TAKUKURU kuwashitaki watu 4 kwa Rushwa na Uhujumu Uchumi, watatu ni waliokuwa wafanyakazi wa Bandari (TPA) pamoja na mfanyabiashara 1

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
Watuhumiwa watatu ambao walikuwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) tayari wamefukuzwa kazi

Mtu wa nne ni mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni M/S Ntinyako Company Ltd. Iliyokuwa ikipewa zabuni ya usambazaji wa vifaa vya ujenzi na miundombinu ya maji katika Bandari ya Kigoma.

Uchunguzi wa TAKUKURU umegundua kuwa watuhumiwa hao wametenda makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ikiwemo: Kuongoza genge la uhalifu, Ubadhirifu na Ufujaji, Ukwepaji Kodi, Utakatishaji wa fedha haramu, Kuisababishia mamlaka hasara

====

Washitakiwa wanakabiliwa na Kesi ya Uhujumu Uchumi Na. 5/2020.

Kesi yao inahusisha makosa ya: -

1. Kuongoza genge la uharifu kinyume na Aya ya 4(1)(d) ya Jedwali la Kwanza likisomwa pamoja na vifungu vya 57(1) na 60(2) Vya Sheria ya Uhujumu Uchumi sura ya 200 kama ambavyo imefanyiwa marejeo mwaka 2002.

2. Ufujaji na ubadhirifu kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa No.11/2007.

3. Kuisababishia Mamlaka Hasara Kinyume na Aya ya 10(1) ya Jedwali la Kwanza likisomwa pamoja na kifungu cha 57(1) na 60(2) Vya Sheria ya Uhujumu Uchumi, Sura ya 200 kama ambavyo imefanyiwa marejeo mwaka 2002.

4.Kushindwa kulipa kodi kinyume na kifungu cha 83(a) cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi Namba 10 ya Mwaka 2015. Na

5. Kutakatisha fedha Kinyume na kifungu cha 12(a) na 13(a) Cha Sheria ya Kuzuia Utakatishaji Fedha No. 12 ya Mwaka 2006 ikisomwa pamoja na Aya ya 22 ya Jedwali la Kwanza la vifungu vya 57(1) na 60(2) Vya Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 kama ambavyo imefanyiwa marejeo Mwaka 2002.

Kesi ipo Mbele ya Mheshimiwa Kenneth Mtembei, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kigoma.

Kesi itakuja Kwa hatua ya kutajwa tarehe 26/10/2020. Ahsante.

1.jpg



2.jpg
3.jpg
 
Utawasikia Chadema ..."serikali imeharibu sekta binafsi...." Makampuni binafsi yaliyokufa ni haya haya kama M/S Ntinyako Company Limited...wapigaji wakisaidiwa na watumishi wa Umma majambazi!
 
mbona zamani hizi kesi za money laundering na kuhujumu uchumi hazikukithiri kama ilivo sasa ?

ai sasa hv imekua ni kukomoana ?
 
Back
Top Bottom