TAKUKURU kuchunguza kuhusika kwa Rais wa TFF kwenye ubadhilifu wa fedha CAF

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,282
2,000
Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU imefanya mawasilino na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), ili kuchunguza ushiriki wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia katika kashfa ya ubadhilifu wa fedha iliyomuweka hatiani aliyekua Rais wa CAF Ahmad Ahmad.

Kamati ya maadili ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) juzi Jumatatu (Novemba 23), ilimfungia miaka mitano Ahmad Ahmad kutojihusisha na masuala ya soka kutokana na kashfa ya ubadhilifu.

Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinadai kuwa, Rais wa TFF Wallace Karia huenda akawa miongoni mwa wanufaika kwa kupata mgao wa dola 20,000, kutoka kwa Ahmad Ahmad.

“Tumewasiliana na CAF, tumeanza uchunguzi, unajua hili suala ni jipya na ndio kwanza tumeanza uchunguzi, siwezi kuahidi itachukua muda gani, lazima kila hatua izingatiwe kwenye uchunguzi huu ili kama Wallace Karia amehusika na wote walionufaika na ubadhirifu huo waweze kubainika na kuchukuliwa hatua za kisheria” amesema Brigedia John Mbungo – Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.

Hata hivyo tayari Shirikisho la soka nchini TFF limekanusha madai ya kuhusishwa kwa Rais wao Wallace Karia katika kashfa hiyo kwa kuandika barua iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari jana
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
6,349
2,000
Hao TAKUKURU ni makakanja tu, hawana jipya wala maana.

Walipaswa kutuambia kwanza lile sakata la uchunguzi wa kutafunwa pesa zilizotolewa na Rais Magufuli kuwezesha mashindano ya kandanda ya vijana afrika kufanyika Tz liliishia wapi?
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,461
2,000
Umbea umewazidi.

Wanakimbilia kufatilia ya mbali, yasiotuhusu, wakati la "WABUNGE WA CHADEMA WA VITI MAALUM 19" kuapishwa bila chama kuwateua hawajatoa tamko lolote.

Hii nchi imenajisiwa kweli.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom