TAKUKURU mnataka ushahidi gani katika rushwa za uchaguzi?!

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,793
12,238
Takukuru yatangaza vita
Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Eunice Mmari alipoulizwa jana kuhusu madai hayo alikiri kuwa na taarifa za baadhi ya wagombea na mawakala wao kutoa rushwa na kusema taasisi hiyo imesambaza vijana wake katika kila kona ya mji huo.
Alisema tangu juzi usiku, wamekuwa wakizunguka usiku na mchana kwenye mahoteli na vijiwe vinavyoaminika kutumiwa na wagombea na wapambe wao lakini hawajafanikiwa kuwakamata.
“Taarifa tunazo tangu jana (juzi), hatujalala mimi na vijana wangu tumekesha kuzunguka kila kona lakini tatizo tunalokumbana nalo ni kwamba wale wanaopokea fedha hizo hawataki kutoa ushirikiano,” alisema.
Aliwataka wabunge na watanzania wenye uzalendo na nchi yao kuipatia taasisi hiyo taarifa za siri za watu wanaotoa fedha hizo na wale wanaozisambaza akiwahakikishiwa kwamba majina yao yatalindwa.
“Nawaomba wabunge watusaidie katika hili kwa sababu wao ndiyo walengwa kwa kuwa ndiyo wanaopiga kura. Kama ni kufuatwa wao ndiyo wanaofuatwa lakini sisi Takukuru hatutakubali nchi iwakilishwe na wala rushwa,” alisema Mmari.

Source: Mwananchi

Katika chaguzi mbalimbali za hivi karibuni rushwa imekuwa ikipigiwa sana kelele lakini hakuna hata mmoja aliyekamatwa na kufikishwa mahakamani!

  1. Nini kifanyike kukomesha rushwa hizi Tanzania?
  2. Je kuna umuhimu wo wote wa TAKUKURU kuendelea kuwepo au ni sehemu ya ulaji tu?
 
Ukweli kama CHADEMA au chama kingine makini cha upinzani wagombea wake wangekuwa wana honga hapo ndo ungewajua TAKUKURU, lakini kwakua wahongaji ni magamba, huwezi sikia mtu kakamatwa unless wawe hawampendi na kutaka kumtoa kwenye system yao, kama walivyo mafanyia Mwakalebela kure Iringa (ili tu yule mama apitishwe) na bwana Mungai wa Mufindi, huwezi kutofautisha CCM na rushwa na wao ndo wanaoimiliki TAKUKURU, au hamkumbuki maneno ya Dr Hosea alipoongea na wikeleaks?
 
Ni vema basi TAKUKURU waka-declare interest!
 
Ndg zangu hapa hakuna cha takukuru wala bibi yake takukuru wote hawa ndo wale wale waliiweka tu kutafutiana ajira wao na watoto wao,kwanza hao ndo wala rushwa namba moja .nyani akamkamate ngedere kwa wizi mahindi hajawahi tokea?
 
..anataka taarifa ili awatonye...janja ya jusii kusa juaa nana mmariii...acha longo longoo
 
Ukweli kama CHADEMA au chama kingine makini cha upinzani wagombea wake wangekuwa wana honga hapo ndo ungewajua TAKUKURU, lakini kwakua wahongaji ni magamba, huwezi sikia mtu kakamatwa unless wawe hawampendi na kutaka kumtoa kwenye system yao, kama walivyo mafanyia Mwakalebela kure Iringa (ili tu yule mama apitishwe) na bwana Mungai wa Mufindi, huwezi kutofautisha CCM na rushwa na wao ndo wanaoimiliki TAKUKURU, au hamkumbuki maneno ya Dr Hosea alipoongea na wikeleaks?

na herbert mtangi je?
 
Back
Top Bottom