TAKUKURU, Polisi waja na muarobaini wa rushwa za barabarani wakishirikiana na wadau

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,878
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) leo imefanya maongezi ya kimkakati na Wadau mbalimbali wakiwemo Sekta Binafsi, Sekta za Umma, Asasi za Kiraia, Taasisi za Dini, Vyombo vya Habari, Viwanda vya Uchapaji na Uchapishaji, Kampuni za Simu, Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri, Wasanii, Madereva wa Vyombo vya Moto na Wananchi kuelezea Kampeni inayotarajiwa kuzinduliwa ya kupunguza ama kutokomeza kabisa rushwa Barabarani.

PCCB_Utatu.JPG

TAKUKURU imeeleza kuwa Kampeni hiyo imepewa jina la ‘UTATU’ ikimaanisha ni muunganiko wa pande Kuu tatu: TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Wadau

Imedaiwa kuwa lengo kuu la kampeni ni kuzuia rushwa za barabarani ambayo imebainika ni kisababishi kimojawapo cha ajali zinazotokea barabarani; tatizo ambalo limekuwa likikemewa sana na viongozi mbalimbali wa Serikali. Aidha imesema UTATU huo unatakiwa kuweka mikakati ya pamoja na endelevu ya kutibu tatizo la ajali badala ya kulaumiana na kunyoosheana vidole.

Kampeni hiyo imejiwekea mambo malengo mahususi manne, ikiwa kila lengo linatakiwa kutekelezwa na kila mdau kwa nafasi yake:
  • Kudhibiti vitendo vya rushwa miongoni mwa wasimamizi wa sheria za barabarani
  • Kuandaa mkakati wa kuzuia vitendo vya rushwa barabarani
  • Kushirikisha Umma kuzuia vitendo vya rushwa barabarani
  • Matumizi ya TEHAMA kudhibiti vitendo vya rushwa barabarani
Kuhusu matumizi ya TEHAMA kudhibiti vitendo vya rushwa barabarani, TAKUKURU imesema tayari limeanza kutekelezwa kwa kutengeneza mfumo utakaotumika kuchukua matukio ya vitendo vya rushwa kwa kutumia simu ya mkononi (Mobile App).

Mfumo huo (Mobile App) utakaozinduliwa pamoja na Kampeni hii ya UTATU, utapakuliwa kutoka Play Store au App Store ya simu ya mkononi kisha mtu ataweza kupiga picha za video, mnato au sauti na kuzituma TAKUKURU.

Baadhi ya Majukumu ya Wadau wa Kampeni hii yametajwa kuwa:

Wasimamizi wa sheria na miundombinu ya Barabara (TANROADS, TARURA, LATRA na wengine)
Wanalo jukumu la kusimamia ubora wa miundombinu na Vyombo vya Usafiri ikiwa ni pamoja na
  • Kuboresha sheria, kanuni na miongozo
  • Kuboresha miundombinu ya barabara na mizani
  • Kusimamia usajili wa Vyombo vya Usafiri
  • Kuhakikisha alama za usalama barabrani zinaonekana vizuri
  • Kutoa taarifa za vitendo vya rushwa barabarani
Wasanii wa fani mbalimbali
  • Wana jukumu la kuhamsisha watumiaji wa barabara kupitia Sanaa zao zinazosisimua na kuburudisha huku ujumbe wao ukisaidia kubadili mitazamo ya watumiaji wa barabara kuacha vitendo vya rushwa
  • Wanatarajiwa kutoa michango yao ya kuandaa Sanaa zitakazohusiana na kampeni ya UTATU
PCCB_Wasanii.JPG

AZAKI wao wametajwa kuwa wahamasishaji ambapo majukumu yao yatakuwa:
  • Kuhamasisha wananchi kutuma taarifa za vitendo vya rushwa barabarani
  • Kuhamasisha wananchi waache uoga wa kutoa taarifa za rushwa
  • Kutumia mtandao wao kutoa taarifa za vitendo vya rushwa
  • Kuhamasisha wananchi kuacha kutoa rushwa kwa masimamizi wa sheria za usalama barabarani
Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri ambao majukumu yao ni
  • Kusimamia Vyombo vya Usafiri ili kutoruhusu magari mabovu kuingia barabarani
  • Kuajiri madereva wenye sifa na kuwalipa vizuri
  • Kuacha kutoa Rushwa ili wapate leseni bila kufuata utaratibu
  • Kuwachukulia hatua madereva wazembe
  • Kuwasimamia madereva kuacha kutoa rushwa kwa wasimamizi wa sheria za usalama barabarani
Wamiliki wa Vyombo vya Habari ni kundi lingine ambalo katika Kampeni hii majukumu yake yamebainishwa kuwa
  • Kuelimisha wananchi kupitia Vyombo vyao vya Habari
  • Kusaidia kutoa nafasi kwenye Vyombo vya Habari na kurusha matangazo kuhamasisha kampeni
  • Kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa
PCCB_Media.JPG

Wamiliki wa Viwanda vya Uchapishaji na Uchapaji wao wataweza kushiriki kwa:
  • Kusaidia kuchapa machapisho ya kuhamasisha kampeni
  • Kutoa taarifa za vitendo vya rushwa
Vingozi wa dini wao wana majukumu muhimu ya
  • Kufundisha maadili kwa waumini wao ili wasitoe rushwa kwa wasimamizi wa sheria za usalama barabarani
  • Kutumia Vyombo vya Habari vinavyomilikiwa na dini zao ili kuhamasisha kampeni
  • Kutoa taarifa za vitendo vya rushwa
PCCB_Dini.JPG

Katika mkutano huu, wadau walioshiriki kutoa maoni wamedokeza haya:-

Kwanza, wamesema Rushwa ni mtazamo wa ndani ya Polisi na nje ya Polisi, watu wanaona Polisi ni fursa. Kwenye vitengo vinavyoongoza kwa rushwa ni pamoja na kwenye kutoa leseni, ukaguzi wa barabarani. Polisi walio kwenye Pikipiki maarufu kama ‘tiGO’ na madereva wa magari ya Kirikuu wanaodai kuwa wakipita ni lazima wasimamishwe na kuombwa rushwa

Aidha, wengine wamehoji kwanini TAKUKURU hawapo barabarani? Huku wengine wakisema ni bora adhabu ziongezwe kwenye makosa ya barabarani na adhabu ya fedha iondolewe kabisa.

Wengine wakiwemo Viongozi wa Dini wametoa maoni kuwa hofu ya Mungu ndio suluhisho pekee la tatizo la rushwa kwa wananchi wanaweza kuwaepuka TAKUKURU na Polisi ili wasikamatwe kwenye masuala ya rushwa. Pia, Polisi wakiwa na hofu ya Mungu wanaweza kukataa rushwa na kuwakamata wanaotaka kutoa na hivyo kuzuia rushwa.

Lakini, kuhusu App TAKUKURU waliyozungumzia wadau wamesihi sana kuwa kunatakiwa kuwe na elimu ya awali itakayotolewa kwa Wananchi kabla ya kuanza kutumia App hiyo na pia kuwapa muda Wananchi kuielewa.

Wametaka pia Makamanda wa Polisi na watumishi waboreshewe maslahi kwa kuwa hiyo inaweza kuwa njia mojawapo ya kuzuia rushwa.
 
Iringa rushwa imetamalaki, gari zinaanza kisimamisha kuanzia stendI na polis hawajali. Bora basi hata wawe watano lakini utakuta gari imejaza mpaka mnabanana hasa daladala za Iringa Mjini polisi wanazagaa tu.

Juzi nimeenda kwa majukumU yangu kuna stendi mpya sasa hivi ni balaa. Gari imejaa lakini haiondoki stendi mpaka ijaze wa kusimamisha na polisi wanaangalia tu mpaka nilishangaa.
 
Sijaelewa TAKUKURU watakuwa makonda kwa muda au wata play part ya abiria na dereva

Hapa sidhani kabisa kama kuna utatuzi.

Mgeni akija nyumbani hata ukifanya kosa huchapwi,subiri aage unaweza ukatamani muondoke wote.

Hawa TAKUKURU wanataka kutupalia makaa halafu wasepe watuache barabarani tunapambana na matrafiki

Ingekuwa zoezi hili endelevu na uhakika upo sawa ila kwa Tanzania yetu hii kila jambo linaanzishwa kwa nguvu ila mwisho haujulikani, sijui.
 
Kukomesha Traffic wawe wanakaa sehemu zenye CCTV camera ndipo wasimamishe magari na kukagua.Hili la kusimama popote linachangia Sana Rushwa.

Pia ziwekwe kamera automatic fixed sehemu.za spidi limit Askari traffic waondolewe wakafanye Kazi zingine badala ya hiyo ya kuvizia na kamera zao.

Maeneo ya mataa na zebra zifungwe kamera za CCTV traffic police waondolewe
 
Kuna vitu vingine hizi taasisi zina takiwa ziache kutufanya.. Hivi TAKUKURU hawajui jinsi polisi hasa trafiki wanavyopokea rushwa?

Kwa Arusha kila baada ya mita zisizozidi mia mbili kuna trafiki wanne au sita utadhani kuna uhalifu unazuiwa. Kila askari akija Arusha anataka kuwa trafiki.

Zaidi waangalie mali walizonazo trafiki ukilinganisha na mishahara yao.. Sio jambo la kutuambia wanaweka mikakati..
 
Dar es salaam ndio kabisa kuna over-employment ya traffic .Kuendesha gari ni kero na adhabu breki inatumika zaidi kwenye kuendesha gari kila hatua chache traffic Tena sio mmoja kibao.Ukikata kona traffic .Yaani kisatari kidogo tu unasimamishwa kila kona hadi inaudhi hata uwe na kila kitu.

Wanaanza kukagua upya. Huyu anakagua kasimama mbele ya mataa. Unatoka hapo kwenye mataa unakata kona au mbele tu unakutana na wengine wanaanza tena ukaguzi hapo saa nyingine unawahi hospitali.

