TAKUKURU mulikeni mchakato wa ajira za TPDC uliosimamiwa na TAESA

Capsicum

Member
Jul 20, 2018
24
30
Straight to the point.

TAKUKURU hebu kwa heshima na taadhima nawaomba mkafuatilie huu mchakato jinsi ulivyofanyika maana una viashiria vya RUSHWA ndani yake, kwanini nasema hivi:-

1) Hakukua na tangazo la ajira publicly watu waliitwa kwa kupigiwa simu kwenda kufanya usaili.

2) Baada ya usaili kufanyika watu walianza kupigiwa simu waende kusign mikataba ya ajira

Sasa hapa ndio ujanjaujanja ulipoanza.. Ikumbukwe kwenye kampuni tanzu za TPDC especially GASCO kuna vijana wamekua wanafanya intern kwa muda mrefu wengine hadi miaka miwili inafika. Hivyo vijana hawa ndio wana uelewa mkubwa sana kuhusu process zote za GASCO ila cha kushangaza watu waliopewa hizi ajira ni tofauti kabisa.

Imagine unamuajiri mtu kutoka NHC, TEMESA aende akafanye kazi kwenye Gas processing plant wakati kuna intern amekuwepo huko kwa zaidi ya mwaka na anajua kila kitu!

Wakati wa usaili kulikua na vigezo vinavyotakiwa ikiwepo mtu kua amehudumu kama intern ktk shirika kwa muda kadhaa, awe amesajiliwa na board kama graduate engineer lakini unakuta waliosign hizo cintract kwanza wengine hawajawahi kufanya kazi TPDC, wengine hawajasajiriwa na board! Kigezo gani kilitumika kuwachagua hao watu?

Kama kweli tupo serious na process za uchakataji Gas kwanini tunaajiri watu ambao hawajui kitu kuhusu hizo kazi na tunaacha watu ambao wamekua wanawakiwa na jua muda mrefu wakilitumikia shirika kwa moyo mmoja na kwa ujira mdogo?

Kiukweli TPDC/TAESA mmewavunja sana moyo vijana hawa waliojitolea kulitumikia shirika kwa muda mrefu na mwisho wa siku mmewatupa pembeni.

Kazi kwenu TAKUKURU, mkafanyie kazi ili mjiridhishe mkikuta mchakato ulikua sawa itapendeza ila kama haupo sawa hatua kali zichukuliwe kukomesha huu uonevu.
 
Tuanzie hapa kazi ni permanent au temporary maana kazi zote za kudumu serikalini muajiri sio TAESA ni PSRS (public service recruitment secretariat) chini ya utumishi na TAESA iko chini ya ofisi ya waziri mkuu jukumu ni kusidia vijana kupata intern au ajira makampuni binafsi
 
Hizo ndio kazi za TAKUKURU. Sio kama alivyosema Dr Gwajima eti wamkamate Mbunge wa Kawe kwa kupinga chanjo
 
tuanzie hapa kazi ni permanent au temporary maana kazi zote za kudumu serikalini muajiri sio TAESA ni PSRS ( public service recruitment secretariat) chini ya utumishi na TAESA iko chini ya ofisi ya waziri mkuu jukumu ni kusidia vijana kupata intern au ajira makampuni binafsi
TAKUKURU ndio wataenda kupata ufafanuzi sehemu husika
 
Kwa Serikali hii ya Awamu ya 6 hiko kitu hakiwezi kufanyika na Serikali iko bize na Chanjo
 
tuanzie hapa kazi ni permanent au temporary maana kazi zote za kudumu serikalini muajiri sio TAESA ni PSRS (public service recruitment secretariat) chini ya utumishi na TAESA iko chini ya ofisi ya waziri mkuu jukumu ni kusidia vijana kupata intern au ajira makampuni binafsi
Nadhani wamepelekwa kwa ajili ya internship na sio ajira.

TAESA inapeleka vijana wengi kwenye taasisi za serikali na binafsi kwa ajili ya kupata uzoefu kwa muda wa mwaka mmoja na sio kwamba wanataftiwa ajira.

Na hata mishahara ama posho wanalipwa nauli kutoka ofisi ya waziri Mkuu.

Huyo jamaa alete tangazo la ajira ya hizo kazi kama aliliona.
 
Lifestyle ya awamu ya nne kipindi cha JK imerudi kwa kasi kubwa. Wasiostahili ndio wanapewa vitengo. It is very painful.
Tuambie mtu kama Mpuuzi Makondo na wanaofanana na hao walipewa kazi na nani ?
 
Walau ajira zimeanza kuonekana sio wakati ule ajira zilikuwa ni kwa ajili ya akina Chato tu na watu wanaofanana na hao
Ajira hizi za kupeana.

Kuna tukio lilitokea Serikali ya Awamu ya 5 kuna ajira za Tenesco , Interview walikuwa wanasimamia Tenesco . Baada ya watu kupiga kelele kulalamika mchakato wa Ajira. Utumishi wakaingilia kati ikabidi mchakato nzima wa Ajira usimamiwe Na utumishi.

Hiki Kitu inabidi ifanyeke kwa Ajira Hizi za TPDC, je kitawezekana.

Awamu ya 5 Ajira zilikuwa chache ila siyo za ubabaishaji
 
Nadhani wamepelekwa kwa ajili ya internship na sio ajira.

TAESA inapeleka vijana wengi kwenye taasisi za serikali na binafsi kwa ajili ya kupata uzoefu kwa muda wa mwaka mmoja na sio kwamba wanataftiwa ajira.

Na hata mishahara ama posho wanalipwa nauli kutoka ofisi ya waziri Mkuu.

Huyo jamaa alete tangazo la ajira ya hizo kazi kama aliliona.
Hawa interns wanalipwa kiasi gani?
 
-------------------- UPDATES ------------------------


Kwanza nitoe shukrani kwa taasisi yetu ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kwa kulifanyia kazi hili suala. Ni matumaini yangu kua kuna kitu wamebaini katika mchakato wa hizi ajira ndio maana kuna candidate mmoja mkataba wake ulisitishwa mara moja baada ya kuonekana hakua na sifa stahiki kuhudumu katika nafasi aliyopewa.

Pamoja na hilo ningependa TAKUKURU wajiridgishe na mambo yafuatayo incase hawajayajua bado:-

1) Katika hao vijana hao walioajiriwa kimchongo kuna mmoja wao ambae (kwa makubaliano) analazimika kukata sehemu ya mshahara wake (sina hakika ni robo au nusu) na kumpa aliyempigia pande akaajiriwa. Hii sio haki kwani kama ni kulipa fadhira basi ingekua mara moja tuu kiungwana inatosha.

2)Katika hao waajiriwa kuna employees wanne (4) ambao INASEMEKANA waliitwa na kupewa mikataba bila kufanya usaili (inawezekana walikua kwenye database ya TAESA) lakini sio mbaya mkaenda kujiridhisha.


------KAZI IENDELEE------
 
Back
Top Bottom