TAKUKURU Tanga mnaendeshaje kesi na mtumishi ambae bado ameshikilia ofisi? RAS achunguzwe

Standards Person

JF-Expert Member
Apr 22, 2021
673
855
Ninawasalimu wanajukwaa nimatumaini kumekucha salama na mnaendelea na majukumu.

Kuna wakati niliandika uzi kuelezea namna ambavyo aliyekua mkurugenzi Tanga jiji alishiriki kuwatuliza Takukuru wasimzonge dada mmoja hivi ambae alifanya ubadhirifu wa mchana kweupe na akawa haogopi.

Tena ili kuonesha kwamba takukuru wamesinzia dada huyo akazidi kupandishwa cheo wakati wao wanamchunguza.

Mpaka kufikia sasa DPP amempeleka mtumishi huyo mahakamani kwa kesi ya uhujumu uchumi lakini bado mtumishi huyo ameshikilia madaraka eti ni afisa elimu kata.

TAKUKURU acheni kuwafanya watu wazidi kukosa imani na nyie.

Kama sio mpango wenu wa muda mrefu na hao viongozi,ingilieni kati mumhoji RAS kwa aibu hii
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom