TAKUKURU mpo mnatazama mchezo wa kuhonga watu kwa fedha za umma ili wahame vyama

ntemintale

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
952
1,871
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mpo, mkitazama mchezo wa kuhonga watu wahame vyama, kwa fedha za umma. Nawakumbusha tu kwamba hakunaga Rais anayedumu milele.

Rais Magufuli na wasaidizi wake wote watapita. Atakuja Rais mpya na mambo yake mapya. Atafukua kila ovu lililotendeka kipindi cha utawala huu wa Rais Magufuli. TAKUKURU hamtabaki salama. Ni kheri mkafanya kazi zenu kwa weledi leo, ili kesho mkumbukwe.

Ni ushauri wa bure.
 
Makonda a.k.a Maliyamungu Bashite yy ana mkataba na Mungu anajua kuwa Mungu atamweka madarakani Mtukufu malaika wa chato mpaka milele kama Mseveni wa Uganda, Wamebuni Mladi wanakula Pesa za walipa kodi kuwanunua Wapinzani kurudia uchaguzi ni Ufisadi wa kisayansi, Pesa za Umma zinatumika kwa mambo ya hovyo hovyo ili Maliyamungu Bashite na Lipumba wapate 10% zao ni Ufisadi Hatari kuliko wote uliopata kutokea huko nyuma.
 
Huwatakii mema wenzako!! Unataka wafukuzwe kaz?? Serikali ndio huteua viongoz wa takukukuru, tuanze na mfumo kujitegemea ndio tuwape majukumu makubwa
Waziri mkuu, makamu wa Rais mpaka mawaziri wote wanamuogopa Bashite Maliyamungu Sembuse boss wa Takukuru, Kwa sasa Maliyamungu anaogopwa kama yule Maliyamungu wa enzi za idd Amin Dada wa Uganda hakuna ambaye anaweza kubishana nae akapona mbele ya Mtukufu malaika wa chato.
 
Nchi hii kwa sasa Rais mtendaji ni Maliyamungu Bashite na Mtukufu Rais yy ni Rais mkuu tu lakini kazi zote ushauri wote anapokea toka kwa Maliyamungu Bashite ambaye kapewa fungu kubwa la pesa kwa ajili ya kuua kudhoofisha upinzani hususani UKAWA, wanataka mwaka 2020 chadema CUF viwe hoi ili wakifanya uchakachuaji vishindwe kuwakemea.
 
Pesa za walipa kodi imetumika kwa kazi Haramu kuwanunua Wapinzani kurudia uchaguzi kisa Maliyamungu Bashite na Lipumba wana Dili lao wapate cha juu 10% kwenye manunuzi ya Wapinzani, Nchi imeharibika Madalali wa siasa wanatumia fursa kujipatia pesa Ufisadi wa pesa za Umma kwa kazi haramu ndiyo mladi mkubwa kwa sasa hakuna viwanda tena,
 
Taasisi ya dikteta uchwara hii, kama hataki kitu kichunguzwe hakichunguzwi ushahidi huu hapa chini.
Kalewa madaraka huyu uchwara.

Takukuru yachunguza Sh10 milioni za wabunge CCM

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mpo, mkitazama mchezo wa kuhonga watu wahame vyama, kwa fedha za umma. Nawakumbusha tu kwamba hakunaga Rais anayedumu milele.

Rais Magufuli na wasaidizi wake wote watapita. Atakuja Rais mpya na mambo yake mapya. Atafukua kila ovu lililotendeka kipindi cha utawala huu wa Rais Magufuli. TAKUKURU hamtabaki salama. Ni kheri mkafanya kazi zenu kwa weledi leo, ili kesho mkumbukwe.

Ni ushauri wa bure.
 
Watafanya nini ?Huyo mtoa pesa ndiye aliyewaajiri na wenyewe wanamchukulia kama ndiye mungu wao. Unataka wafanye nini? Wenye kupokea ndio wapuuzi
 
Nchi hii kwa sasa Rais mtendaji ni Maliyamungu Bashite na Mtukufu Rais yy ni Rais mkuu tu lakini kazi zote ushauri wote anapokea toka kwa Maliyamungu Bashite ambaye kapewa fungu kubwa la pesa kwa ajili ya kuua kudhoofisha upinzani hususani UKAWA, wanataka mwaka 2020 chadema CUF viwe hoi ili wakifanya uchakachuaji vishindwe kuwakemea.
Lakini wanasahau kuwa Upinzani ni movement ya kupinga utawala mbovu. Vyama vya siasa na wanasiasa ni sehemu tu ya hiyo movement. Wataendelea kupingwa tu kwa maovu yao, bila kujali uko CCM, UKAWA au bila chama. Wanapoteza pesa za umma bure, movement hii haitegemei chama au mtu fulani.
 
Taasisi ya dikteta uchwara hii, kama hataki kitu kichunguzwe hakichunguzwi ushahidi huu hapa chini.
Kalewa madaraka huyu uchwara.

Takukuru yachunguza Sh10 milioni za wabunge CCM
Tena bila aibu wakatangaza kuachana na kesi ya rushwa. Ingekuwa busara Mkurugenzi wa Takukuru angejiuzuru. Lazini kwa sababu ya uchumia tumbo, yupo tu akitafuna fedha zetu za mshahara na marupurupu.
 
Back
Top Bottom