nyundo2017
JF-Expert Member
- Sep 7, 2017
- 1,439
- 859
Afisa wa TAKUKURU mbaroni kwa kumbaka mtoto wa dada yake
Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Rukwa, Jonas Jackson (34) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumbaka na kisha kumlawiti mtoto wa dada yake aliyekuwa akiishi naye. Ofisa huyo alikamatwa Februari 7, 2019 baada ya mtoto huyo kwenda kuripoti kituo kikuu cha...
www.jamiiforums.com
Ukisoma hapa mtuhumiwa alisingiziwa kesi na boss wake ambaye alikuwa ni mkuu wa takukuru mkoa wa rukwa ndugu hamis mwenda kwa ugomvi wao binafsi juu ya mwanamke.
Kwa kutumia cheo chake na kwa kuwatumia rco na mwendesha mashitaka wa mkoa wa rukwa kwa jina Silaji pamoja na jaji mfawidhi aliyestafu mlango kwa pamoja walimshikilia mtuhumiwa polisi kwa muda mrefu na baadae walimfunga mtuhumiwa kwa hila ili kuunga umoja wao.
Chakushangaza mtuhumiwa alifukuzwa kazi na takukuru kwa uonevu kabla hata ya kesi kusikilizwa kama ilivyokawaida yao na baadae aliposhinda kesi hiyo alirudishwa kazini kinyemela tu pasipo kuangalia athari zilizojitokeza na mhusika aliyesababisha hajachukuliwa hatua yeyote.
Pamoja na jaji mfawidhi msatafu mlango kusitafu na mwendesha mashitaka wa mkoa Salaji kuhamishwa na Mkuu wa takukuru mkoa rukwa mwenda kuhamishwa bado kuna watu wameumizwa na watu hawa kwa maana hiyo hata walikohamishiwa hao wawili bado watakuwa na madhara pia.
Watu wameka sana mahabusu kwa hira zao hadi ujio wa kaimu jaji mfawidhi mh. Mkeha na kuzifuta baadhi ya kesi zisizo na mashiko ingawa bado kuna kesi hazina mashiko ziko mahakamani.
Mh Rais Samia kwa huruma zako tunashauri iundwe tume huru kufuatilia kesi za watuhumiwa walioko mahabusu na zinazoendelea kwani ni wazi kwa mahakama hii hakuna haki itakayopatikana hakika.