TAKUKURU Tunaomba msiwaonee haya viongozi wote waliopokea hongo ili chanjo ije Tanzania kama ilivyodaiwa na Askofu Gwajima

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Kwa madai ya askofu Gwajima ni kwamba kuna viongozi walipokea hongo ili chanjo ije, na akauliza walihongwa kiasi gani hicho mpaka kuwauza watanzania?

Askofu alidai pia viongozi hao wamechanjwa chanjo feki ili kuwahadaa wananchi.

Sasa basi kwakuwa Tayari Waziri kaelekeza TAKUKURU mumkamate na mumuhoji athibitishe hoja zake basi tunaomba askofu akileta list ya wale waliopokea hongo msiwaonee haya kuwakamata, awe waziri au kama alihusika kupokea hongo akamatwe na achukuliwe hatua.

Tunaimani na TAKUKURU lakini tunaomba mtwambie ni lini mtamkamata maana naona imefika jioni hatuna taarifa ya kukamatwa kwakwe.
 
Nao wamekula hongo.. Yaani maigizo ya Bongo movie yamehamia serikalini
 
HII TUNAITA WEKA TUWEKE, HIT AFTER HIT

KOPO LANGU LA POPCORN MPAKA LIMEISHA
 
Gwajima anamaanisha mwenyekiti wa chama chake amekula hongo? ili madai ya Gwajima yawe na uzito lazima yaambatane na ushahidi, sio ataje majina tu, hivyo hatakuwa na tofauti na Bashite.

Issue ya chanjo feki akiambiwa athibitishe sijui atafanyaje, hapa anaiweka serikali ya chama chake matatizoni isiaminiwe na wananchi sababu ya mdomo wake asiojua kuufunga.

Huyu mtu kama alidhani anaweza kuwa Askofu halafu afanye na siasa kwa wakati mmoja amekosea, atapasuka msamba siku sio nyingi zijazo.
 
Marufuku kumkamata mtu Kama upelelezi haujakamilika. Hivyo Gwajima atapaswa kuthibitisha pasipo shaka.Aliyeidhinisha chanjo Ni Rais hivyo Gwajima anataka kusema Rais kala Rushwa.Sidhani Kama Gwajiboy atabaki salama hapa
 
Back
Top Bottom