TAKUKURU Je, ni sahihi aichofanya Mkurugenzi wa Kasulu?

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,111
2,000
Mkurugenzi wa Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma Fatna Laay amekataa kutumia fedha zote shilingi milioni 210 alizopewa kwa ajili ya kujinunulia gari lake la kazi na badala yake amenunua gari la Milioni 162 na fedha iliyobaki amewanunulia pikipiki Watendaji wa Kata 12.

Swali: Je, alichofanya ni sahihi, hakuna kanuni au sheria amezikiuka hapa?
 
Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
2,741
2,000
Dah mkuu

Huoni Kama katumia busara sana kuna mmoja huko kanda ya ziwa aligombana na msukuma juu ya ununuzi wa v8 kwa gharama

Binafsi nampongeza Bi fatna

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ndalilo

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
2,065
2,000
Muhimu ni kuwa hajafuja, kidogo alichopata, kagawana na wenzake, hakuna kanuni iliyokiukwa, well done.

Wabunge waige, ile milioni kadhaa ya gari wasaidie sehemu moja wapo jimboni
 
Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
30,375
2,000
Muhimu ni kuwa hajafuja, kidogo alichopata, kagawana na wenzake, hakuna kanuni iliyokiukwa, well done.

Wabunge waige, ile milioni kadhaa ya gari wasaidie sehemu moja wapo jimboni
Wabunge Gani? Hawa Wanaosema Posho Hakitoshi Tusiwaogope Wananchi Tuwaambie Ukweli πŸ˜…πŸ˜„πŸ˜ƒπŸ˜‚πŸ˜πŸ˜πŸ˜€ Wabunge Wa Tozo!πŸ˜πŸ™„πŸ˜ΆπŸ˜‘
 
Paf

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,715
2,000
Kwanza hayo magari kwa wakurugenzi ya bei kubwa yanini.
Wangetumia RAVA 4 au PRADO
Wao mda mwingi ni ofisini nyumbani.

Unakusanya 1000 kila Siku kwa muuza mboga halafu unanunua gari la kifahari.
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,415
2,000
Mkurugenzi wa Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma Fatna Laay amekataa kutumia fedha zote shilingi milioni 210 alizopewa kwa ajili ya kujinunulia gari lake la kazi na badala yake amenunua gari la Milioni 162 na fedha iliyobaki amewanunulia pikipiki Watendaji wa Kata 12.

Swali: Je alichofanya ni sahihi, hakuna kanuni au sheria amezikiuka hapa?
Sio sahihi kwasababu magari ya serikali yana technical specifications zake na sio kukurupuka tu.

Ndio tatizo la watu kuingilia kazi za watu wengine! Haya ndio madhara yake. Halafu kiutaratibu yeye na wengine, hawatakiwi kabisa kuingilia haya mambo yaani anakabidhiwa tu dereva na gari! Maana ni Mali ya serikali sio Mali binafsi
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,415
2,000
Pili, kama wanaweza kucheza na specs ambazo ziko approved na wataallam wa manunuzi na mambo ya usafiri basi wana uwezo pia wa kucheza nazo wakanunua gari ya bei ya juu zaidi kwa specs za gari ya bei halisi!

Ni muda na muktadha tu
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,647
2,000
Uongozi ni kufuata taratibu pamoja na kutumia busara

Mkurugenzi kafanya jambo jema
mama D acha kuchanganya madesa bhana! Inawezekana kweli huyo Mkurugenzi amefanya jambo jema na la busara kugawana hizo hela na hao Watendaji kwa kununua hilo gari la bei nafuu na pikipiki!

Ila kwenye kufuata taratibu, nadhani hapo hakufuata! Maana alitakiwa kununua gari la milioni 210! Na siyo la milioni 162!

Ila hii nchi haina usawa hata kidogo!! Yaani yeye amejinunulia gari la milioni 162, halafu Watendaji pikipiki za milioni 2!! πŸ™„
 
Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
7,647
2,000
Mkurugenzi wa Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma Fatna Laay amekataa kutumia fedha zote shilingi milioni 210 alizopewa kwa ajili ya kujinunulia gari lake la kazi na badala yake amenunua gari la Milioni 162 na fedha iliyobaki amewanunulia pikipiki Watendaji wa Kata 12.

Swali: Je alichofanya ni sahihi, hakuna kanuni au sheria amezikiuka hapa?
Sio vizuri hata kidogo yaani anashindwa kununua hata gari la millioni 20 ananunua mia na kitu.
 
Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,111
2,000
Sio sahihi kwasababu magari ya serikali yana technical specifications zake na sio kukurupuka tu.

Ndio tatizo la watu kuingilia kazi za watu wengine! Haya ndio madhara yake. Halafu kiutaratibu yeye na wengine, hawatakiwi kabisa kuingilia haya mambo yaani anakabidhiwa tu dereva na gari! Maana ni Mali ya serikali sio Mali binafsi

Hapa ndipo ilipo Mantiki yangu. Amefanya kama vile gari la kwake
 
August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,321
2,000
Mkurugenzi wa Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma Fatna Laay amekataa kutumia fedha zote shilingi milioni 210 alizopewa kwa ajili ya kujinunulia gari lake la kazi na badala yake amenunua gari la Milioni 162 na fedha iliyobaki amewanunulia pikipiki Watendaji wa Kata 12.

Swali: Je, alichofanya ni sahihi, hakuna kanuni au sheria amezikiuka hapa?
Ukiwa ni mkweli toa hiyo specification la gari la 210m na uweke specification ua hilo la 162m, ndio tunaweza kuchambua kuliko kusema la budget ya 210m dhidi ya matumizi halisi ya 162m
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom