TAKUKURU tupeni mrejesho wa kesi zote mlizokuwa mnashughulikia

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Kwanza kabisa mtambue kuwa mnatumia kodi za Watanzania kufanya shughuli zenu. Kwa hiyo kufanya maigizo yasiyo na kichwa wala miguu sio jambo jema.

Sakata la Mbowe kujilipa bil 8 liliwekwa wazi na wanachama waliokuwa wanakatwa hizo pesa na mpaka leo mliishia maigizo ya kuhoji wanachama bila kuchukua hatua.

Sakata la Sabaya mpaka sasa lipo hewani, hatujasikia akisomewa charge Mahakamani. Leo hii tunasikia eti Manji nae mnashikilia na kumhoji.

Huku mitaani mnakomaa na walimu, manesi, makarani ,mahakimu na mapolisi kuwapandisha vizimbani. Lakini vigogo wakubwa hatusikii wakipanda kizimbani.

Kwani kufanya kazi mpaka muwe na maigizo kuwa mnawahoji watu bila kuwa kuwapeleka mahakamani?
 
Kuhusu CHADEMA hapakuwa na kesi ndio maana wakawa wanalazimisha makosa kutafuta ushahidi kwa kila mtu mwishowe wakapotea, huyo Manji wako lazima ahojiwe kama alikwepa kodi awamu zilizopita alipe, kuhusu Sabaya naamini ni suala la muda tu kabla hajafikishwa mahakamani, ushahidi dhidi yake upo wa kila aina.
 
Kuhusu Chadema hapakuwa na kesi ndio maana wakawa wanalazimisha makosa kutafuta ushahidi kwa kila mtu mwishowe wakapotea, huyo Manji wako lazima ahojiwe kama alikwepa kodi awamu zilizopita alipe, kuhusu Sabaya naamini ni suala la muda tu kabla hajafikishwa mahakamani, ushahidi dhidi yake upo wa kila aina.
Takukuru imekuwa TRA wao kudili na kodi za Manji? Ushahidi wa Mbowe kutafuna pesa upo wazi acha kutetea. Bil nane zilienda wapi?

Kama ushahidi wa Sabaya upo tayari mbona hajapanda kizimbani?
 
Kuhusu Chadema hapakuwa na kesi ndio maana wakawa wanalazimisha makosa kutafuta ushahidi kwa kila mtu mwishowe wakapotea, huyo Manji wako lazima ahojiwe kama alikwepa kodi awamu zilizopita alipe, kuhusu Sabaya naamini ni suala la muda tu kabla hajafikishwa mahakamani, ushahidi dhidi yake upo wa kila aina.
Mkuu utamuweza mtoa mada! Tangu mwendazake azime Kama mshumaa, Wabondei wanasema ( kaitamugima) mtoa mada hayuko sawa , Basi tu ila kiroho hayuko sawa
 
Uzuri wa Takukuru, wanatupaga Mwanzo wa story, lakini mwisho wa story wanatuachia tumalizie wenyewe tunavyotaka!
 
Back
Top Bottom