Dar es salaam ni police traffic city. Huko Arusha ni cha mtoto fika Dar es salaam.

Safari ndefu barabara kuu hivyo hivyo .Matraffic kibao njia nzima hata porini wapo, sehemu ambazo hata watu hawaishi unakuta trafiki hao wanakupiga mkono. Arusha na Dar ni kero si uongo.Tena kero kubwa mno sio kidogo.

Unashangaa mikoa mingine unakuta traffic wachache sana na wanakaa sehemu moja tu ya mji na hawana usumbufu wa hovyo. Dar es salaam gari ikichubuka rangi kidogo tu unakomaliwa kila kitu unacho mchubuko.tu mdogo wa rangi wana wewe.

Hivi mlundikano wa matrafiki Dar es salaam Ni wa Nini?

Daladala ndio usiseme kutwa yeye ni.kama mradi wa traffic kila trip ni yeye na traffic route ni hiyo hiyo ana kila kitu lakini kusimamishwa na traffic kwenye hiyo route sehemu kibao. Ni kama kawa. Hadi unawahurumia. Hawezi kusimamishwa labda mara moja tu akakaguliwa akaachwa yaani yeye ni kupigwa mkono tu kutwa.

Nashauri TAKUKURU muwe mnapanda daladala muone kero za traffic kwenye daladala hasa za Dar es salaam.

Wanyonge na wanaohangaishwa namba moja na traffic Dar es salaam.ni daladala
 
Kuna mtindo umekuja polisi wanajificha porini na kutumia simu zao za smart phone kupiga Magari over speed, ukifika mbele unasimamishwa unaonyeshwa Picha ya gari lako na speed yako kwenye siku ya trafic mwingine, wanakudai rushwa na faini hawataki kukuandikia, mfano kuna eneo LA low gear, kule babsti mkoani kuelekea kateshi, pale polio ni kitovu cha kuombea na kukusanyia rushwa, tunaomba takukuru Mkoa wawe pale kusaidia wananchi.

RTO na RPC wapi pale wanajifanya hawaone wananchi wanavyonyanyaswa ,imefika mahali au wakati penye traffic point awepo MTU mmoja Wa takukuru,hali sio mzuri haya kidogo.pili kwanini serikali isiweke camera barabarani ili Picha ikipigwa isome na kupeleka Picha moja Kwa moja ofisi za polisi Mkoa na wilaya badala ya sasa Picha kuwepo kwenye siku za watu binafsi na kutoza faini au rushwa?

Je RPC anajua ni Picha ngapi zimepigwa Kwa siku au anasubiri tu kuambiwa kilichotokea? Ushauri wangu ziwekwe camera za kudumu barabarani kama Nairobi zitasaidia kupunguza rushwa ya speed na haya wizi Wa Magari.pili vituo vya polisi USA river,pia ni shida askari wawe wanahamishwa Mara Kwa mara
 
Hakuna haja ya CCTV. Wakamate tu hao maskari wanaopokea rushwa. Wao wenyewe watabadilika. Kuna siku nasimamishwa pale Kariakoo wako tayari kupokea au wanaita wenyewe kuwezeshwa.
 
Awamu ya tano rushwa imepungua sana. Ukipatikana na kosa basi Maaskari wanafuata sheria.
 
Tutaachaje kutoa rushwa? Rushwa tunatoa kwa sababu ya utatu huo huo.

Mosi: Serikali (faini 30,000), dereva hana uwezo wa kutoa faini ya 30,000 na askari yuko tayari kupokea rushwa ya 5,000-10,000. Binafsi nitatoa rushwa kuliko kulipa faini ambayo kiuhalisia hiyo fedha sina. Wakifanya faini 10,000 nitailipa.

Pili: li tuache kutoa rushwa, ni lazima serikali ipambane kuhakikisha kuwa polisi wanaacha kubambika makosa kwa waendesha vyombo vya barabarani. Trafiki anaanza, leseni (hiyo), triangle (hiyo), sticker ya usalama (hiyo), breki (zipo), siti (haina mchubuko), kwanini umepakia mzigo umepita urefu wa bodi? Unatakiwa ulipe faini (30,000).

Au tairi zinaelekea kuisha (faini), gari rangi imebabuka (faini), kioo kimegongwa na changarawe na kuonyesha kanyota bila kupasuka (faini), pale nyuma uliovertake pasiporuhusiwa (wakati gari uliovertake ilipaki pembeni).

Hii inakuwa karaha sana kwa kuwa huwezi kuwa mtakatifu kwa haya watakayo askari wetu wenye njaa kali. Mwisho wa siku ni kuishia kutoa rishwa ili japo ubakize hela ya sembe kwa ajili ya watoto. Ningekuwa naweze nisingepita barabarani kabisa kuepukana na polisi hawa wenye kero za kutosha.
 
Huku kote ni ku complicate mambo, njia rahisi ilikuwa kuweka vituo maalumu vya ukaguzi wa magari na viwe na cctv camera zinazotuma taarifa moja kwa moja. Habari ya app si rafiki kwa kila mdau kwasababu tayari askari watajua kuwa wanarekodiwa
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom