njeeseka
JF-Expert Member
- Oct 19, 2012
- 1,371
- 976
Kuna unyanyasaji na mateso makubwa wanafanyiwa wastaafu wa private sector pindi wanapoomba kupewa mafao yao. Kuna watu zaidi wa watano nimewasikiliza na kuona kuna bomu kubwa hapo NSSF UBUNGO.
Kuna wanaolalamika kwamba ukiomba kulipwa michango yako utazungushwa sana mpaka uwape kuanzia laki tano (500,000) hadi milioni.
Imefikia hatua maafisa wanaoshughulikia madai ya wastaafu/walioachishwa kazi WANAFICHA MAFAILI na pindi pesa ikitolewa mafaili yanaonekana.
Hii sio tabia mzuri piatabia inayokera sana hasa ukizingatia hiyo ni michango halali ya wanachama.
Yupo aliyediriki kusema ni bora kwenda kuanzishia madai yako mkoani kuliko hapo UBUNGO.
Niwaombe TAKUKURU hizi ni tuhuma zifanyieni kazi kama kuna mafaili yanafichwa mtajua tu -ombeni orodha ya maombi yaliyowasilishwa hapo na muone yamelipwa lini, mtaona kuna waliotoa pesa wakalipwa haraka na kuna walioomba tarehe sawa na aliyelipwa na bado mafaili yamefichwa.
Uongozi wa hapo inaonekana umeshindwa kusimamia watendaji wanaodhalilisha ofisi hiyo.
Inakera sana usiombe ukutane na mtu aliyefanyiwa hivyo utamuonea huruma.
TAFAKARINI NA MJIULIZE ENDAPO SERIKALI TULIYO NAYO YA MHE. MAGUFULI KAMA INARUHUSU HAYO WANAYOYAFANYA