Elections 2010 Takukuru ni nn?

Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
682
323
Hii ni taasisi ambayo nathubutu kusema inaiangusha serikali machoni pa watawaliwa na inawalinda vigogo ambao enzi za mwalimu tengewaita wahujumu uchumi machoni pa sheria za nchi. Ili waponde nchi kwa raha zao.
Ni Taasisi hii hii iliyosema richmond haikuwa na matatizo kabisa katika ule mkataba tena chini ya Mkurugenzi huyu huyu, Leo bila soni inasema Chenge ni safi huku ikijua sio safi hata kiduchu.
Dah huyu jamaa Hosea sijui ana hisa gani na mkuu wa kaya!!! kama watahujumu sheria na kuiiba siku zote then the history will mark them.
 
Tatizo mkuu ni ukosefu wa utawala bora na kutoheshimu katiba! Wanasema nyumba ya kambale kila mmoja ana ndevu!
 
Hujasema sasa unataka nini TAKUKURU ndio PCCB kizungu, zote ulizosema
ni simulizi machoni mwa watanzania. sasa lete hoja hapa nimeipenda hii thread!
 
Hii ni tasisi iliyoundwa kuchakachua ufisadi unafanywa na vigogo ili uonekane ni Takrima za kawaida. Ni taasisi itakayo kumbukwa ktk historia za nchi hii kuwa iliwalinda wahalifu na kuwaonea wanyonge na wale wanao onekana kuwa wana mtazamo tofauti na Manyang'au na makambale wa ufisadi.
 
TAKUKURU ni moja ya nyenzo tano zinazotumiwa na serikali ya CCM kuhakikisha kuwa mafisadi wanaendelea kushika hatamu. Nyenzo nyingine ni NEC, polisi, JWTZ na usalama wa taifa (la mafisadi:bowl:)
 
Hii ni taasisi ambayo nathubutu kusema inaiangusha serikali machoni pa watawaliwa na inawalinda vigogo ambao enzi za mwalimu tengewaita wahujumu uchumi machoni pa sheria za nchi. Ili waponde nchi kwa raha zao.
Ni Taasisi hii hii iliyosema richmond haikuwa na matatizo kabisa katika ule mkataba tena chini ya Mkurugenzi huyu huyu, Leo bila soni inasema Chenge ni safi huku ikijua sio safi hata kiduchu.
Dah huyu jamaa Hosea sijui ana hisa gani na mkuu wa kaya!!! kama watahujumu sheria na kuiiba siku zote then the history will mark them.

TAKUKURU-TAasisi ya KUkuza na KUendeleza RUshwa Tanzania
:A S angry:
 
kama kuna kitu ambacho kinapaswa kufanyiwa marekebisho/kuondolewa ni Taasisi hii. Wakati wa uchaguzi ndo haikusika kabisa, hata wakipewa taarifa kuwa kuna suala la rushwa mahali kama jambo linamhusu mtu wao hawaendi kama wanaenda ni baada ya tukio. Sioni kazi inayofanywa na taasisi hii. Ni afadhali kutokuwa na chombo kama hicho kuliko kuwa nacho lakini ikafanya kazi ya kueneza rushwa
 
Ninachosema hii taasisi ifutwe maana haina faida kwa wananchi zaidi ya kulamba kodi za waBongo huku ikiwafagilia wanapunguza mapato ya nchi na kupoteza mpenyo wa huduma za jamii. Haina maana ifutweeee
 
Takukuru ipo kwa ajili kukamata mahakimu wa mahakma za mwanzo na walimu wa shule za msingi kwa rushwa ya sh 5000.
 
Back
Top Bottom