Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Awamu ya sita inalo Jambo la kutafakari kuhusu mmomonyoko wa maadili unaoendelea Nchini. Tumewalea watu wachache wameafika mahali wananguvu kuliko Viongozi wa kitaifa. Tunaweza tukadhani tunapambana na wapinzani kumbe tunapambana kuuwa usawa katika jamii.
Tuna vyombo vya dola ambavyo kwa kiasi kikubwa vimeshindwa kutekeleza majukumu yao bila kuelekezwa na Rais au Waziri Mkuu. Tukio lililotokea Clouds leo la mahojiano Kati ya Sabaya DC wa hai na mtangazaji wa chombo hicho ni moja ya vitu vinavyofanywa na mtu huyu mmoja adharani bila utawala kuhoji Wala kukemea. Huyu DC alianza kufanya vurugu Hai akiwa anaambatana na polisi, akaingia kuvamia biashara na makazi ya watu akiwa na silaha Leo hii amenunua kipindi kwenye Televisheni kusafisha au kuongea Yale anayodhani yanamsafisha kuendana na utawala uliopo.
Naomba Takukuru mtuambie alichofanya DC kununua kipindi kwenye chombo cha habari kujadili masuala ya serikali Ni rushwa au siyo rushwa. Kama siyo rushwa well and good lakini Kama ni Rushwa inayolenga kupata upendeleo Basi nategemea hatua zichukuliwe.
Kwa upande wa CCM nadhani huu ni wakati wakuamua njia sahihi yakusonga mbele, mnaweza mkaamua kusonga mbele kwa kutumia mabavu kukandamiza watu au mkasonga mbele kwa kuondoa uonevu na watawala wenye mabavu. Tusione kimya Cha wananchi tukadhani wao wanafurahia dhuluma, tuelewe wananchi wanavumilia kwa sababu hawana uwezo wakuelekeza dola itende haki.
Lakini kumbukeni dharau ya Sabaya inakwenda mbali nakuamthiri RC na hata Waziri wa utawala Bora. Kumjenga mtu mmoja akawa na nguvu kuliko taasisi zinazomsimamia ni hatari kwa mustakabali wa taifa, ipo siku huyu mtu atakuza mtandao wake nakufanya Jambo kubwa zaidi ya tunayoaona adharani leo.
Tanzania siyo nchi yakufuata Wafanyabiashara na SmG usiku wa manane, siyo nchi ya DC kubeba silaha nzito ni nchi ya amani. Na Kama tunaamini ni nchi ya DC kubeba silaha nzito tungeona na wakuu wengine wa wilaya nchini wakifanya hivyo. Hatuoni DC mwingine hata ndani ya mkoa wa Kilimanjaro akifanya haya, je hai Kuna Nini zaidi au DC wake ana Nini anachodhani anaweza kufanya kuliko watu wengine Hadi atumie silaha?