Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Matokeo yapingwa uchaguzi wa Wenyeviti
Matokeo ya uchaguzi wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza, yamepingwa katika wilaya nne kati ya saba za Mkoa wa Mwanza kutokana na madai ya kugubikwa na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi.
Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Acheny Maulid alitaja wilaya ambazo matokeo yake yamewekewa pingamizi kuwa ni Magu, Nyamagana, Misungwi na Sengerema.
Aliwataja wenyeviti ambao ushindi wao unapingwa ni Zebedayo Athumani kutoka Nyamagana, Daudi Gambadu (Misungwi), Zabloni Makoye (Magu) na Agostine Makoye wa Sengerema.
“Vikao husika vitakutana kujadili na kuamua pingamizi hizo kwa mujibu wa katiba na kanuni za uchaguzi ndani ya chama,” amesema Maulid.
Na David Nyembe