Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,174
- 4,062
TAKUKURU inamshikilia Meneja wa Bandari ya Kipumbwi, Stephen Elly Mbakweni kwa kuomba na kushawishi Hongo ya Tsh. 900,000 kutoka kwa mteja wake ili aweze kumruhusu kusafirisha mzigo kutoka Handeni kwenda Zanzibar kupitia Bandari hiyo.
Uchunguzi wa TAKUKURU umebaini kuwa Meneja huyo aliomba na kushawishi hongo hiyo baada ya mteja wake kumpatia nyaraka zote za malipo zilizohitajika na zinazoonesha alitekeleza taratibu zote kwa mujibu wa Sheria ili asafirishe mzigo wake.
Nyaraka hizo zilikataliwa na Meneja Stephen kwa madai kwamba hazitambui, huku akiwa na lengo la kushawishi apewe hongo ya Tsh. 900,000 ili aweze kuruhusu mzigo huo upite katika bandari hiyo.
Baada ya TAKUKURU kupokea taarifa hizo ilianza kumfuatilia Meneja huyo na kumuwekea mtego ambapo ilifanikiwa kumkamata kwa kupokea Tsh. 270,000 kutoka kwa mteja huyo aliyemuomba ashushe kutoka Tsh. 900,000. Atafikishwa Mahakamani baada ya Uchunguzi.