TAKUKURU: CHADEMA badala ya kulalamika wanapaswa kusoma sheria, mwisho wa uchunguzi waweza kuwa mwanzo wa uchunguzi mwingine

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,779
141,667
Mkurugenzi mkuu wa Takukuru amewajibu Chadema kwa kuwataka wakasome vizuri sheria ya kupambana na rushwa kabla ya kulalamika.

Mkurugenzi amesema taasisi yake inafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na anaamini Chadema wakisoma sheria hawatalalamika tena kwani watajua utaratibu wa uchunguzi ulivyo.

Kadhalika amesisitiza kuwa mwisho wa uchunguzi mmoja inaweza kuwa mwanzo wa uchunguzi mwingine kulingana na kile kinachochunguzwa na yale yaliyobainishwa katika uchunguzi wa kwanza.

1593778910788.png

1593778936578.png

1593778957738.png
 
Haya. Tusubiri. Yetu masikio na macho. Vitajulikana tu mbele kwa mbele. Hila na heri havifichiki.
 
Kuwa na uchunguzi mwingine baada ya wa mwanzo kukamilika sio tatizo, tatizo ni uchunguzi huo mpya, unafanywa kwa kificho? je CDM waliambiwa tuhuma zao? Je walipewa muda wa kuzijibu? Je due process and natura justice zilifuatwa? Inataka kwamba kama unamchunguza mtu, unamwambia unamchunguza kwa reasonable suspicion ipi na kimaandishi na ndio sasa unapomwambia akupe nyaraka A, B,C. Hwezi anza omba nyaraka kabla ya tuhuma... hakuna kitu kama hicho duniani humu kwa nchi zote zinazofuata mfumo wa " you're innocent till proven guilty".

Takukuru wangeeleweka zaidi kama tungekuwa na mfumo wa - " you are guilty until you are proven innocent "... labda kwa sababu ni mwanajeshi na kazoe amri amri basi anajua kwamba amri hizo pia zinafanya kazi uraiani...
 
Mkurugenzi mkuu wa Takukuru amewajibu Chadema kwa kuwataka wakasome vizuri sheria ya kupambana na rushwa kabla ya kulalamika.

Mkurugenzi amesema taasisi yake inafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na anaamini Chadema wakisoma sheria hawatalalamika tena kwani watajua utaratibu wa uchunguzi ulivyo.

Kadhalika amesisitiza kuwa mwisho wa uchunguzi mmoja inaweza kuwa mwanzo wa uchunguzi mwingine kulingana na kile kinachochunguzwa na yale yaliyobainishwa katika uchunguzi wa kwanza.

Chanzo: ITV digital
Wanao tu mama kieleweke kabla ya uchaguzi, ila Bajaj za Iringa bado zinafanyiwa utafiti kama zipo kweli.
 
Back
Top Bottom