TAKUKURU Mara yaokoa Tsh. Milioni 600 zilizokusanywa kupitia jina la Rais kujinufaisha kipindi cha Uchaguzi Mkuu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,539
TAKUKURU mkoani Mara wamebaini watu wanaotumia jina la Rais Magufuli kujinuifaisha katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ambapo taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa zaidi ya Tsh. milioni 600 ambazo zilikuwa zimekusanywa kupitia jina la Rais Magufuli na uchunguzi unaendelea

Mkuu wa Mkoa Mara, Adam Malima amesema hatokubali hii tabia mkoani kwake kufanyika, Mzee wa watu kasema hajatuma mtu kuja kugombea

Malima.jpg
Mara.jpg
 
Kina nani walikuwa nazo? walizipata wapi? kivipi?mbona hao wezi hamuwapeleki mahakamani? kuokoa pesa bila kuadhibu wezi ni sifa za kijinga tu bora msingeandika hapa jukwaani!! mpelekeeni Magu majina ya wezi na pesa hiyo!
 
Kama picha zinaendana na maandishi, nina mashaka makubwa sana kama habari hii ni kweli? Kama ni kweli basi kuna namna ya upigaji, kwani iweje minoti imefungwa kibenki na kuonesha zimetokea benki na zimechangwa na watu wengi? Ingekuwa kugawiwa watu ni sawa baada ya ku-withdraw, lakini kukusanya na mikanda ya benki!?
 
Hivi TAKUKURU wakikamata fedha kwa kuzi-withdraw kutoka benki wanazipeleka kwa mkuu wa mkoa?
 
Back
Top Bottom