TAKUKURU na Siku ya Maadili Kitaifa

M

MegaPyne

Guest
M

MegaPyne

Guest
[FONT=arial,sans-serif]Wakati Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) PCCB leo inaadhimisha siku ya Maadili kitaifa, suala la rushwa bado linaonekana kuwa kubwa, huku taasisi hiyo ikionesha kuchangia kuongezeka kwa tatizo hilo kutokana na mfumo mbovu wa uongozi wa Mkurugenzi Mkuu wake Bw. Edward Hosea.

[/FONT]
[FONT=arial,sans-serif]Bw. Hosea amekuwa kikwazo kikubwa kwa wasomi hao kutekeleza majukumu ya msingi ya kupambana, kuzuia, ili kutokomeza mdudu huyo mbaya wa rushwa nchini.

[/FONT]
Taarifa za ndani ya Taasisi hiyo zimesema kuwa Bw. Hosea amemtoa Kamanda wa Taasisi hiyo wa mkoa wa Shinyanga na Kumpeleka kusimamia Maktaba ya Idara ya Elimu kwa Uma, Sasa kweli RBC Region PCB Kamanda anakuwa mtunza mavitabu na mafaili, kwa kosa lipi kubwa? pia amekuwa akiwashutumu wakurugenzi wenzake kwa masuala mbalimbali ya kiutendaji kutokana na udhaifu wake.

Huyu Bw. Hosea amediriki hata kudai kuwa Rais KIKWETE ni Msela mwenzake na kwamba amemsaidia sana katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005, katika mchakato wa kumpata mgombea wa CCM Mjini Dodoma kwa kuunda safu ndani ya PCB ya wakati huo ili kuvuruga njama za wagombea wengine kuwashawishi wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM 2005, ili apite yeye.

"Poleni sana yote ambayo Wakurugenzi wangu mnayapeleka Ikulu mie nayajua, kila siku mnajihimu ikulu mkitegemea kuwa mtaweza kujaribu kuyarekebisha haya, hamuwezi hata kwa dawa, ukweli ni kwamba ukienda kwa Luwanjo (Katibu Mkuu Kiongozi) na yeye akimwambia Jakaya(Rais) Lazima jioni katika kijiwe chetu aniambie yote, na mara nyingine hata hunishauri nimpelekee mapendekezo ya kuwakandamiza ili awapige chini" ni sehemu ya sentensi ya Bw. Hosea aliyoitoa Marangu mbele ya maafisa mbalimbali wa Taasisi hiyo.

Akizungumza kwa uchungu mmoja wa Wakurugezni ambaye hajataka kutaja jina lake amesema "Kwa ujumla wanahabari kuna mengi yanatendeka ndani ya PCCB kiasi kwamba sasa hivi vijana wetu ambao ni wasomi wazuri huko mawilayani wajuta kwanini walijiunga na Taasisi hii, kwani pesa zote zinaishia kumnufaisha yeye ( Bw.Hosea) peke yake bila kutekeleza mambo muhimu ya kiutendaji.

Hivi sasa Bw. Hosea anajenga jumba la kifahari wilayani Maswa, huku akimiliki jingine kubwa nchini Marekani, hali ambayo inafanya kuwepo kwa kiini macho cha kiutendaji ndani ya Takukuru.

Amezuia maafisa wote wa PCCB kutoonekana wakifanya mazungumzo wala kusalimiana na KAMAZIMA(EX-Director General) wa PCCB kwa madai kuwa anampiga vita ili aikose nafasi hiyo ambayo tayari anayo.

Wanahabari na watendaji wa nchi hii, ili tunsaidie Rais Kikwete katika vita dhidi ya rushwa ni lazima tumshauri kwa hoja za kina, na tusifikie mahali tukadanganyika na suti za mtu, tukashindwa kueleza ukweli.

Nategemea wanahabari mtalifanyia kazi hili, kwani katika Journalism, kunautendaji kama katika upelelezi na Uchunguzi, ambao ili uufanye kwa kiwango cha kuwasaidia wengine lazima ufanya kitu wataalamu wanasema kutafuta taarifa kwa mfumo wa 5W and H.

Mfumo huu siye wapelelezi huwa tunautumia kwa minajili ya Nani wa kumchunguza Wapi pakumchunguza Lini anatakiwa achunguzwe, Kwanini achunguzwe, Namna gani achunguzwe, Matokeo ya kumchunguza.

Nawategemea sana katika hili mtasaidia kwa kiwango kikubwa kutukwamua na kidudu mtu hiki ili wakati U [FONT=arial,sans-serif]moja wa Mataifa unadhimisha siku ya Maadili Duniani Decemba 9 kila mwaka na Tanzania kuadhimisha leo Tarehe 10 , Haki itendeke bila kumwacha huyu jamaa akinenepesha tumbo lake.

[/FONT] [FONT=arial,sans-serif]Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili ni Kukataa kwako rushwa kuna thamani.

[/FONT] [FONT=arial,sans-serif]Naambatanisha maelezo yatakayowasaidia kutoka Jambo Forum ambayo yote hayo yanaukweli mtupu.

Source: Niulize hii baadaye!

[/FONT]
 
Mtu wa Pwani

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Messages
4,126
Likes
99
Points
145
Mtu wa Pwani

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2006
4,126 99 145

ww nnakuvulia kofia, habari za uchonganishi mbio unazileta hata ukiulizwa ushahidi ubaki kumangamanga mcho kama ulienyweshwa kungu.

hebu tuletee habari za kuleta umoja wa kitaifa kuwafanya watanzania wawe wabunifu zaidi, kuondosha umaskini na kuleta maendeleo.

ww kutwa huyu kafanya hivi yule kafanywa hivi unabowa mkuu
 
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2007
Messages
2,505
Likes
32
Points
135
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2007
2,505 32 135
udaku tuna wivu,hao watu wa PCCB walizoe kula pesa tu na hawafanyi kazi ya maana,wanapewa oc kwa mwaka mzima kuna kuwa na kesi 100 tu za rushwa huku bajeti yao kubwa..nachokijua Dr. Hoseah anataka kuibadili PCCB iwe ya kisasa na ya kisanyansi na sio mambo ya kurundika vihiyo..Nilimsikia akiteta Jumamosi katka harusi moja ambyo na mie nilikuwapo.Dr. hoseah andonekana mtu makini sana..watu wanaomlaumu Dr. Hoseah ni wale wanaoendekeza ukabila.
 
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2007
Messages
2,505
Likes
32
Points
135
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2007
2,505 32 135
[FONT=arial,sans-serif]
Hivi sasa Bw. Hosea anajenga jumba la kifahari wilayani Maswa, huku akimiliki jingine kubwa nchini Marekani, hali ambayo inafanya kuwepo kwa kiini macho cha kiutendaji ndani ya Takukuru.

Kwani kujenga ni dhambi?nijuavyo mie Hoseah PhD. ana kampuni yake ya uwakili hadvocates,Hawezi kukosa pesa ya kujenga nyumba kwao Maswa labda kama una jingine.Wanahabari na watendaji wa nchi hii, ili tunsaidie Rais Kikwete katika vita dhidi ya rushwa ni lazima tumshauri kwa hoja za kina, na tusifikie mahali tukadanganyika na suti za mtu, tukashindwa kueleza ukweli.

haya sasa ni majungu.Elezea mapungufu yake na sio kutoa hoja dhaifu,suti ina tatizo gani na uwezo wa mtu tena mtu ambaye alishawahi kuwa Mkurugenzi wa upelezi wa PCCB?

Nategemea wanahabari mtalifanyia kazi hili, kwani katika Journalism, kunautendaji kama katika upelelezi na Uchunguzi, ambao ili uufanye kwa kiwango cha kuwasaidia wengine lazima ufanya kitu wataalamu wanasema kutafuta taarifa kwa mfumo wa 5W and H.
John githongo alivyoona Ruswa imekithiri Huko kenya alijitokeza mbele ya watu na kusema yote.Nyie ni wachunguzi sasa mchunguzeni na mje na majibu mbele ya watanzania,Mambo ya majungu muache.

Source ya CMB: watu wakabila..Najua Kamazima aliacha mambo ya Uhaya wake pale PCCB,Sasa hoseah Ni mzungu,Hana muda na Mambo hayo![/I]
 
M

Mugo"The Great"

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2007
Messages
263
Likes
8
Points
35
M

Mugo"The Great"

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2007
263 8 35
CMB,
Una ushahidi wa maneno haya hapa chini? kama kuna mtu alimrekodi irusheni kwenye vyombo vya habari vya kuaminika, kinyume chake itakuwa ni kujadili hisia za watu.

"Poleni sana yote ambayo Wakurugenzi wangu mnayapeleka Ikulu mie nayajua, kila siku mnajihimu ikulu mkitegemea kuwa mtaweza kujaribu kuyarekebisha haya, hamuwezi hata kwa dawa, ukweli ni kwamba ukienda kwa Luwanjo (Katibu Mkuu Kiongozi) na yeye akimwambia Jakaya(Rais) Lazima jioni katika kijiwe chetu aniambie yote, na mara nyingine hata hunishauri nimpelekee mapendekezo ya kuwakandamiza ili awapige chini" ni sehemu ya sentensi ya Bw. Hosea aliyoitoa Marangu mbele ya maafisa mbalimbali wa Taasisi hiyo.
 
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2007
Messages
2,505
Likes
32
Points
135
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2007
2,505 32 135
Mugo"The Great";109189 said:

CMB katumwa tu..
 
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2007
Messages
2,505
Likes
32
Points
135
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2007
2,505 32 135
CMB umekimbilia wapi na maneno yako ya majungu??
 
A

Asha Abdala

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2007
Messages
1,134
Likes
5
Points
0
A

Asha Abdala

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2007
1,134 5 0
Takukuru msalabani

na Schola Athanas
Tanzania Daima

BAADHI ya wakazi wa Dar es Salaam jana waliipasha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa hawana imani nayo kutokana na kutoa ripoti zinazoleta shaka.
Wakizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Takukuru kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili jana, wananchi hao walihusisha ushiriki wa taasisi hiyo katika sakata la Kampuni ya kufua umeme ya Richmond Development (RDC) kuwa ni moja ya matukio yaliyowafanya wapoteze imani na Takukuru.

Walisema kitendo cha Takukuru kufanya uchunguzi na kubaini kuwa hakukuwa na rushwa katika suala la kuipata kampuni hiyo, na baadaye Bunge kuunda kamati ya kupata maoni kuhusiana na suala hilo, baada ya kubaini kuwa kuna harufu ya rushwa, kinaishushia hadhi taasisi hiyo.

Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa masuala ya Bunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mrema, alipokuwa akichangia mada kwenye mdahalo wa wazi kuhusu Rushwa na Maadili.

"Takukuru ni waongo, kwani hufanya kazi yao kwa kuwaogopa wanasiasa na hivyo kushindwa kutimiza maadili ya kazi yao," alisema Mrema.

Mrema aliwataka Takukuru kuacha kuwa wanasiasa, kwani wanatakiwa kufuatilia tuhuma wanazoletewa na kuacha kuhoji ushahidi, kwani wao ndio wanatakiwa kuchunguza na kutafuta ushahidi huo na si mtoa taarifa.

Aidha, Mrema alisema viongozi wanaotiwa hatiani kwa tuhuma za rushwa wasipewe adhabu ndogo ndogo bali wapewe adhabu kali, ikiwa ni pamoja na kufilisiwa mali zao zote.

Pia alisema sekta binafsi nako kunafukuta rushwa kutokana na kukosekana kwa maadili, hasa ikizingatiwa kuwa sehemu kubwa ya shughuli nchini hufanywa na kampuni na taasisi binafsi.

"…kwa mfano hapa tupo katika mjadala wa rushwa na tumepewa T-shirts za Takukuru huku pembeni zikiwa na nembo ya ENGEN, ambalo ni kampuni la mafuta. Unafikiri kampuni hii ikiwa na tuhuma za rushwa wataweza kuwakamata wakati ni wafadhili wao? Hapa maadili yatatoka wapi?" alihoji Mrema.

Alisema ili Takukuru na hata serikali iwe huru kufanya mambo yake bila kuathiriwa, ni lazima iachane na kutegemea wafadhili, hasa kampuni binafsi.

Wakati huo huo, Abubakar Kitogo ambaye ni Ofisa wa Chama cha Wananchi (CUF), akichangia katika mdahalo huo, alidai kuwa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi imeshindwa kufanya kazi yake ipasavyo, kwani haijaonekana kuchukua hatua dhidi ya wala rushwa.

"Nimesema hivyo kwa kuwa wanasiasa wameishasema na kutoa ushaidi kuhusiana na tuhuma za rushwa, ikiwa ni pamoja na nyumba zilizouzwa, mkataba wa Richmond, Buzwagi na mingine mingi lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa," alisema.

Kitogo alisema hii yote inasababishwa na katiba mbovu iliyopo na bila kuifanyia marekebisho itakuwa vigumu kupambana na rushwa na kushinda.

"Hata rais anawajua wala rushwa kwa majina… kusema eti anawapa muda wajirekebishe, hii inathibitisha hata hii taasisi ya Takukuru ni uzushi mtupu," alizidi kudai.

Naye Zawadi Sanga, mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Ualimu Chang'ombe (DUCE), alisema viongozi wa ngazi za juu ndio wanajenga mazingira ya rushwa na kuishia kuunda tume nyingi ambazo hutumia fedha nyingi bila kuleta majibu yoyote ya maana.

Sanga alisema serikali ikitaka kutokomeza rushwa ni lazima ihakikishe inaboresha masilahi ya watumishi wake, kwani inasikitisha kuona mfanyakazi analipwa sh 80,000 na ana familia inayomtegemea.

"Huyu akipokea rushwa kweli utamlaumu?" alihoji na kuongeza:
"Na hii ndiyo sababu inayofanya hata maprofesa wengi kuacha kazi ya kufundisha na kujiingiza katika mambo ya kisiasa ili waweze kupata masilahi yatakayo wawezesha kukimu mahitaji yao muhimu."

Pia Edwin Chitage, ambaye ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi katika Chuo cha Sayansi za Tiba Muhimbili, alisema ili kuhakikisha rushwa inaondoka katika taasisi za umma, kinachotakiwa si kuboresha masilahi ya wafanyakazi tu, bali kuboresha huduma pia.

Chitage alisema katika hili, viongozi wakubwa wanapaswa kuacha tabia ya kwenda kufanya ziara mahospitalini kwa nia ya kujionyesha tu, bali wawe wanakwenda kupeleka vifaa mbalimbali.

Aidha, Chitage alisema ni vigumu kuzungumzia suala la maadili wakati haijulikani hasa nchi inafuata siasa gani, kati ya ujamaa inayoelezwa katika katiba au ubepari, ambayo ndiyo inayoonekana katika hali halisi.

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Loyola, Godfes Msofe, alisema rushwa haitaisha nchini kutokana na viongozi, hasa wa ngazi za juu, kutokuwa waaminifu, waadilifu na kulindana katika utendaji wao wa kazi.

Msofe alisema kuna baadhi ya mifumo haipo wazi, na kutoa mfano wa suala la kusainiwa kwa mikataba mbalimbali, ambayo hufanywa kwa siri bila wananchi kujua.

Mjumbe mwingine ambaye jina lake halikupatikana mara moja, aliituhumu Takukuru na kusema kuwa si taasisi ya kuaminika kwa kuwa haionyeshi mafanikio katika vita dhidi ya rushwa.

Mjadala huo wa wazi uliokuwa unaendeshwa na mhadhiri wa Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC), Ayub Rioba, uliandaliwa na Takukuru, ikiwa ni moja ya maadhimisho ya Siku ya Maadili Kitaifa ambayo hufanyika Desemba 10 kila mwaka. Kaulimbiu ya mwaka huu ilikuwa ni "Kukataa kwako rushwa kuna thamani."

Mjadala huu ulikuwa na utangulizi wa mada tatu ambazo ni umuhimu wa maadili ya umma kama njia ya kuzuia rushwa, umuhimu wa kuzingatia maadili katika utendaji wa sekta binafsi na wanafunzi na mapambano ya rushwa na ulishirikishaji wa wanafunzi kutoka sekondari na vyuo mbalimbali.
 
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2007
Messages
2,505
Likes
32
Points
135
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2007
2,505 32 135
Takukuru msalabani

"Takukuru ni waongo, kwani hufanya kazi yao kwa kuwaogopa wanasiasa na hivyo kushindwa kutimiza maadili ya kazi yao," alisema Mrema.

Mrema aliwataka Takukuru kuacha kuwa wanasiasa, kwani wanatakiwa kufuatilia tuhuma wanazoletewa na kuacha kuhoji ushahidi, kwani wao ndio wanatakiwa kuchunguza na kutafuta ushahidi huo na si mtoa taarifa.

.
brazo John Mrema,Waziri mkuu wa Zamani wa Serikali ya wanafunzai wa chuo kukuu cha Dar es salaam(DARUSO),Sikujua wakati unakisifia chadema kipinde kile kumbe ulihaidiwa uongozi,Nakukumbuka sana hasa kipindi kile nasoma Masters pale Mlimani..wewe ulikuwa Bingwa wa kuuza Vyumba.sasa leo unaona TAKUKURU hawafanyi kazi..au kwasababu walikuacha uuze vyumba.?
wewe bado fisadi tu,Asilimia kubwa ya viongozi wa upinzani ni wale watu walioona chama hakiwakubali ndio mkaamua kwenda huko,Ngudu yako Mwita nasikia yuko Tanga huko anasaidia chama.
Suala la Richmond tusubiri kuona ripoti ya Jk kama itakuwa tofauti na Ripoti ya Hosea basi ndio tumhukumu Dr. Hoseah,ila kwa sasa tumuache aijenge takukuru
 
O

Ogah

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
6,232
Likes
91
Points
145
O

Ogah

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2006
6,232 91 145
Mkuu CMB,

Heshima mbele..................kati ya yaliyosemwa nakumbuka kuna wakati fulani tena kipindi cha General Kamazima huyo Kamanda wa shinyanga ndio alihamishwa, kwa hiyo si kweli kwamba Hosea ndio aliyemtoa....ni Gen Kamazima....ni kweli the guy must have been frustrated kwa kitendo cha kuhamishwa.

However................do not let the guy buy you CMB with cheap shots.............im sure utawala mpya wa PCCB umemuathiri sana

watu wakitaka PCCB ifanye kazi yake ipasavyo....hiki chombo lazima kiwe somehow independent...............short of that tutaendelea kuwa na mikutano, makongamano, semina, warsha, kamati, tume nk nk kuhusu rushwa
 
Bora umenenea,CMB credibility yako inapungua,Unajua kuna watu wanatak kila siku wao ndio wawe juu,sasa taztio linaanzania pale wanapokuwa chini..
 
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,134
Likes
73
Points
145
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,134 73 145
udaku tuna wivu,hao watu wa PCCB walizoe kula pesa tu na hawafanyi kazi ya maana,wanapewa oc kwa mwaka mzima kuna kuwa na kesi 100 tu za rushwa huku bajeti yao kubwa..nachokijua Dr. Hoseah anataka kuibadili PCCB iwe ya kisasa na ya kisanyansi na sio mambo ya kurundika vihiyo..Nilimsikia akiteta Jumamosi katka harusi moja ambyo na mie nilikuwapo.Dr. hoseah andonekana mtu makini sana..watu wanaomlaumu Dr. Hoseah ni wale wanaoendekeza ukabila.

Haya hapa juu ni maneno yako.

brazo John Mrema,Waziri mkuu wa Zamani wa Serikali ya wanafunzai wa chuo kukuu cha Dar es salaam(DARUSO),Sikujua wakati unakisifia chadema kipinde kile kumbe ulihaidiwa uongozi,Nakukumbuka sana hasa kipindi kile nasoma Masters pale Mlimani..wewe ulikuwa Bingwa wa kuuza Vyumba.sasa leo unaona TAKUKURU hawafanyi kazi..au kwasababu walikuacha uuze vyumba.?
wewe bado fisadi tu,Asilimia kubwa ya viongozi wa upinzani ni wale watu walioona chama hakiwakubali ndio mkaamua kwenda huko,Ngudu yako Mwita nasikia yuko Tanga huko anasaidia chama.
Suala la Richmond tusubiri kuona ripoti ya Jk kama itakuwa tofauti na Ripoti ya Hosea basi ndio tumhukumu Dr. Hoseah,ila kwa sasa tumuache aijenge takukuru

Haya nayo ni maneno yako.
1. juu unaipinga TAKUKURU kuwa wanalipwa fedha nyingi na hawafanyi kazi.
2.Chini unasema kuwa Hosea aachwe kwani anaijenga TAKUKURU.

Tukuelewe kuwa msimamo wako ni upi?

3.Umemshambulia huyo Mrema na kusema kuwa alikuwa anauza vyumba na umesema kuwa ulisikia wakisema wakati wewe ukiwa unasoma masters je?waweza kuthibitisha kwani hizi ni tuhuma nzito na sidhani kama CHADEMA watamvumilia ikidhibitika kuwa alikuwa anafanya biashara ya vyumba wakati akiwa Katibu mkuu /waziri mkuu wa DARUSO.

Nasubiri majibu yako tafadhali, na pia ushahidi.
 
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2007
Messages
2,505
Likes
32
Points
135
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2007
2,505 32 135
nimelezea TAKUKURU Ilipokuwa na wapi inakwenda mwaka jana walipeleka kesi 100 tui mahakamani,Dr. Hoseah amegundua kuna mapungufu katika utendaji.

Kuhus kijana huyo wa kichaga si siri,Kauza sana vyumba huyo kijana na vingine aligawa kwa rafiki zake kwa karibu kipindi hicho wakati Mwita Mkikwabe alikuwa RAsi wa DARUSO,Hayo mambo yako sana DARUSO na wala usimtete yeye Si Msafi,Kwanza CHADEMA kumejaaa UKABILA,chama hicho ni cha watu wa Moshi.

Mpaka kieleweke na tena uthithubutu na kamwe uthithubutu kunitisha,ukitaka ushahidi wasiliana nami katika PM.
 
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,134
Likes
73
Points
145
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,134 73 145
Weka ushahidi hadharani ndugu wacha woga kwa nini umtuhumu mtu in public halafu ushahidi umtumie mtu mwingine in private?

Umetishiwa kwa kipi mkubwa?mbona unaishi kwa hofu sana? the only thing to fear is fear by it self.

Najua kuwa huyu kijana alikuwa DARUSO na alishiriki kumfukuza waziri wa makazi hapo mlimani kwa tuhuma za kuuza vyumba wakati wao.
Najua naye ni mwanachama hapa aje ajitetee.
 
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2007
Messages
2,505
Likes
32
Points
135
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2007
2,505 32 135
Weka ushahidi hadharani ndugu wacha woga kwa nini umtuhumu mtu in public halafu ushahidi umtumie mtu mwingine in private?

Umetishiwa kwa kipi mkubwa?mbona unaishi kwa hofu sana? the only thing to fear is fear by it self.

Najua kuwa huyu kijana alikuwa DARUSO na alishiriki kumfukuza waziri wa makazi hapo mlimani kwa tuhuma za kuuza vyumba wakati wao.
Najua naye ni mwanachama hapa aje ajitetee.
kijana,haihitaji ushahidi kuhusu Bwana Mream,Hata Kampeni zao zilitawaliwa na Rushwa ya kuwanyweshwa Watu Pombe pale UDASA,Wao kama wanafunzi walitoa wapi pesa ya kunyweshwa watu?tatzio la CHADEMA mnatafuta wasomi kwa kkasi sana,sababu mnajua wana pesa watawasaidia kushinda majimbo ya uchaguzi,Kama kampeni yenu ya kusaka billion Moja,Mnapotea..WEkeni Sera nzuri then watu watapa kura,na sio Propaganda.
 
M

Mugo"The Great"

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2007
Messages
263
Likes
8
Points
35
M

Mugo"The Great"

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2007
263 8 35
Mbona mjadala unahamia kwenye vyama na ku-personalize issues badala ya kuijadili TAKUKURU?

Si siri wananchi wengi hawana imani na TAKUKURU. Maisha wanayoishi Viongozi wetu wengi wa serikali hayana mlingano na Kipato chao. Huo ni ushahidi tosha kabisa wa kimazingira kuwa ni mafisadi na kama TAKUKURU ingekuwa "HURU" leo tungeshuhudia mapinduzi makubwa sana ya kimaadili. Lakini kwa vile "WAO" huteuliwa na serikali inakuwa ni vigumu sana kuwashughulikia Viongozi wa "Sirikali" hata wanapoingia mikataba ya Kilaghai.
 
Forum statistics

Threads 1,237,572
Members 475,562
Posts 29,293,863