TAKUKURU kuchunguza kuhusika kwa Rais wa TFF kwenye ubadhilifu wa fedha CAF

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,246
2,000
Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU imefanya mawasilino na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), ili kuchunguza ushiriki wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia katika kashfa ya ubadhilifu wa fedha iliyomuweka hatiani aliyekua Rais wa CAF Ahmad Ahmad.

Kamati ya maadili ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) juzi Jumatatu (Novemba 23), ilimfungia miaka mitano Ahmad Ahmad kutojihusisha na masuala ya soka kutokana na kashfa ya ubadhilifu.

Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinadai kuwa, Rais wa TFF Wallace Karia huenda akawa miongoni mwa wanufaika kwa kupata mgao wa dola 20,000, kutoka kwa Ahmad Ahmad.

“Tumewasiliana na CAF, tumeanza uchunguzi, unajua hili suala ni jipya na ndio kwanza tumeanza uchunguzi, siwezi kuahidi itachukua muda gani, lazima kila hatua izingatiwe kwenye uchunguzi huu ili kama Wallace Karia amehusika na wote walionufaika na ubadhirifu huo waweze kubainika na kuchukuliwa hatua za kisheria” amesema Brigedia John Mbungo – Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.

Hata hivyo tayari Shirikisho la soka nchini TFF limekanusha madai ya kuhusishwa kwa Rais wao Wallace Karia katika kashfa hiyo kwa kuandika barua iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari jana
 
rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
8,265
2,000
TFF wapumbavu baada ya kutoa taarifa ya kujikosha walitishia kumchukulia hatua yeyote atakayehoji waichukulie hatua pccb sasa lakini pccb wanatakiwa waombe taarifa fifa na sio caf
 
joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
6,437
2,000
Soka lipo letu deep,yaani Simba,Yanga na baba yao TFF kwenye swala hela ukichunguza lkn utabaki na walakini.
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
4,616
2,000
TFF wapumbavu baada ya kutoa taarifa ya kujikosha walitishia kumchukulia hatua yeyote atakayehoji waichukulie hatua pccb sasa lakini pccb wanatakiwa waombe taarifa fifa na sio caf
Wale wajinga tu, hata ukisoma maelezo yao waliyoyatoa hayaeleweki!! Eti alizitoa hizo dola 20,000 kusaidia shirikisho!!! Sasa huo mkwara wa kuwashitaki wawashitaki shirika la habari la REUTERS, ndio lilioitaja TZ, kama wana ubavu huo!!!
 
KANYIMBI

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
886
1,000
Wakati Karia anachunguzwa. Nashauri Jamal Malinzi au Abas Tarimba akaimu nafasi ya Rais wa TFF kwa muda hadi ligi itakapoisha.
 
Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,087
2,000
Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU imefanya mawasilino na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), ili kuchunguza ushiriki wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia katika kashfa ya ubadhilifu wa fedha iliyomuweka hatiani aliyekua Rais wa CAF Ahmad Ahmad.

Kamati ya maadili ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) juzi Jumatatu (Novemba 23), ilimfungia miaka mitano Ahmad Ahmad kutojihusisha na masuala ya soka kutokana na kashfa ya ubadhilifu.

Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinadai kuwa, Rais wa TFF Wallace Karia huenda akawa miongoni mwa wanufaika kwa kupata mgao wa dola 20,000, kutoka kwa Ahmad Ahmad.

“Tumewasiliana na CAF, tumeanza uchunguzi, unajua hili suala ni jipya na ndio kwanza tumeanza uchunguzi, siwezi kuahidi itachukua muda gani, lazima kila hatua izingatiwe kwenye uchunguzi huu ili kama Wallace Karia amehusika na wote walionufaika na ubadhirifu huo waweze kubainika na kuchukuliwa hatua za kisheria” amesema Brigedia John Mbungo – Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.

Hata hivyo tayari Shirikisho la soka nchini TFF limekanusha madai ya kuhusishwa kwa Rais wao Wallace Karia katika kashfa hiyo kwa kuandika barua iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari jana
Hivi ile B aliyoitoa mheshimiwa Rais Magufuli uchunguzi unaendeleaje?
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,885
2,000
Msomali hana mshahara. Anajilipa kwaujanjaujanja mwingi. Kaweka kibaraka Mrundi awe Mtendaji Mkuu wake
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom