TAKUKURU na CAG fuatilieni hili la Mkurugenzi wa UCC

Fanfa

JF-Expert Member
Sep 25, 2009
1,815
2,862
Heshima kwenu wana jamiiforums,

Nimepenyezewa taarifa zinazohusu mazingira ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka yanayofanywa na mkurugenzi wa kampuni ya chuo kikuu cha Dar es salaam iitwayo University of Dar es Salaam Computing Centre (UCC), Dr. Ellinami Minja.

Nimeona ni vyema niliseme hili ili vyombo husika vichunguze na kubaini ukweli wa jambo hili. Serikali yetu inapinga kwa nguvu zote rushwa za aina zote (fedha na ngono) na matumizi mabaya ya madaraka na hasa katika taasisi za umma.

Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye hoja niliyopenyezewa.

Ni kwamba Dr. Ellimani Minja ambaye ni Mkurugenzi wa UCC inasemekana alitumia madaraka yake kumwajiri mwanamama aitwaye Nkwaya Esther Kipilyango. Mwana mama huyu inasemekana ana mahusiano yenye kutia mashaka na mkurugenzi huyo, Mnyetishaji anasema, mahusiano yao yalianza tangu wakati anasoma pale chuo kikuu cha Dar es salaam, shule ya Biashara (UDBS) na Dr. Minja ni mwalimu anayefundisha pale UDBS.

Kwa kutumia madaraka yake alimwajiri na kumpa mshahara mkubwa tofauti na kiwango cha Elimu (Academic Qualifications) alichonacho. Nkwaya Esther Kipilyango ni mhasibu mwenye Bachelor of Commerce (GPA 2.9) aliyopata mwaka 2007 kutoka shule ya biashara, chuo kikuu cha Dar es salaam (UDBS). Baadae May 2015 alifanya mitihani ya CPA na kupewa cheti. Bado hajawa mwanachama kamili kwenye hiyo taaluma (full membership of the profession). Hana elimu nyingine zaidi ya hii kwa mujibu wa mtoa taarifa.

Taarifa zinasema kuwa Mkurugenzi huyu kwa kutumia madaraka yake alimpendelea mwana mama huyu na kumpa mshahara ambao uko nje ya scheme of services. Kwa mujibu wa mtoa taarifa alisema, mshahara wa juu kabisa (senior officers) kwa kada ya wahasibu (senior Accountant) na maafisa utumishi na utawala (Senior Human Resources and administrative officers) kwa mujibu wa scheme of service ya UCC ni TZS 2,865,000/-. Lakini mwanamama huyu alipewa mshahara wa milioni tatu na laki saba (3.7 million).

Mtoa taarifa alitoa mfano kuwa kuna wahasibu ambao wameajiliwa siku nyingi ambao wanamzidi ama wanalingana kiwango cha elimu lakini wanalipwa chini ya milioni 2.5. Hata mhasibu mkuu (Chief Accountant) ambaye naye ana CPA mshahara wake hauzidi milioni 2.5. Swali la kujiuliza iliwezekanaje huyu alipewa mshahara wa milioni 3.7 wakati hana sifa za ziada. Kama sababu ni kuwa mkuu wa idara, mbona kuna mkuu wa idara ambaye ana PhD na yuko kwenye senior position kwa zaidi ya miaka 18 kama mkuu wa idara, lakini mshahara wake hauzidi milioni 2.8.

Namna alivyoajiliwa UCC:

Mnyetishaji aliendelea kusema kuwa mwishoni mwa mwaka 2018, Mkurugenzi wa UCC alitangaza kazi nafasi ya Finance and Administration Manager (FAM). Nkwaya Esther Kipilyango alikuwa miongoni wa watu waliofanyiwa usaili (interview). Pamoja na kwamba kuna kamati ya ajira (recruitment committee), lakini Dr. Minja alidai kuwa kwa nafasi ya FAM interview inatakiwa ifanywe na yeye badala ya kamati ya ajira. Mkurugenzi huyu akaunda kamati ndogo yeye ndo akawa mwenyekiti wa kamati. Waliitwa waombaji watatu (3) kwa ajili ya interview akiwepo Nkwaya Kipilyango. Mwombaji mmoja alihudhuria interview ya kwanza ambapo ya pili hakufika yaani negotiation ya mshahara.

Inasemekana Nkwaya Kipilyango hakufanya vizuri kwenye usaili (interview) maana alipobanwa maswali na wajumbe wengine alifika mahala akatoa kilio. Alipoulizwa kwa nini unalia akajibu kuwa ana “Domestic problems” ndiyo maana ameshindwa kujibu maswali mengine kwa kuwa hayuko vizuri kisaikolojia na kwamba ana matatizo ya kifamilia. Wajumbe wengine walisema kuwa kwa sifa alizonazo hatoshi kwenye nafasi aliyoomba ya Finance and Administration Manager, kwa kuwa hajasomea mambo ya Human resources management and administration. Lakini Dr. Minja kwa kuwa ndo alikuwa mwenyekiti alidai kuwa CV ya Kipilyango inaonyesha ana Master ya Business Administration in Human Resources Management japo hapakuwepo na cheti cha kudhibitisha. Aliwashawishi wajumbe kuwa anamfahamu na kwamba anafundishika (trainable). Kwa maoni yake aliona kuwa huyo ndo anafaa kuwa FAM, japokuwa naibu mkurugenzi wake alisema wazi kuwa huyu hatatufaa kwenye nafasi hii, na mwisho walikubaliana na maoni ya mkubwa kwa kuzingatia kuwa mkubwa hapingwi.

Mtoa taarifa anaendelea kusema kuwa Mkurugenzi (Dr. Minja) alijua kabisa asiposimamia usaili pengine angepewa mtu mwingine ajira hiyo. Mkurugenzi alitumia madaraka yake akaicheza karata vizuri ili kuhakikisha Nkwaya Esther Kipilyango anaipata hiyo kazi. Mtoa taarifa anasema pia kuwa mwanamama huyu alidanganya wakati wa interview na kwenye CV kuwa ana MBA in Human Resources management, cha ajabu ni karibu miaka miwili kashindwa kuwasilisha cheti hicho na mkurugenzi yuko kimya kwa hilo.

Wafanyakazi wamekuwa wakihoji kuwa;
  • Kwa nini apewe mshahara mkubwa ambao haulingani na elimu yake
  • Je kuna scheme of services nyingine ambayo mkurugenzi huyu anaitumia
  • Kwa nini anafanya kazi za Human resources management and administration wakati hajawahi kusomea kazi hiyo. Wakati huo huo kuna watumishi ambao wana masters na wamesomea kazi hiyo.
Hoja hizi zilimfanya mwana mama huyu kuanza kusoma MBA in Human Resources management. Inasemekana anaendelea na masomo ya jioni. Lakini kufanya hivo hakutaondoa ukweli.

Inasemekana kuwa mwana mama ana kiburi na dharau ya hali ya juu kwa watumishi wengine. Mnyetishaji amesema atanipa taarifa kamili kuhusu swala la kunyanyasa watumishi na hata wakilalamika kwa mkurugenzi hawasilikizwi na kwamba alipoajiriwa tu hakumaliza miezi miwili akampiga mfanyakazi. Mtoa taarifa alitaja jina moja la mtu aliyepigwa kuwa ni ndugu Michael.

Nimeamua kusaidia kuweka taarifa hii wazi ili TAKUKURU na ofisi ya CAG wafanye uchunguzi kubaini ukweli kama;
  • Mkurugenzi alitumia madaraka yake vibaya kuhakikisha kuwa mwanamama huyu anamwajiri bila kuwa na sifa husika
  • Kulikuwa na upendeleo katika kumwajili mwana mama huyu
  • kuna upendeleo wa kupewa mshahara asiostahili na kwa nini uko nje ya UCC scheme of services
  • Je ni kweli ana MBA na cheti anacho kama ilivyoandikwa kwenye CV yake.
  • Kamati ya ajira haikuhusishwa
  • Mwana mama huyu anatisha wafanyakazi na wakati mwingine kuwapiga
Kwa kuwa TAKUKURU na ofisi ya CAG wana utaalamu mkubwa wa kiuchunguzi wataweza kupata ukweli juu ya tuhuma hizi dhidi ya mkurugenzi wa UCC.

Uzi unaofuata nitawaletea kwa undani baada ya kukusanya taarifa za kutosha kuhusu mfanyakazi anayelipwa kwa dola kama expert kutoka nje wakati ni mtanzania. Yajayo yanafurahisha.
 
Mi nadhani ungepeleka ushahidi Takukuru kuliko kuandika humu ni kuzalilishana tu nachokiona, msigeuze JF ionekane kama ni kijiwe cha mtu kuandika mabaya na kutaja Majina ya watu tuwe tunapeleka hayo mambo idara husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hofu yako nini mkuu. Wahusika watalifanyia kazi na ukweli wataupata
 
Back
Top Bottom