataba, soma: TANESCO yaingia mkataba wa kukodi software kutoka India kwa USD 30M
Acha bhana eeeee! Uchunguzi wako kwani unasemaje?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom