TAKUKURU mnapofumbia macho Rushwa ya Trafiki mnazidi kuwachonganisha wanyonge na Serikali

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Nadhini mnaopita barabarani mtakuwa shahidi kwamba Sasa hivi Rushwa si siri tena. Unapanda bajaji wanalalamika kuna maeneo wanatoa elfu mbili kwa siku na maeneo mengine elfu moja kwa siku.

Daladala kila siku lazima watoe kuanzia elfu mbili Hadi tano kwa siku na usipotoa gari Yako haitafanya kazi. Ninachosikitika ni kwamba tunaopita barabarani tunaona daladala zikisimama na Makondakta kuzunguka nyuma nakutoa rushwa yao kisha kuwasha gari na kuendelea na safari.

Wakati Sisi tunayaona haya tunajiuliza Watumishi wa TAKUKURU wao awapandi dalala, bajaji au mabasi? Kama wanapanda wakiona matukio kama haya wanajisikiaje hasa wakikumbuka wanalipwa kudhibiti hii hali?

Lakini tuseme basi wao ni familia Bora awaruhusiwi kupanda public transport , wakiwa kwenye magari Yao hii Hali ndo awaioni?

Ukipiga mahesabu unaweza ukabaini ukibwa wa rushwa hii

1. Tuseme Kwa siku bajaji elfu Tano zitoe 3000 Kwa mwezi (Tshs3000*30Dys*5000Bajaji). Hapa utabaini Kila bajaji Kwa mwezi inatoa rushwa ya 90,000, lakini Kwa mwezi mmoja Bajaji 5000 zitatoa rushwa ya 450,000,000. Je hizi babaji unaweza ukaKuta zipo wilaya Moja TU ya Dsm. Nchi nzima Kwa mwezi bajaji zinatoa rushwa ya shs ngapi?

Hapo Kuna malori, mabasi, daladala na pikipiki pamoja na gari binafsi. Hii rushwa inapokelewa na watu ambao tayari wameajiriwa wakiwanyonya ambao awajaajiriwa. Naomba nieleze madhara ya hii hali

1. Moja ya eneo linalochangia unyonge wa watoa rushwa ni kukosa kuwa na lesini . Faida inayotokana na rushwa hii ni kubwa kwa Askari na matokeo yake utoaji wa lesini za kuendesha vyombo vya moto unasuasua Ili kundi kubwa zaidi likose vigezo na hivyo Kila ukikamatwa lazima utoe Fedha.

2. Rushwa hii imewafanya vijana wengi kushindwa kujiajiri, kama polisi atachukua 90,000 kwa kijana anayetakiwa kupeleka Lakini 4+ Kila mwezi Kwa tajiri unadhani vijana wangapi wataweza kujiajiri?

3. Rushwa hii imekuwa chanzo cha ajali za barabarani, mtu hana sifa anatoa pesa anaendelea kuendesha chombo cha moto matokeo yake anaua na trafic yuleyule aliyepokea rushwa anaenda kupima ajali bila hata kuumia nafsi.

Ushauri wangu: Mhe. Rais fanya maamuzi magumu Kwa maslahi ya wale wasio na ajira. Tupe kazi wananchi tukuletee picha za ushahidi wa trafic Wala rushwa. Ukizipata hizo picha kupitia njia utakayotoa usimfunge trafic yeyote bali elekeza afukuzwe kazi mara moja aje uraiani akawa Dreva daladala au bajaji then nafasi zitakazopatikana tuajiri watu wapya walioko uraiani. Hapo ndipo waajiriwa watatambua kwamba mshahara Wanaolipwa ni mkubwa au unatosha.

2. Mfumo wa utoaji leseni uboreshwe na urahisishwe na ipitishwe sheria kwamba hakuna mmiliki wa chombo Cha moto ataruhusiwa kumkabidhi chombo chake mtu asiye na leseni. Vijana watakuja kuchukua leseni na serikali itaingiza mapato.

3. Ruhusuni madreva watume taarifa na namba za maaskari wala Rushwa kupitia namba maalumu ambavyo inaficha taarifa za mtoa taarifa.

Tunatatizo la ajira ila tatizo Ili linachangiwa zaidi na waajiriwa. Wanataka mshahara wa serikali na Bado Wanataka kutunyanyasa tusio na kazi za umma.
 
Chukua hatua badala ya kuwalaumu TAKUKURU. Kwani kupiga picha ya uhalifu unaotokea mpaka uruhusiwe? Ukikuta wezi wanavunja nyumba yako au ya jirani utawaacha ukisubiri polisi? Mapambano ya uhalifu ikiwemo rushwa ni jukumu la kila Mtanzania hasa mzalendo.
 
Kuna trafiki huwa wanatega maeneo ya Victoria karibu kabisa na jengo la TanHouse, ni wala rushwa hawafai...
 
Rushwa haiwezi kwisha sababu gari nyingi zina vipengele kibao.

Na madereva pia asilimia kubwa leseni hawana ndio mana mambo yanaisha kimya kimya.

Coz mtu anaposimamishwa tyr anajua ana kosa so kutoa efu 2 sio ishu kwa dereva suala la efu 2 inaenda wapi hyo ishu ingine
 
Back
Top Bottom