TAKUKURU Songwe yamrejeshea mkopaji nyumba ya TSh165 milioni

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
10,730
2,000
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Songwe imeokoa nyumba yenye thamani ya Sh165milioni iliyochukuliwa baada ya mmiliki kushindwa kurejesha mkopo wa Sh15milioni mali ya Jacob Masebo (62).

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Songwe, Damas Suta amesema, Masebo alikopa Sh15milioni miaka 11 iliyopita kutoka kwa Richard Kalonge, ambapo alipaswa kurejesha TSh33 milioni baada ya siku 18 ambazo hata hivyo mkopaji alishindwa kurejesha hali iliyosababisha mkopeshaji kunyang'anya nyumba ambayo iliwekwa kama dhamana.

Suta amesema Kalonge alipoichukua nyumba hiyo yenye ghala kubwa moja, maghala madogo mawili na vyumba vitatu vya maduka, aliibadilisha jina na kutengeneza hatimiliki ya kudumu kwa jina lake, jambo alilosema ni uonevu kupitia mikopo umiza.

"Tulipomhoji Kalonge alisema nyumba hiyo imekuwa ikimwingizia Sh3 milioni kila mwaka zinazotokana na kupangisha," amesema Suta.

Naye Mkuu wa wilaya Mbozi, John Palingo amewasihi wananchi kuwa makini wanapofanya makubaliano yoyote kwa kuelewa vizuri mkataba ulivyo ili waepuke kuingia mikataba yenye makubaliano yenye utata.

Kwa upande wake Jacob Masebo amesema alilazimika kuchukua mkopo huo baada ya kukosa mkopo alioomba benki na kwamba alitaka fedha hizo ili akamilishe ujenzi wa jengo hilo.

"Sielewi kilichotokea, niliomba mkopo benki walituma wataalamu wa uthaminishaji lakini baada ya muda mrefu waliniambia mkopo umeshindikana," amesema Masebo.

NYUMBA.JPG

Mwananchi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom