TAKUKURU Songwe yamrejeshea mkopaji nyumba ya TSh165 milioni

Kwa hiyo mkopeshaji analipwaje chake?.

kisheria apaswi kulipwa kwa sababu kwanza hapo kafanya makosa mengi.

Moja ni kufanya biashara ya kukopesha kinyume na sheria kwa kukosa leseni benki kuu.

Ukwepaji wa kodi, kwa kuwa biashara iyo haitambuliki, maana hayo mapato haramu hayatotozwa kodi.

Kwa kupokea na kutumia hayo mapato ya riba kinyume na sheria, inaweza kutafsiriwa kama utakatishaji wa fedha.

Kwa iyo kurudisha tu iyo dhamana (nyumba ) iliyokwa rehani wamemsaidia tu mkopaji maana anastahili adhabu nyingi.

Ikitokea mtu anashida alafu akakuambia umkopeshe pesa na atakurudishia zaidi ya iyo kwa kuda mfupi ama mrefu kwa kukupa dhamana yoyote usikubali kwa maana akilalamika kwenye vyombo husika utakosa yote pamoja na kuingia matatani.
 
Toka aanze kukusanya hazijatimia tu? Unaweza kuta mkataba una muhuri wa mahakama ya mkoa
watu wenye hela wanatunyanyasa sisi ambao hatunazo. nimeona leo eti zoezi la uvunaji viungo vya binadamu linataka kuanza pia hapa bongo wapo hatua ya kutengeneza mswada ili uwe sheria, nikawazaaaaaaaaa🤔🤔🤔, hivi si watatumaliza sisi masikini jamani! tajiri anaumwa moyo masikini amelazwa kwa shida ya vidonda vya tumbo hivi watamwacha? mbona naona rushwa itakuwa nje nje wa madaktari jamani, pia naona vile visa vya watu kupotea vitakuwa vingi mnoooo.
NIMEENDA MBALI SANA NA MAADA ILA NI KWASABABU YA KITU HELA😁
 
Unyang'anyi tu huo....
11M rejesho 33M...kiukweli mbinguni mbali!
Kisha kashachukua kodi at least miezi 100 ya 3M kila mwezi tokea amnyang'anye! Jumla yote alichopata ni 300M+, daah!
Ni zaidi ya unyang'anyi! Hapo utakuta na mawakili wasomi walihusika pia!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Hahaaa... Dunia tambala bovu
 
Hii mikopo umiza huwa inamsaidia Sana, kikubwa mkopaji uwe na uhakika mujarabu,. Tatizo hizi taasisi za mikopo pasua kichwa Sana.... Unaambiwa upeleke mpaka picha za watoto....
 
kisheria apaswi kulipwa kwa sababu kwanza hapo kafanya makosa mengi.

Moja ni kufanya biashara ya kukopesha kinyume na sheria kwa kukosa leseni benki kuu.

Ukwepaji wa kodi, kwa kuwa biashara iyo haitambuliki, maana hayo mapato haramu hayatotozwa kodi.

Kwa kupokea na kutumia hayo mapato ya riba kinyume na sheria, inaweza kutafsiriwa kama utakatishaji wa fedha.

Kwa iyo kurudisha tu iyo dhamana (nyumba ) iliyokwa rehani wamemsaidia tu mkopaji maana anastahili adhabu nyingi.

Ikitokea mtu anashida alafu akakuambia umkopeshe pesa na atakurudishia zaidi ya iyo kwa kuda mfupi ama mrefu kwa kukupa dhamana yoyote usikubali kwa maana akilalamika kwenye vyombo husika utakosa yote pamoja na kuingia matatani.
Umenyambua vizuri sana

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
11M rejesho 33M...kiukweli mbinguni mbali!
Kisha kashachukua kodi at least miezi 100 ya 3M kila mwezi tokea amnyang'anye! Jumla yote alichopata ni 300M+, daah!
Ni zaidi ya unyang'anyi! Hapo utakuta na mawakili wasomi walihusika pia!

Everyday is Saturday............................... :cool:
Kabisa, hawa wakopeshaji wa mikopo umiza wanamsaidia Sana na mawakili, mahakimi na Saa zingine mapolisi

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Songwe imeokoa nyumba yenye thamani ya Sh165milioni iliyochukuliwa baada ya mmiliki kushindwa kurejesha mkopo wa Sh15milioni mali ya Jacob Masebo (62).

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Songwe, Damas Suta amesema, Masebo alikopa Sh15milioni miaka 11 iliyopita kutoka kwa Richard Kalonge, ambapo alipaswa kurejesha TSh33 milioni baada ya siku 18 ambazo hata hivyo mkopaji alishindwa kurejesha hali iliyosababisha mkopeshaji kunyang'anya nyumba ambayo iliwekwa kama dhamana.

Suta amesema Kalonge alipoichukua nyumba hiyo yenye ghala kubwa moja, maghala madogo mawili na vyumba vitatu vya maduka, aliibadilisha jina na kutengeneza hatimiliki ya kudumu kwa jina lake, jambo alilosema ni uonevu kupitia mikopo umiza.

"Tulipomhoji Kalonge alisema nyumba hiyo imekuwa ikimwingizia Sh3 milioni kila mwaka zinazotokana na kupangisha," amesema Suta.

Naye Mkuu wa wilaya Mbozi, John Palingo amewasihi wananchi kuwa makini wanapofanya makubaliano yoyote kwa kuelewa vizuri mkataba ulivyo ili waepuke kuingia mikataba yenye makubaliano yenye utata.

Kwa upande wake Jacob Masebo amesema alilazimika kuchukua mkopo huo baada ya kukosa mkopo alioomba benki na kwamba alitaka fedha hizo ili akamilishe ujenzi wa jengo hilo.

"Sielewi kilichotokea, niliomba mkopo benki walituma wataalamu wa uthaminishaji lakini baada ya muda mrefu waliniambia mkopo umeshindikana," amesema Masebo.

Mwananchi
Hatima ya mdai vipi? Maana yupo kwenye makubaliano bado alipwe chake, na mtu uanwezaje kukopa pesa ya milioni 15 ukaweka dhamana nyumba ya milion 165 hizi ni akili ama
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Songwe imeokoa nyumba yenye thamani ya Sh165milioni iliyochukuliwa baada ya mmiliki kushindwa kurejesha mkopo wa Sh15milioni mali ya Jacob Masebo (62).

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Songwe, Damas Suta amesema, Masebo alikopa Sh15milioni miaka 11 iliyopita kutoka kwa Richard Kalonge, ambapo alipaswa kurejesha TSh33 milioni baada ya siku 18 ambazo hata hivyo mkopaji alishindwa kurejesha hali iliyosababisha mkopeshaji kunyang'anya nyumba ambayo iliwekwa kama dhamana.

Suta amesema Kalonge alipoichukua nyumba hiyo yenye ghala kubwa moja, maghala madogo mawili na vyumba vitatu vya maduka, aliibadilisha jina na kutengeneza hatimiliki ya kudumu kwa jina lake, jambo alilosema ni uonevu kupitia mikopo umiza.

"Tulipomhoji Kalonge alisema nyumba hiyo imekuwa ikimwingizia Sh3 milioni kila mwaka zinazotokana na kupangisha," amesema Suta.

Naye Mkuu wa wilaya Mbozi, John Palingo amewasihi wananchi kuwa makini wanapofanya makubaliano yoyote kwa kuelewa vizuri mkataba ulivyo ili waepuke kuingia mikataba yenye makubaliano yenye utata.

Kwa upande wake Jacob Masebo amesema alilazimika kuchukua mkopo huo baada ya kukosa mkopo alioomba benki na kwamba alitaka fedha hizo ili akamilishe ujenzi wa jengo hilo.

"Sielewi kilichotokea, niliomba mkopo benki walituma wataalamu wa uthaminishaji lakini baada ya muda mrefu waliniambia mkopo umeshindikana," amesema Masebo.

Mwananchi
Kisheria hapa mdai akienda mahakamani ana hoja za kumlinda maana si waliingia mikataba ya ukopeshaji
 
Kama mkataba ulikua na stemp ya TRA hapo mkopwaji alikua na haki kutelekeza agizo lake, muwe mnapelekea mikataba yenu TRA kwa kuwalinda maana mambo ya kukopeshana mitaani ni ishu
 
Back
Top Bottom