TAKUKURU kumhoji Maalim Seif

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
20,056
23,509
SEIF SHARIF HAMAD KUIELEZA MAMLAKA YA KUPAMNANA NA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI ZANZIBAR WALIOJIPATIA UTAJIRI WA HARAKA KATIKA SERIKALI ILIOPITA NA KUWEKA FEDHA NJE YA NCHI.

Akizungumza na Nipashe Jumapili jana, Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Mussa Ali, alisema watamhoji kiongozi wa upinzani na Katibu Mkuu huyo wa Chama cha Wananchi (CUF), ili kusaidia uchunguzi dhidi ya madai yake.

Alisema wanataka awasaidie taarifa za vigogo hao wanaomiliki fedha chafu nje ya nchi ili wachukuliwe hatua za kisheria.

“Tumeunda timu maalum ya kuchunguza tuhuma kama hizo kwa madhumuni ya kuchukua hatua za kisheria pale tunapopata ushahidi wa kutosha hivyo
tutamhoji Maalim Seif,” alisema Mussa.

Akizungumza na waandishi wa habari Shangani mjini Zanzibar wiki iliyopita, Maalim Seif alisema kuna viongozi wengi wa SMZ ambao wameficha fedha chafu nje ya nchi.

Alizitaka Jumuiya za Kimataifa kufuatilia akaunti za viongozi hao nje na kuwachukulia hatua za kisheria.

Madai ya Maalim Seif yalikuja katika kipindi ambacho dunia imegubikwa na kashfa ya 'Nyaraka za Panama' ambapo viongozi mbalimbali mashuhuri duniani, akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroon wamegundulika kuficha fedha kwenye nchi hiyo ya Panama.

Waziri Mkuu wa Iceland, Sigmundur Gunnlaugsson alijiuzulu nafasi hiyo Aprili 5 kutokana na maandamano ya kumtaka awajibike baada ya jina lake kuwa mmoja wa watu waluioficha fedha Panama.
 
Jamani waache kuyafukua wengine tupumue.
tatizo siasa za Znz ni zaidi ya '' nyengine "

Wengi wanacheza ngoma waioijua....
wajuzi na wajanja wanachochea kuni tu..

Haya na tuyaone....
 
Back
Top Bottom