TAKUKURU Arusha Yawaburuza Mahakamani watumishi watano wa Tanesco kwa kukwapua milioni 387.1

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
610
1,000
Taasisi Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha imewafikisha mahakamani watumishi watano wa shirika la umemeTanesco mkoani hapa kwa makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kwa kusababisha upotevu wa fedha sh, milioni 387.1

Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake Mkuu wa Takukuru Mkoani hapa James Ruge amewataja Watuhumiwa hao kuwa ni Maria Mwakabage aliyekuwa afisa Ugavi na usafirishaji Mwandamizi.

Wengine ni Zipporah Dedu(Mtunza Stoo),Ruth Dedu(Mtunza Stoo),Florencia Nyambari(Mtunza Stoo msaidizi) na Michael Gumbo (Mtunza Stoo msaidizi).

Ruge alisema kuwa Takukuru kwa kushirikiana na ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali imewapandisha kizimbani Watuhumiwa hao katika mahakama ya hakimu Mkazi Arusha iliyopo Sekei ,wilayani Arumeru.

Alifafanua kwamba watuhumiwa hao wakiwa wafanyakazi wa shirika Hilo la umma walisababisha upotevu wa shilingi mil.387,167,413/-na baadaye kuingiza taarifa za uongo kwa Mfuko wa kutunza kumbukumbu za bohari kwa lengo la kufichua ukweli wa Mali zilizopotea.

Watuhumiwa hao wamesomewa mashtaka matatu likiwemo la uhujumu uchumi kwa makosa ya kuisababishia hasara Serikali kinyume Cha sheria.

Kosa jingine ni kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri pamoja na Wizi .

Watuhumiwa wote wamepelekwa mahabusu ya gereza kuu la Arusha kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Takukuru Mkoani hapa imewaasa watumishi wa umma kuepuka kujihusisha na vitendo vya Rushwa kwani watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria .
 

nra2303

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
2,913
2,000
Wangeanza na tetesi za upigaji wa Bashiru na Dotto ndio ningewaona wanafanya la maana,yale yale wanahangaika na dagaa mapapa yanawaangalia tu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom